DOKEZO BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo Kisheria na zinalipa kodi?

DOKEZO BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo Kisheria na zinalipa kodi?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
hizi taasisi nijuavyo Mimi hazipo kisheria na km sikosei BOT walishatolea maelezo kuhusu hizi taasisi kipindi kile cha wale wakenya WA Tala. Kiufupi hazipo kisheria, wao wenyewe wanatumia ujinga wetu kujinufaisha. Zile SMS wanazokutumia na simu wanazopiga, wewe kausha tu usipokee simu zao, pakua app kopa hela wakikupa hela futa app acha kupokea simu hawatakupeleka popote Kwa sababu wanajua hawapo kisheria. Wao ni matapeli, chukueni pesa msirejeshe wataacha wenyewe kukopesha!
 
hawa jamaa ni changamoto kwakweli nilikopa pesa juzi marejesho ilikuw leo asubuh lakin kutokana na hali ya hewa na nilipokuw ni changamoto kidogo!!! lakini wakawapigia ndugu zangu wote simu kuwa wananidai na ikiwa hata siku haijapita na msg zao juu!!! hawa jamaa hawana customer care nzurView attachment 2821916
Uliwapaje namba za ndugu zako!!??
 
hizi taasisi nijuavyo Mimi hazipo kisheria na km sikosei BOT walishatolea maelezo kuhusu hizi taasisi kipindi kile cha wale wakenya WA Tala. Kiufupi hazipo kisheria, wao wenyewe wanatumia ujinga wetu kujinufaisha. Zile SMS wanazokutumia na simu wanazopiga, wewe kausha tu usipokee simu zao, pakua app kopa hela wakikupa hela futa app acha kupokea simu hawatakupeleka popote Kwa sababu wanajua hawapo kisheria. Wao ni matapeli, chukueni pesa msirejeshe wataacha wenyewe kukopesha!

Kwa kweli kabisa
 
YAH: MALALAMIKO JUU YA TAASISI ZA MIKOPO MTANDAONI
Kama mnavyojua changamoto zipo kwa Kila mtu hasa upatikanaji wa fedha pale unapokuwa umepata shida ya ghafla yenye uhitaji wa pesa au changamoto kwenye Biashara, mara nyingi unatafuta sehemu kama kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ya kifedha ili kupata hela na kutatua tatizo lako.

Kuna taasisi zinazo toa MIKOPO kupitia Mtandaoni ambazo unapakua Application kwenye simu yako kutoka kwa Google unaweka taarifa zako na wanakupa mkopo wa haraka. Sasa malalamiko yangu au pengine kwa niamba ya Watanzania wengine ni kama ifuatavyo;

1. Riba wanazotoza ni kubwa sana wakati wa kurejesha tofauti na maelezo ya hawali, yaani unaweza kuambiwa ukichukua 100,000 unarejesha 130,000 ndani ya wiki moja lakini wakati wa kurejesha unaambiwa rejesha 185,000, huu ni wizi wa hali juu.

2. Unaweza kurejesha hiyo hela lakini hawakufuti kwenye mifumo yao wataendelea kukusumbua wakidai haujalipa.

3. Taratibu za kumdai mteja siyo nzuri kwanza hawana customer care wanatunia kauli mbaya za udhalilishaji pamoja na matusi.

OMBI LANGU
1. Naomba nyinyi kama kama nyinyi wa habari tusaidie kwanza kujua kama hizi taasisi zinazotoa MIKOPO MTANDAONI zimesajiliwa na zinatoa MIKOPO kwa kufuata Sheria, kanuni na Taratibu.

2. Tusaidie kupaza sauti ili kama taasisi hizi zipo kihalali basi ziweke riba halisia ambayo mteja anaweza kumudu na isijekuwa kama ile MIKOPO tunayosika KAUSHA DAMU.

3. Waajiri Wafanyakazi wenye weredi na mafunzo ya huduma kwa mteja (Customer care)

Note: kwa ufuatiliaji naomba nizitaje chache;
1. SINGULARITY MICROFINANCE LTD - kwenye Mtandao (play store au app store wakitumia "Mkopo wako"

2. TEMERIA MICROFINANCE LTD - kwenye mtandao (play store au app store wakitumia " Zima Cash"

Hizo ni chache lakini zipo nyingi sana

Tunaomba Beki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi zinazo husika kufuatilia na ikiwezekana kutoa muongozi kama taasisi hizo za kukopesha zinalipa kodi na masharti yao yameridhiwa na mamlaka husika.
Mtanzania aliponzwa na ujinga na upole wake. Kila kitu ni kuomba tu. Akiwekewa dole utasikia naomba mamlaka husika ije ilitoe!
 
Walipe kodi wapi wao wanataka wanaotangaza biashara mtandaoni walipe kodi ila wanaokopesha fedha mtandaoni kwa riba kubwa hawachukui kodi mpaka unaona hao Songesha sijui Mpawa wapo nyuma ya hawa watu...
 
Tunaomba Beki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi zinazo husika kufuatilia na ikiwezekana kutoa muongozi kama taasisi hizo za kukopesha zinalipa kodi na masharti yao yameridhiwa na mamlaka husika.
Kipanya alishasema
"Ili mwanasiasa apate umaarufu lazima atengeneze tatizo kisha aliondoe ili ashangiliwe kuwa ni mbunifu" ukisoma hali ya hewa utagundua kuna mwanasiasa anaandaliwa pongezi shangwe na nderemo
 
Back
Top Bottom