Washitaki mkuu hawa kwanza watakuwa na makosa mawili, mosi kutoa lugha chafu pili kujihusisha na biashara haramu lazima wakutafute wakupoze ili yaisheSerikali kupitia BOT , TCRA wanapaswa kutoa kauli kuhusu Kampuni hizi. Binafsi ninajipanga Kufungua Kesi dhidi ya Kampuni ya BAROMO MICROCREDIT inayoendesha Application ya OnePesa pamoja na Kampuni ya WILKUDOS LIMITED kwa kutumia Lugha za Matusi dhidi yangu tena Mimi nikiwa sio Mkopaji Bali namba yangu imewekwa kama mdhamini bila ridhaa yangu .
Click Screenshots hapo chiniView attachment 2822421View attachment 2822422
mkuu nielekeze ulipitia njia gani mpaka ukakopa!Walinipa 55k baada ya siku 8 wanataka niwalipe 78k....na hapo siku ya sita ndio walianza vurugu za kunipigia simu zao za mikwara mbuzi.
Imagine from 55k to 78k in 8 days.
Nilifuta app yao na kublock namba zao zote.
99% hapo ni kampuni moja hiyo ya wachina wapo Makumbusho pale ila wana app zaidi ya 20 kwa majina tofautiHizi app ziko nyingi sana aisee ukiamua kucheza nao hukosi 1m +
Maana kuna:
- PesaX
- M-Safi
- Zima Cash
- Twiga Loan
- Cash X
- OnePesa
- Mkopo haraka kwa dakika mbili
- BongoPesa
- FiniLoan
- SilkLoan
- MkopoFasta
- Ustawi Loan
- MkopoWako
- PesaM Loan
- Okoa Maisha
- Branch
Kweli kuUWA BANK MOJA KAZI... SIJUI MENGI ALIWEZAJE KUUWA NBCHizi app ziko nyingi sana aisee ukiamua kucheza nao hukosi 1m +
Maana kuna:
- PesaX
- M-Safi
- Zima Cash
- Twiga Loan
- Cash X
- OnePesa
- Mkopo haraka kwa dakika mbili
- BongoPesa
- FiniLoan
- SilkLoan
- MkopoFasta
- Ustawi Loan
- MkopoWako
- PesaM Loan
- Okoa Maisha
- Branch
Nmejiunga wanataka niweke akiba. Nikiweka lak 3 ntapewa sh ngap mkopo?Inigia kwa menu ya Mpesa *150*00#ok,chagua namba 6 mikopo na akiba,halafu namba 3 mgodi.then ufuate maelekezo
akiba? mtego huo...Nmejiunga wanataka niweke akiba. Nikiweka lak 3 ntapewa sh ngap mkopo?
Hahaha mi mwenyewe babu njunju mzee wa kunjunjumilaakiba? mtego huo...
huwezi kupewq mkopo zaidi ya akiba yako.. chemsha bongo kabla hujapagawa
Kupata namba za ndugu ni Rahisi pale anapokuambia Allow Zima Cash to acces your Contacts or phone Log.Namba za ndugu zako wamezitoa wapi?
Niliandika mada ya kuhoji mikopo umiza ya Makampuni ya Simu Hadi Sasa Serikali haijajibu.YAH: MALALAMIKO JUU YA TAASISI ZA MIKOPO MTANDAONIKama mnavyojua changamoto zipo kwa Kila mtu hasa upatikanaji wa fedha pale unapokuwa umepata shida ya ghafla yenye uhitaji wa pesa au changamoto kwenye Biashara, mara nyingi unatafuta sehemu kama kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ya kifedha ili kupata hela na kutatua tatizo lako.
Kuna taasisi zinazo toa MIKOPO kupitia Mtandaoni ambazo unapakua Application kwenye simu yako kutoka kwa Google unaweka taarifa zako na wanakupa mkopo wa haraka. Sasa malalamiko yangu au pengine kwa niamba ya Watanzania wengine ni kama ifuatavyo;
1. Riba wanazotoza ni kubwa sana wakati wa kurejesha tofauti na maelezo ya hawali, yaani unaweza kuambiwa ukichukua 100,000 unarejesha 130,000 ndani ya wiki moja lakini wakati wa kurejesha unaambiwa rejesha 185,000, huu ni wizi wa hali juu.
2. Unaweza kurejesha hiyo hela lakini hawakufuti kwenye mifumo yao wataendelea kukusumbua wakidai haujalipa.
3. Taratibu za kumdai mteja siyo nzuri kwanza hawana customer care wanatunia kauli mbaya za udhalilishaji pamoja na matusi.
OMBI LANGU
1. Naomba nyinyi kama kama nyinyi wa habari tusaidie kwanza kujua kama hizi taasisi zinazotoa MIKOPO MTANDAONI zimesajiliwa na zinatoa MIKOPO kwa kufuata Sheria, kanuni na Taratibu.
2. Tusaidie kupaza sauti ili kama taasisi hizi zipo kihalali basi ziweke riba halisia ambayo mteja anaweza kumudu na isijekuwa kama ile MIKOPO tunayosika KAUSHA DAMU.
