BOT: Tunageukia kutoa elimu fedha kwa kilimo cha mbogamboga na nafaka

BOT: Tunageukia kutoa elimu fedha kwa kilimo cha mbogamboga na nafaka

Bagamoyo

Platinum Member
Joined
Jan 14, 2010
Posts
32,522
Reaction score
37,398
01 August 2025
BOT ACADEMY, WFP KUSHIRIKIANA KUTOA ELIMU YA FEDHA KWA VIJANA

View: https://m.youtube.com/watch?v=WugyiK5DhAY
A big step for Tanzanian youths in agri-finance

Hon. Gov. Emmanuel Tutuba and WFP’s Christine Mendes launch the Certified Financial Educators Initiative — empowering 150 youth and partners to drive financial inclusion in agriculture in this great nation of East Africa which is a bread basket in the entire region.
Chuo cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT Academy) kimesaini Hati ya Makubaliano (MoU) na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) kwa lengo la kuwapatia elimu ya fedha vijana kupitia Mradi wa Vijana Kilimo Biashara (VKB).

Hafla hii ya utiaji saini imefanyika leo, Julai 31, 2025, katika ofisi za BoT jijini Dar es Salaam ambapo mgeni rasmi alikuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Bw. Emmanuel Tutuba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Gavana Tutuba ameishukuru na kuipongeza WFP kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuwawezesha vijana wanufaika wa mradi huo kupata maarifa ya kifedha yanayowawezesha kuboresha maisha yao kupitia kilimo biashara.

“Leo tumesaini rasmi ushirikiano wa Mradi wa Vijana Kilimo Biashara, ambao unatekelezwa kwa pamoja na BoT Academy Mwanza na WFP. Wenzetu wa WFP wamekubali kufadhili masuala ya elimu ya fedha kwa vijana katika mikoa saba hapa nchini. Mikoa hiyo ni Dodoma, Arusha, Tabora, Singida, Manyara, Simiyu na Shinyanga.” amesema Gavana Tutuba.

Ameeleza kuwa Chuo cha Benki Kuu kitatoa elimu ya fedha kwa vijana ambao watawezeshwa na WFP kupitia mradi wa VKB ili waweze kusimamia fedha zao kwa ueledi pamoja na kutumia mifumo rasmi ya fedha.

Aidha, Gavana Tutuba amebainisha kuwa Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha elimu ya fedha inawafikia makundi yote ya jamii, wakiwemo wanawake, watu wenye ulemavu, wavuvi, na wajasiriamali wadogo ambao utafiti unaonesha makundi hayo hayajafikiwa na elimu ya fedha ya kutosha.

Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mkazi wa WFP nchini, Bi. Christine Mendes amesema Mradi wa VKB, unaofadhiliwa na Mastercard Foundation, unalenga kuwapatia vijana wakulima ujuzi na rasilimali muhimu ili kuboresha uzalishaji na kukuza uchumi endelevu.

Bi. Mendes amesema tangu kuanza kwa mradi huo mwaka 2022, zaidi ya vijana 83,000 wameshanufaika – asilimia 70 kati yao wakiwa wanawake.

Ameongeza kuwa lengo ni kuwafikia jumla ya vijana 115,000 ifikapo mwaka 2027, huku kupitia ushirikiano huo, WFP ikitoa ufadhili wa dola za Marekani 100,000 (sawa na zaidi ya shilingi milioni 250).
 
01 August 2025

Uzinduzi wa Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS)

View: https://m.youtube.com/watch?v=N_SW7UtG-E4
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Isdori Nzabhayanga Mpango, alizindua rasmi Mfumo Mkuu Jumuishi wa Kibenki (iCBS) tarehe 30 Julai 2025, katika ofisi za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) jijini Dar es Salaam.

Mfumo huo umebuniwa na kutengenezwa na wataalamu wa BoT, ikiwa ni hatua muhimu ya kuimarisha mifumo ya ndani na kuongeza ufanisi wa kiutendaji wa Benki Kuu.
 
Back
Top Bottom