BOT kushusha riba za mikopo ni mpaka waagizwe ili hali wao ndio wataalam wa kushauri zishuke?

BOT kushusha riba za mikopo ni mpaka waagizwe ili hali wao ndio wataalam wa kushauri zishuke?

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Suala la kushusha riba nchi hii linaonekana kufanyika kutokana na maagizo ya wanasiasa (liko kisiasa) na si Benki Kuu kama wataalamu kushauri au kushusha riba kwa mabenki ili nayo yashushe riba kwa wananchi.

Kwa mfano, leo Mama kaagiza Benki Kuu kuhakikisha mabenki yanashusha riba kufika chini ya asilimia 10 (jambo jema na la kupongeza).

Swali langu ni je, Benki Kuu kama wataalamu, huwa hawaoni umuhimu wa kushusha riba mpaka waagizwe na wanasiasa?

Katika hili, si BOT kama wataalamu ndio wa kushauri wanasiasa waridhie BoT kushusha riba kama BoT hawana mamlaka hayo mpaka wapete idhini ya watawala?

Kama tatizo ni sherai na taratibu, je hatuoni sheria na taratibu hizo zinastahili kufanyiwa marekebisho?

Mambo ya ajabu sana haya!
 
BOT ndio wanaotoa leseni na ku regulates hizo taasisi za kifedha zanazotoa mikopo kwa hiyo wanawamudu vizuri tu, hayo mabenki yanaumiza sana wakopaji riba zipo juu sana wakati wao wanakopa kwa unafuu zaidi kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii.
 
Bank Kuu inawakopesha pesa, hawa commercial banks kwa interest, ambazo zinakuwa determined kwa forces ya demand and supply. Wao wanaipitisha kwa final consumer, kwa interest kubwa ili wapate faida.

Haya basi mama aongeze ruzuku huko BOT, ili commercial bank wapunguziwe riba. Na wao wapunguze riba kwa walaji. Its possible.
 
Ngoja tusubiri tuone kama watafanya, na hii mikopo tuliyonayo riba ipungue Ili tuwahi kumaliza tuchukue mingine nauhakika wakifanya hivyo Benki wajiandae kuzidiwa na sisi wateja wa mikopo na sijui kwa hili walikuwa wapi? Wakati msemo wa mama yetu kama Mwigulu anavyomuita mikopo imekatiwa bima na walipaji tunalipa sasa sijui walikwama wapi kuja na mkakati huo wa kuzungusha hizo hela kwenye Benki zao huku wakiongeza wateja kwa njia hizo.
 
.Bank kuu inawakopesha pesa, hawa commercial banks kwa interest, ambazo zinakuwa determined kwa forces ya demand and supply. Wao wanaipitisha kwa final consumer, kwa interest kubwa ili wapate faida.Haya basi mama aongeze ruzuku huko BOT ili commercial bank wapunguziwe riba.Na wao wapunguze riba kwa walaji. Its possible.
Demand and supply ama monetary policy? Sometimes hta demand ikiwa kubwa BOT inaweza lazimu benki zibadili rate ili kuendana na sera ya fedha ya wakati huo. Pengine mfumuko ni mkubwa, mzunguko mkubwa wa fedha (demand deposits + CC) n.k

Pia BOT haitegemei bank rate kucontrol/kupata pesa kutoka kwa mabenki. Inaweza uza hati fungani au kupandisha reserve ratio requirement ili ukwasi upungue. So it's not really about demand for credit but monetary policy ya wakati husika.

Cc Gerald .M Magembe
 
Punguza riba toka BOT had 2%
Punguza kodi kwa commercial bank had 10 au 15%

Halafu waambie riba zisizid 10% na haitakuwa na madhara kwetu sote
Hiki ulikoshauri kma kikifanywa kwa mkupuo huu, Inflation pamoja na kushuka kwa thamani ya shillingi dhidi ya dollar havikwepeki.

Nadhani BOT waelekezwe tu ila sio kupewa exact figures..ni hatari
 
.Bank kuu inawakopesha pesa ,hawa commercial banks kwa interest, ambazo zinakuwa determined kwa forces ya demand and supply. Wao wanaipitisha kwa final consumer ,kwa interest kubwa ili wapate faida.Haya basi mama aongeze ruzuku huko BOT ,ili commercial bank wapunguziwe riba.Na wao wapunguze riba kwa walaji.Its possible.
Ni wazi Mama hajui jukumu la serikali kwa BOT vinginevyo asingetoa hiyo kauli.
 
