DOKEZO BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo Kisheria na zinalipa kodi?

DOKEZO BoT, TCRA na TRA hivi hizi Taasisi za Mikopo ya Online zipo Kisheria na zinalipa kodi?

  • Thread starter Thread starter Anonymous
  • Start date Start date
Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Serikali kupitia BOT , TCRA wanapaswa kutoa kauli kuhusu Kampuni hizi. Binafsi ninajipanga Kufungua Kesi dhidi ya Kampuni ya BAROMO MICROCREDIT inayoendesha Application ya OnePesa pamoja na Kampuni ya WILKUDOS LIMITED kwa kutumia Lugha za Matusi dhidi yangu tena Mimi nikiwa sio Mkopaji Bali namba yangu imewekwa kama mdhamini bila ridhaa yangu .

Click Screenshots hapo chiniView attachment 2822421View attachment 2822422
Washitaki mkuu hawa kwanza watakuwa na makosa mawili, mosi kutoa lugha chafu pili kujihusisha na biashara haramu lazima wakutafute wakupoze ili yaishe
 
Walinipa 55k baada ya siku 8 wanataka niwalipe 78k....na hapo siku ya sita ndio walianza vurugu za kunipigia simu zao za mikwara mbuzi.

Imagine from 55k to 78k in 8 days.

Nilifuta app yao na kublock namba zao zote.
mkuu nielekeze ulipitia njia gani mpaka ukakopa!
 
Hizi app ziko nyingi sana aisee ukiamua kucheza nao hukosi 1m +
Maana kuna:
  1. PesaX
  2. M-Safi
  3. Zima Cash
  4. Twiga Loan
  5. Cash X
  6. OnePesa
  7. Mkopo haraka kwa dakika mbili
  8. BongoPesa
  9. FiniLoan
  10. SilkLoan
  11. MkopoFasta
  12. Ustawi Loan
  13. MkopoWako
  14. PesaM Loan
  15. Okoa Maisha
  16. Branch
99% hapo ni kampuni moja hiyo ya wachina wapo Makumbusho pale ila wana app zaidi ya 20 kwa majina tofauti
 
Hizi app ziko nyingi sana aisee ukiamua kucheza nao hukosi 1m +
Maana kuna:
  1. PesaX
  2. M-Safi
  3. Zima Cash
  4. Twiga Loan
  5. Cash X
  6. OnePesa
  7. Mkopo haraka kwa dakika mbili
  8. BongoPesa
  9. FiniLoan
  10. SilkLoan
  11. MkopoFasta
  12. Ustawi Loan
  13. MkopoWako
  14. PesaM Loan
  15. Okoa Maisha
  16. Branch
Kweli kuUWA BANK MOJA KAZI... SIJUI MENGI ALIWEZAJE KUUWA NBC

Sehemu Salama KUTAFUTA NA KUPATA wanawake wazuri wa KUOA NA kulea WATOTO NA KUZAA WATOTO KATIKA MIAKA 200 IJAYO NI CHATO.

KABILA ALIKOTOKA JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI – HAKIKA WAMEMALIZA ICE-CREAM YOTE, WANAHAMU YA KUTOA RAIS MWINGINE KWA MIHULA 20 IJAYO.

MAKABILA MENGINE YOTE NDOTO ZA KUTOA URAIS KWENYE MIHULA IJAYO ZIPO KWA ASILIMIA 200- UTAPIGWA JELA LA NJE
 
YAH: MALALAMIKO JUU YA TAASISI ZA MIKOPO MTANDAONI
Kama mnavyojua changamoto zipo kwa Kila mtu hasa upatikanaji wa fedha pale unapokuwa umepata shida ya ghafla yenye uhitaji wa pesa au changamoto kwenye Biashara, mara nyingi unatafuta sehemu kama kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ya kifedha ili kupata hela na kutatua tatizo lako.

