- Thread starter
- #41
Tatizo letu wengi bado tuna hangover ya siasa za ujamaa na kujitegemea. Eti binadamu wote ni sawa! Kivipi?
Jamani, ingawa ukweli ni kwamba inauma..kwamba Tanzania umaskini umekithiri lakini hebu tuangalie upande mwingine wa shillingi. Hawa jamaa hawapewi hizo hela bure. Wanakopeshwa. Na watarudisha. Hivi inatofauti gani na mtu anayenunua nyumba kwa mortgage huko ulaya au kwingineko na akatakiwa kulipa kwa kipindi cha miaka 30?
People, lets face it. Umasikini TANZANIA hautaisha kwa Gavana Ndullu kuwanyima mikopo wafanyakazi wake. Rather umasikini utaisha kwa wale wanaokabidhiwa dhamana ya kuongoza haya mashirika kwa kuchapa kazi kwa ufanisi kusudi waweze kutoa incentive kwa wafanyakazi wao. Alichokifanya Ndullu ni halali kabisa. Sema tunaona ni abnormal kwa sababu ya umasikini wetu..... wote macho yetu yako BOT. Infact kama mashirika yote yangekuwa yanaendeshwa kwa ufanisi...hii ingekuwa ni namna ya kumotivate watu wachape kazi...
Msisahau kwamba jamani..human being is inherently selfish. Mtu huwezi kumwambia amalize PhD yake Harvard au kwingineko..then aje umpe mshahara wa nyanya! Na mikopo ya namna hii ni mojawapo ya kutoa incetives za kuwa attract wataalamu makini. Hivi Ndullu na PhD yake ya Northwestern..mnadhani angekosa kazi makini huko World Bank au kwingineko? Lets face it. Ndo ukweli unaouma huo.
I may be wrong, lakini nadhani this is a good strategy, as long as watu wanafanya kazi. Harafu tusitake kumsingizia Ndullu..anayeharibu ni JK na serikali yake kwa kushindwa kupambana na ufisadi..there enough for all of us..but when you allow the few to rip off the whole country..even hard working men and women...wanakuwa victims.... Let every hard working man and woman be rewarded. Huwezi sema kwamba kwa vile we are the poorest nation on earth basi mimi Masanja na PhD yangu (mfano) nisipate kitu kusudi tulingane. Hizo ni zama za ujima!
Kama alivyosema Waberoya, its only hard work which can liberate a person from the equation of poverty. Hata hawa wananchi lazima wafike kipindi..wajue kwamba na wao wana obligation kama raia..siyo kutetewa tuu. Mfano wanapohitajika kupiga kura..let them elect serious and responsible leaders. Leo unapewa tshirt unampigia kura fulani..kesho jamaa akijineemesha na wewe unakufa kwa njaa..utamlaumu nani? Otherwise..poverty is here to stay..whether Ndullu gives out Largesse za BoT kwa wafanyakazi wake or not.
Tuache kusingizia ufisadi kila kitu..I say Ndullu amefanya jambo jema. Cha muhimu kuwe na transprency na accountability.
Masanja,
Ni vizuri na ni maneno ya busara uliyoyaeleza but ukae ukijua haya maneno yako yanaapply katika mazingira tofauti na unavyofikiria wewe. Kwanza ukae ukijua mtazamo wa kila mtu alipwe kwa mafanikio au efforts alizozifanya (i.e. pay to performance) ni mtindo unaufanyika katika organisation ambazo mtazamo wake ni profit maximization sasa BOT lengo ni kusimamia pesa za serikali au kumaximize profits!!!!
Perhaps labda tukufafanulie kazi ya BOT imegawanyika katika makundi makuu tano.
Moja Bankers to Bank au msimamizi wa mabenki mengine
Pili Government Banks ambapo inasimamia accounts za serikali.
Tatu Policy making ambapo BOT inasimamia Monetary Policy, vile vile ikishirikiana na Ministry of Finance Kuset up fiscal policy.
Nne Lender of Last Resort kama banks zikiwa na matatizo zinaweza kuenda kuomba rescue BOT.
Tano Clearing house to facilitate payment systems ndani ya nchi.
Sasa kamanda hebu niambie Profit maximization ipo wapi??? Na hoja ya kwamba mtu na PhD ya Harvard kwenda kufanya kazi BOT nataka nikuulize alienda kufanyia kazi nini BOT kama anajua ni civil job. It is a free world akijijua kama yeye ni competitive kwanini asiende HSBC au Barclays ambapo watu wanakula bonus ya $1 Million anang'ang'ana na BOT . BOT mhimimiliki wake mkuu ni mimi na wewe tunaolipa kodi tofautisha bonus na incentives za Barclays na BOT ni vitu viwili tofauti mzee BOT ni kazi ya serikali kama ungelikuwa unataka pesa angelienda private sector.