Inflation itatokeaje mkuu? Mbna walipopunguza interest ya BOT from 9% to 5% hakukutokea hio inflation?
Walipunguza ila je katika wakati huo hawakuuza hati fungani? Au hawakupandisha reserve ratio? Hawakupunguza currency in circulation? Vipi broad money (Forex Inclusive) haikupungua kwa wakati huo? Factor moja tu haipelekei inflation. Kma vitu vyote vikiwa constant afu ukashusha tu bank rate obviously italeta inflation long term sababu ukwasi utazidi hivyo currency in circulation itaongezeka... Hizo spillover effects zake zitaleta mfumuko wa bei tu sababu mzunguko utaongezeka kwa mkupuo. Ila ukiona wameshusha rate alafu hakuna mfumuko wa bei ujue tu monetary policy tools zingine bado zimeminywa ila wanaziachia taratibu taratibu
 
Ni wazi Mama hajui jukumu la serikali kwa BOT vinginevyo asingetoa hiyo kauli.
Jukumu la BOT analijua na anajua viongozi wengi kutoa maamuzi niwaoga wanasubiri waelekezwe ndo maana katoa maagizo Ili wajishughulishe kupunguzia wale wanahitaji hiyo mikopo wapate, Kwanza huko BOT hakuna haja ya riba maana huko pesa zinatuzwa tu kama mapambo, riba zibaki kwa wale wanaozikopesha Ili zikazungushwe kama zile talanta zilivyogawiwa Ili zikazalishwe zingine.
 
Hiki ulikoshauri kma kikifanywa kwa mkupuo huu, Inflation pamoja na kushuka kwa thamani ya shillingi dhidi ya dollar havikwepeki.

Nadhani BOT waelekezwe tu ila sio kupewa exact figures..ni hatari
Hakuna inflation hata zingekopeshwa bila riba ni pesa mtu ataenda kukopa Ili akazungushe kwenye maendeleo yake, inflation labda kama zingegawiwa bure kila nyumba bila watu kufanya kazi huku wakilipiwa mahitaji yao mengine na hizo pesa za bure zikawa akiba tu.
 
Mkuu lazima ufahamu mzunguko wa pesa kutoka BOT kuja kwa raia huwa unategemea OMO na mabenki ya biashara. Sababu benki zikiwa na pesa zitakopesha/zitawekeza n.k so mzunguko wa pesa utaongezeka mtaani mwisho wa siku mfumuko wa bei. Na ndio maana moja ya monetary policy tools za BOT mfano reserve ratio requirement, Bank rate, Directives, kuuza hati fungani n.k zote zimelengwa kwa benki za biashara ili kuweza kudictate jinsi pesa zinavyojaa (Velocity + circulation) na kupungua.

Labda unisaidie jinsi gani BOT itahakikisha pesa zinajaa mtaani au kupungua mtaani bila kuinvolve Commercial banks hta kidogo?
 
Ni wazi Mama hajui jukumu la serikali kwa BOT vinginevyo asingetoa hiyo kauli.

Ni wazi Mama hajui jukumu la serikali kwa BOT vinginevyo asingetoa hiyo kauli.
mulikuwa munasema vyuma vimekaza wakati wa mwendazake sasa tunatafuta namna ya kupaka angalau kagirisi munasema mama hajui jukumu la serikali., sasa kama mwananchi anakopa milioni 1 analipa milioni moja na nusu hali ya maisha itakuwaje kwa wananchi, mlisema hamna hela mifukoni sasa mwancheni mama afanye namna mambo yaende.

Mamam ana washauri wa uchumi kila upande anajua anachokifanya, tulieni wabongo nchi ipo kwenye mikono salama,
Ni wazi Mama hajui jukumu la serikali kwa BOT vinginevyo asingetoa hiyo kauli.
 
Hiki ulikoshauri kma kikifanywa kwa mkupuo huu, Inflation pamoja na kushuka kwa thamani ya shillingi dhidi ya dollar havikwepeki.

Nadhani BOT waelekezwe tu ila sio kupewa exact figures..ni hatari

Inflation haiwezi kutokea kama interest rate ni ndogo. Pia thamani ya pesa haitashuka. Interest rate ikiwa kubwa, shida ndiyo huanzia hapo.
 
Suala la kushusha riba nchi hii linaonekana kufanyika kutokana na maagizo ya wanasiasa (liko kisiasa) na si Benki Kuu kama wataalamu kushauri au kushusha riba kwa mabenki ili nayo yashushe riba kwa wananchi.

Kwa mfano, leo Mama kaagiza Benki Kuu kuhakikisha mabenki yanashusha riba kufika chini ya asilimia 10 (jambo jema na la kupongeza).

Swali langu ni je, Benki Kuu kama wataalamu, huwa hawaoni umuhimu wa kushusha riba mpaka waagizwe na wanasiasa?

Katika hili, si BOT kama wataalamu ndio wa kushauri wanasiasa waridhie BoT kushusha riba kama BoT hawana mamlaka hayo mpaka wapete idhini ya watawala?

Kama tatizo ni sherai na taratibu, je hatuoni sheria na taratibu hizo zinastahili kufanyiwa marekebisho?

Mambo ya ajabu sana haya!
Tuna mifumo ya hovyo sn, inawezekana wataalam wanashauri vizuri sn lakini wanaoshauriwa wapo tayari kufuata ushauri?
 
BOT tangu aondoke marehemu Beno Ndulu limekuwa litaasisi la hovyo kabisa tangu waweke yule profesa anayejikojolea kwa ulevi haku na alichofanya chochote outstanding kwa ufupi hamna kitu pale walikua wanashiriki kupika matakwimu tuuu lakini sasa wanaumbuka sana pumbaf sana
 
Back
Top Bottom