3. Waajiri Wafanyakazi wenye weredi na mafunzo ya huduma kwa mteja (Customer care)
Note: kwa ufuatiliaji naomba nizitaje chache;
1. SINGULARITY MICROFINANCE LTD - kwenye Mtandao (play store au app store wakitumia "Mkopo wako"
2. TEMERIA MICROFINANCE LTD - kwenye mtandao (play store au app store wakitumia " Zima Cash"
Hizo ni chache lakini zipo nyingi sana
Tunaomba Beki Kuu ya Tanzania (BOT), Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na taasisi zinazo husika kufuatilia na ikiwezekana kutoa muongozi kama taasisi hizo za kukopesha zinalipa kodi na masharti yao yameridhiwa na mamlaka husika.
najaribu kujiunga hapa nione kama nitapataHahaha mi mwenyewe babu njunju mzee wa kunjunjumila
haina haja ya kuscreenshot ww nenda play store andk mikopo mtandaoni zpo kibao zaid ya hzo hapoAsante sana mkuu. Achana niiscreenshot hii comment nitaifanyia kazi kesho.
Watu wakiwa na shida hawajui ni nini wanayofanya na madhara yake, wanakuja kuzinduka baada ya matokeo ya matendo yao!Namba za ndugu zako wamezitoa wapi?
Sidhani kama kwa sasa ni rahisi BOT kudhibiti hili bila kuzifuta kabisa hizi taasisi zisiwepo sababu Kukopa online ni gharama.Niliandika mada ya kuhoji mikopo umiza ya Makampuni ya Simu Hadi Sasa Serikali haijajibu.
Makampuni ya Simu yanatumia Huduma za kifedha kuinyonya Wananchi.Ni wizi mpya.
Makampuni ya mawsiliano kuachwa yaendelee kutoa mikopo ya kausha damu Serikali imebariki wananchi kufilisiwa kwa maslahi ya kikodi?
Kukua kwa teknolojia kumeyavuta makampuni ya Simu kuanza kufanya biashara ya huduma za kifedha ambazo hapo awami zilikuwa zinafanya na taasisi za fedha tuu kama benki. Katika kufanya biashara hiyo makampuni ya simu yameanzisha huduma mbalimbali ya muda mfupi za kifedha ikiwemo kuwezesha...www.jamiiforums.com
Mie nlitaka kukopa ili nijue tu lakini hichi kipengele nilikuwa naki ignore na ukikikataa haikubali kuendelea nkaamua kuachana nayo sababu nakuwa uchi kila nachofanya wanakionaKuweni makini na permissions mnazoruhusu apps kwenye simu zenu.
App ukiipa permission au access ya contacts ina uwezo wa kusoma namba zote zilizk kwenye simu yako kwa jinsi ulivyosave na kuzibeba kuzipeleka kwenye server zao. Hapo wanaona “baba” “mjomba” “wife” na namba zao
Siyo kazi rahisi kubeba data za kila mtu na kuzitunza. Gharama ni kubwa kumantain hiyo database.Mie nlitaka kukopa ili nijue tu lakini hichi kipengele nilikuwa naki ignore na ukikikataa haikubali kuendelea nkaamua kuachana nayo sababu nakuwa uchi kila nachofanya wanakiona
Gharama which? Database ya namba ina ukubwa gani?Siyo kazi rahisi kubeba data za kila mtu na kuzitunza. Gharama ni kubwa kumantain hiyo database.
Sijui labda kwa hizo namba za simu ila pia sioni kwanini taasisi ya mikopo iingie gharama kulipia database ya kuhifadhi taarifa za mawasiliano za kila mteja.
Hao wahuni nadhani wana namna nyingine ya kupata taarifa. Sijui lakini ila naona kama ni ujinga kulipia database ili tu usubiri mtu aliyekopa laki yenye riba ya elfu 20 akishindwa kulipa upate namba za simu usumbue ndugu zake.
Well sijajua iwapo kama gharama kwenye ofisi au shughuli zako unacharge vipi au uzoefu ulionao ila kwa shughuli ninazofanya kuna gharama naingia kwenye hayo madude ya database na kutunza taarifa za wateja sijui system na ni material .Gharama which? Database ya namba ina ukubwa gani?
Tupige hesabu,
Assuming Kila contact ina jina lenye herufi 20 na namba 3 tofauti kila moja ikiwa na tarakimu 12
Size ya contact moja ni 20+(3x12)
Kila contact ina 56bytes
Assuming kila mteja wao ana contact 1000, database kamili ya contact za mteja ni 56x1000 = 56kB
Assuming wana wateja 100,000
Database kamili ya contact zote za wateja wao wote
56kB x100000 = 5.6GB
Hapo nimeweka namba kubwa kubwa kwenye assumptions lakini unapata picha kwamba si ajabu database yao yote ya kuhifadhi contacts za wateja ni 5GB. Ndogo mno. Negligible.
Tueleze hiyo gharama unayosema kubwa iko wapi?