BOT kushusha riba za mikopo ni mpaka waagizwe ili hali wao ndio wataalam wa kushauri zishuke?

Kaishi Zimbabwe!
 
Ndiyo maana nikakwambia akili zako na za mwendazake hazikuwa na tofauti, yeye alikuwa na utaalamu wa kuiba kura,kupima mapapai corona,kupora watu pesa nk
 
Nashukuru sana mkuu,akishindwa kukuelewa atakuwa na tatizo kubwa somewhere.
 
Is professionalism nowadays in the toilet? Interest rates are market driven instruments as inflation rates. They can only be controlled through "proper" monetary policies. "Hizi siyo issue za majukwaani".
 
Matatizo ya Tanzania ni mengi sana, mpaka ufumbuzi wake unakuwa na matatizo.

Kwa mfano, hili la riba.

1. Riba ziko juu sana. BOT walitakiwa kushusha riba na kuanzisha "domino effect" ya benki nyingine kushusha riba. Kwa hiyo habari nzima ya kushusha riba inaweza kuwa na msingi mzuri.

2. Kiuchumi, rais hatakiwi kuipangia BOT ishushe riba. Hili ni jambo hatari. BOT inatakiwa kujiendesha kwa uhuru bila kuingiliwa na wanasiasa, kwa kuangalia "economic indicators".

Napata shida ku support rais kuipangia BOT ishushe riba, hata pale ninapoona kwamba riba zipo juu sana.

Hizi habari za rais kuagiza BOT ndizo zilifanywa na Idi Amin alipoagiza hela za Uganda zichapishwe nyingi ili watu wawe na hela, matokeo yake Shilingi ya Uganda ikashuka thamani, na haijafanya recovery fully mpaka leo.
 
Benki kama NMB ina ukwasi usio na kifani, lkn wapi haitaki kuwakwamua wateja wake, ilipaswa ipunguze riba mpaka kufikia 5%
Kila benki imepewa rukhusa kupunguza riba kwa jinsi inavyotaka ndani ya theshold iliyowekwa na BOT tatizo mabenki yote hakuna lenye ubunifu kupunguza riba ili kuvutia wateja yote utakuta riba zinalingana. Hoja ya Rais kupunguza riba ni muhimu kiuchumi vinginevyo watu hawatakopa na pia watashindwa kurejesha mikopo. Kipindi hiki cha recession ya korona hii ndiyo mikakati mojawapo ya kukwamua uchumi. Rais ni mchumi anajua vizuri hali hii.Iwapo BOT wanashindwa kuchukua hatua Rais anayo haki ya kuwaagiza wataalam wa Benki kuu kuliangalia hilo vinginevyo haiwezekani warudi kwake na kushauri wakiwa na options na madhara yake huku wakizingatia hali halisi ya sekta ya fedha inavyoathirika kwa sasa.
 
Mimi nataka nikope 800M niingize kwenye biashara zangu. Hizo 800M ni za bure!!??
 
Suala la risk compensation haiwezi kuwa kigezo pekee cha kuongeza riba. Mabenki yenyewe pia yaangalie operational costs zake, weledi katika kutathmini risks na hapo rushwa iondoshwe kwa kuajiri wafanyakazi waaminifu, matumizi ya mifumo ya kisasa kudhibti Non perfomaning Loans na kubadilishana taarifa za wakopaji. Serikali nayo iangalie macro economic policies, monetory and fiscal policies kulegeza riba vinginevyo tusahau kupata wawekezaji
 
Shida uchumi wetu unapaswa ubadilike kwa kuendana na msukumo wa uchumi wa dunia ie paypal etc. Lakini pia milango ya biashara ifunguliwe kati serikali na sekta binafsi tukwepe kabisa kurudi kwenye state monopoly type of economy itatugharimu.
 
Politics are killing this country.Hakuna kinachotekelezeka
 
Huo uchumi muliokalili chuo umelisaidia nini Taifa ......thus why wanasiasa wanaweza adjust mambo na kisiharibike kitu......maana huko chuo vitabu hata vya uchumi si vya Tanzania......kisha mjinga mmoja anaongea eti usiige uchumi wa nchi fulani.
Mkuu mmefikia wapi kwenye hzo adjustment zenu za riba mpaka sasa 🤣 🤣
 
Mkuu mmefikia wapi kwenye hzo adjustment zenu za riba mpaka sasa [emoji1787] [emoji1787]
Monetary policy committee imebariki na ina-expect quarterly hii mambo yataimalika.....ni muda sasa mkuu wa kupitia policies na economic informations za nchi yako...ingia website ya B.O.T....hakuna faida vizazi vyako viwe masikini kwa kupenda ubishi kuliko kujifunza
 
🤣 🤣 🤣 Muda ni ukuta,anyway-Ngoja tusubirie nyama hope hiyo quarter yenu hata iwe ndefu vp haifiki december 🤣 🤣 🤣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…