Nadhani hujui kuwa BOT haipunguzi riba za commercial banks kwa kuwaamrisha, bali wanawashauri tu kupunguza riba kwa kuwapa incentives fulani, fulani. Riba za Commercial banks zinajengewa na vitu vingi kuanzia, riba wanazotozwa kuchukua pesa BOT, risk, n.k.
Sasa utauliza kwanini BOT wasishushe riba wanazotoza Commercial banks ili riba ziwe ndogo?
So far BOT imekuwa ikishusha Centra Bank rate (CBR), ili kuwapunguzia gharama banks ila riba bado zimebaki kuwa juu, hii ina maana kuwa kuna factors nyingine nje ya CBR ambazo zinafanya riba zibaki juu, kwa uelewa wangu mdogo hizo factor nyingine ni pamoja na risk za kumkopesha mtanzania.
Imagine bank wamkopeshe mmachinga ambaye kwanza biashara yake haina permanent address, makazi yake rasmi hayajulikani na vitu vingi vinavyoenda na hivyo, so ili kuhedge against hizi risk lazima wakupenalize riba kubwa incase ukishindwa kulipa wawe wamepata hela yao kidogo.