Kuna taasisi zinazo toa MIKOPO kupitia Mtandaoni ambazo unapakua Application kwenye simu yako kutoka kwa Google unaweka taarifa zako na wanakupa mkopo wa haraka. Sasa malalamiko yangu au pengine kwa niamba ya Watanzania wengine ni kama ifuatavyo;

1. Riba wanazotoza ni kubwa sana wakati wa kurejesha tofauti na maelezo ya hawali, yaani unaweza kuambiwa ukichukua 100,000 unarejesha 130,000 ndani ya wiki moja lakini wakati wa kurejesha unaambiwa rejesha 185,000, huu ni wizi wa hali juu.

2. Unaweza kurejesha hiyo hela lakini hawakufuti kwenye mifumo yao wataendelea kukusumbua wakidai haujalipa.

3. Taratibu za kumdai mteja siyo nzuri kwanza hawana customer care wanatunia kauli mbaya za udhalilishaji pamoja na matusi.

OMBI LANGU
1. Naomba nyinyi kama kama nyinyi wa habari tusaidie kwanza kujua kama hizi taasisi zinazotoa MIKOPO MTANDAONI zimesajiliwa na zinatoa MIKOPO kwa kufuata Sheria, kanuni na Taratibu.

2. Tusaidie kupaza sauti ili kama taasisi hizi zipo kihalali basi ziweke riba halisia ambayo mteja anaweza kumudu na isijekuwa kama ile MIKOPO tunayosika KAUSHA DAMU.

3. Waajiri Wafanyakazi wenye weredi na mafunzo ya huduma kwa mteja (Customer care)

Note: kwa ufuatiliaji naomba nizitaje chache;
1. SINGULARITY MICROFINANCE LTD - kwenye Mtandao (play store au app store wakitumia "Mkopo wako"

2. TEMERIA MICROFINANCE LTD - kwenye mtandao (play store au app store wakitumia " Zima Cash"

Hizo ni chache lakini zipo nyingi sana

Tunaomba Beki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi zinazo husika kufuatilia na ikiwezekana kutoa muongozi kama taasisi hizo za kukopesha zinalipa kodi na masharti yao yameridhiwa na mamlaka husika.
Niliandika mada ya kuhoji mikopo umiza ya Makampuni ya Simu Hadi Sasa Serikali haijajibu.

Makampuni ya Simu yanatumia Huduma za kifedha kuinyonya Wananchi.Ni wizi mpya.
 
Hahaha mi mwenyewe babu njunju mzee wa kunjunjumila
najaribu kujiunga hapa nione kama nitapata
Screenshot_20231123-151837.jpg
 
Kwa mtu anayeihoji akili yake hawezi kuwadhulumu hawa wababe. Jiulize wanajiamini nini kukukopesha kirahisi hivyo halafu na wewe uwadhulumu kirahisi hivyo?
 
WaTz tuache roho mbaya! Ulipokuwa na shida, ulijipeleka mwenyewe kuomba mkopo, na uelewa wako mdogo wa mambo ya riba au uvivu wa kusoma (janga la taifa), huiusoma na kuelewa unajiinguza kwenye nini. Sasa unadaiwa, mbadala unaouona ni kuwachongea kwa taasisi onevu za serikali.
Kama ungewalipa kama mhemuko wako ulivyokuwa unakusukuma wakati wa shida, ungekuwa hapa na malalamiko haya?

Sent from my moto g 5G (2022) using JamiiForums mobile app
 
Niliandika mada ya kuhoji mikopo umiza ya Makampuni ya Simu Hadi Sasa Serikali haijajibu.

Makampuni ya Simu yanatumia Huduma za kifedha kuinyonya Wananchi.Ni wizi mpya.
Sidhani kama kwa sasa ni rahisi BOT kudhibiti hili bila kuzifuta kabisa hizi taasisi zisiwepo sababu Kukopa online ni gharama.

