Tatizo letu wengi bado tuna hangover ya siasa za ujamaa na kujitegemea. Eti binadamu wote ni sawa! Kivipi?
Jamani, ingawa ukweli ni kwamba inauma..kwamba Tanzania umaskini umekithiri lakini hebu tuangalie upande mwingine wa shillingi. Hawa jamaa hawapewi hizo hela bure. Wanakopeshwa. Na watarudisha. Hivi inatofauti gani na mtu anayenunua nyumba kwa mortgage huko ulaya au kwingineko na akatakiwa kulipa kwa kipindi cha miaka 30?
People, lets face it. Umasikini TANZANIA hautaisha kwa Gavana Ndullu kuwanyima mikopo wafanyakazi wake. Rather umasikini utaisha kwa wale wanaokabidhiwa dhamana ya kuongoza haya mashirika kwa kuchapa kazi kwa ufanisi kusudi waweze kutoa incentive kwa wafanyakazi wao. Alichokifanya Ndullu ni halali kabisa. Sema tunaona ni abnormal kwa sababu ya umasikini wetu..... wote macho yetu yako BOT. Infact kama mashirika yote yangekuwa yanaendeshwa kwa ufanisi...hii ingekuwa ni namna ya kumotivate watu wachape kazi...
Msisahau kwamba jamani..human being is inherently selfish. Mtu huwezi kumwambia amalize PhD yake Harvard au kwingineko..then aje umpe mshahara wa nyanya! Na mikopo ya namna hii ni mojawapo ya kutoa incetives za kuwa attract wataalamu makini. Hivi Ndullu na PhD yake ya Northwestern..mnadhani angekosa kazi makini huko World Bank au kwingineko? Lets face it. Ndo ukweli unaouma huo.
I may be wrong, lakini nadhani this is a good strategy, as long as watu wanafanya kazi. Harafu tusitake kumsingizia Ndullu..anayeharibu ni JK na serikali yake kwa kushindwa kupambana na ufisadi..there enough for all of us..but when you allow the few to rip off the whole country..even hard working men and women...wanakuwa victims.... Let every hard working man and woman be rewarded. Huwezi sema kwamba kwa vile we are the poorest nation on earth basi mimi Masanja na PhD yangu (mfano) nisipate kitu kusudi tulingane. Hizo ni zama za ujima!
Kama alivyosema Waberoya, its only hard work which can liberate a person from the equation of poverty. Hata hawa wananchi lazima wafike kipindi..wajue kwamba na wao wana obligation kama raia..siyo kutetewa tuu. Mfano wanapohitajika kupiga kura..let them elect serious and responsible leaders. Leo unapewa tshirt unampigia kura fulani..kesho jamaa akijineemesha na wewe unakufa kwa njaa..utamlaumu nani? Otherwise..poverty is here to stay..whether Ndullu gives out Largesse za BoT kwa wafanyakazi wake or not.
Tuache kusingizia ufisadi kila kitu..I say Ndullu amefanya jambo jema. Cha muhimu kuwe na transprency na accountability.
Masanja,
Hakuna mtu anaye pinga kiongozi wa sehemu ya kazi kuwapa motisha au maslahi bora wafanya kazi wake.
Tunachopinga ni kuwa Bank kuu ni taasisi ya serikali ambayo mimi na wewe tunahisa pale.
Pili ndio chombo chenye kuratibu vyombo vya fedha ikiwemo mikopo iwe ya biashara au ya kujenga nyumba.
Tatu kuna upungufu/mapungufu kwenye eneo hilo la mikopo hasa hasa ya kujenga nyumba, kwa wafanyakazi na wakulima na wafanya biashara kwa asilimia kubwa.
Sasa ikiwa BOT ndio msimamizi wa hayo mabenki na kuna tatizo hilo katika nchi hii, basi wao wangekuwa wa kwanza kutengeneza sera ambayo itafanikisha jambo hili kwa watanzania walio wengi.
na kama tunasema kuhusu kustimulate the economy na mambo mengine, suala la mikopo ya nyumba ni la muhimu, maaa kutokana na nyumba bora, afya za watu zitakuwa bora, utendaji mzuri wa kazi utakuwepo, wizi utapungua, shinikizo za damu nk zitapungua, watoto wetu watapata nafasi nzuri zaidi ya kujisomea jioni, wateja na waumeme wataongezeka, maana kwenye nyumba ya matope au nyasi ningumu /haiwezekani kuweka umeme hivyo kurahisha utumiaji wa majiko ya gesi na umeme kutapunguza ukataji wa miti nk nk.
nne kwa sababu hiyo sio biashara ya Bank kuu kutoa mikopo, kwa staff basi utaona watakuwa na limitation ya mtaji wa fungu la mikopo/au ukasababisha washindwe kutimiza majukumu ya kuanzishwa kwa BOT
Tano kuna kiongozi moja aliwahi kupoteza kazi BIMA kwa kutoa mikopo kwa Staff ambao baadae walitumia kinyume cha walivyo tarajiwa kwa sababu shirika hilo au mkurugenzi huyo alishindwa kufuatilia matumizi yake, maana anamajukumu ya uongozi na kuendesha biashara ya bima.
Lakini leo hii kama ukienda Azania Bank kwa sababu wao ndio oja ya biashara zao wana njia za kukufuatilia na ku-minimise risk.
Sasa sijui Human resource/Finance Dept ya BOT baadae wanafualia na kuhifadhi hizo hati za viwanja za wakopaji? na ku-kokorotoa interest rate kila mwenzi kama sio free.