Gharama ni sababu ya mifumo inayotumika ya software kukuwezesha kukopa.

Mfano ukiwa unarejesha MGODI kuna gharama ambazo wala mnufaika si microfinance wala mtandao wa simu bali wamiliki wa mifumo inayoupdate taarifa zako. Hapo hujaongelea gharama za miamala. Sasa hizi gharama nani atazilipia kukuwezesha kukopa? Shida inaanzia hapo. Unakuta umekopa Tsh 100,000 lakini cost ya per unit ya kuutunza mfumo wa taarifa zako ni gharama hapo ni ukijumuisha mfumo wa wewe kupata taarifa kwa ujumbe wa sms, intergration kati ya mifumo ya fedha na mifumo ya microfinance na mengine mengi.

Pia risk ni kubwa sana sababu wanatoa fedha bila dhamana yoyote rasmi na BOT wanafahamu hilo ndo maana ni kazi kweli kudhibiti hizi taasisi maana hazina mbadala rasmi na anayeenda kukopa huko hakopesheki kwengine ambapo ni rasmi.

Kuepuka huu usumbufu ni kuwa rasmi na kukopa Bank au microfinance ambazo utaweka dhamana na kufanya marejesho kupitia bank.
 
Kuweni makini na permissions mnazoruhusu apps kwenye simu zenu.

App ukiipa permission au access ya contacts ina uwezo wa kusoma namba zote zilizk kwenye simu yako kwa jinsi ulivyosave na kuzibeba kuzipeleka kwenye server zao. Hapo wanaona “baba” “mjomba” “wife” na namba zao
Mie nlitaka kukopa ili nijue tu lakini hichi kipengele nilikuwa naki ignore na ukikikataa haikubali kuendelea nkaamua kuachana nayo sababu nakuwa uchi kila nachofanya wanakiona
 
Mie nlitaka kukopa ili nijue tu lakini hichi kipengele nilikuwa naki ignore na ukikikataa haikubali kuendelea nkaamua kuachana nayo sababu nakuwa uchi kila nachofanya wanakiona
Siyo kazi rahisi kubeba data za kila mtu na kuzitunza. Gharama ni kubwa kumantain hiyo database.

Sijui labda kwa hizo namba za simu ila pia sioni kwanini taasisi ya mikopo iingie gharama kulipia database ya kuhifadhi taarifa za mawasiliano za kila mteja.

Hao wahuni nadhani wana namna nyingine ya kupata taarifa. Sijui lakini ila naona kama ni ujinga kulipia database ili tu usubiri mtu aliyekopa laki yenye riba ya elfu 20 akishindwa kulipa upate namba za simu usumbue ndugu zake.
 
Gharama which? Database ya namba ina ukubwa gani?

Tupige hesabu,
Assuming Kila contact ina jina lenye herufi 20 na namba 3 tofauti kila moja ikiwa na tarakimu 12
Size ya contact moja ni 20+(3x12)
Kila contact ina 56bytes

Assuming kila mteja wao ana contact 1000, database kamili ya contact za mteja ni 56x1000 = 56kB

Assuming wana wateja 100,000
Database kamili ya contact zote za wateja wao wote
56kB x100000 = 5.6GB

Hapo nimeweka namba kubwa kubwa kwenye assumptions lakini unapata picha kwamba si ajabu database yao yote ya kuhifadhi contacts za wateja ni 5GB. Ndogo mno. Negligible.

Tueleze hiyo gharama unayosema kubwa iko wapi?
 
Well sijajua iwapo kama gharama kwenye ofisi au shughuli zako unacharge vipi au uzoefu ulionao ila kwa shughuli ninazofanya kuna gharama naingia kwenye hayo madude ya database na kutunza taarifa za wateja sijui system na ni material .

Hatahivyo Sina hoja zinazojitosheleza za kukukatalia sababu sio mtaalam wa It pengine upo sahihi.
 
Back
Top Bottom