Greenspan watanzania badala ya kufikiria ni jinsi gani atawawezesha watanzania milioni 40 pamoja na wawekezaji sera zake ni za kuwafikiria wafanyakazi 600 wa Bot
Hivi kweli tutafika? hivi toka Greenspan wetu ameingia BOT ametoa sera gani ya kuweza kusaidia kufufua Uchumi wa Tanzania? au kuzui EPa ndio achievement yake na kufanya audit ya ajira ya watoto wa Vigogo?
Au tuseme sera za kuendeleza nchi ni Siri?
Hivi Kishoka unaelewa Role mojawapo ya BOT ni kuzuia muzunguko mbovu wa Peesa, kama Capital Flight inayofanywa na RITES? je Greenspan wetu amelishughulikia vipi suala kama Hilo?
Hivi unajua Role nyingine ni kuishauri serikali na kutoa sera ambazo zitawezesha Commercial Bank kuongeza fungu la mikopo ya Nyumba ikiwa ni pamoja kuwa na specific Deparment iwe ni NSSF, PPF, CRDB nk nk ambazo zipo wazi kwa watu wote kwa ajili ya mikopo ya Nyumba, badala ya sasa hivi kila shirika/kampuni nk wamekuwa ma-expert wa kutoa mikopo.
Je waelewa miongozo hiyo unayo sema ya Soft loan ina limitation, inatolewa in terms ya Salary advance, ambayo to the maximum ni 3 years salary.
sasa ukija mkopo unaozidi hapo inabidi ujiulize una resource za kuhifadhi hati za nyumba za wakopaji, wafanyakazi wa ku-manage hiyo mikopo, na siku hizi mambo ya Software, hivyo una progaramme ya kumanage hiyo mikopo?
Ni consequencies za capital outlay ya kutoa hiyo mikopo kwenye core activities zako ipoje?
Halafu hiyo context ya kusema BOT inafanya Biashara ? biashara gani binadamu anayofanya isiyo na Competition? maana Commercial Bank zote lazima wapitishie mambo ya huko, na kwa serikali lazima wapitishie transaction zao huko, na Treasury Bills lazima zipitie huko.mimi ninachona wanatoa huduma kama ilivyo Muhimbili, na angalau Muhimbili Hospital wana Competition ya Agakhan Hospital, Lugalo, Regency Mikocheni, na waganga wa Kienyeji.
Labda tunaweza walinganisha na JWTZ.
Gavana aikingia kifua mikopo ya watumishi BoT
Na Ramadhan Semtawa
UONGOZI wa Benki Kuu (BoT), umetetea mikopo ya mamilioni ya watumishi wake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, ukisema mpango huo, unalenga kuwajengea maisha bora watumishi hao.
Kauli hiyo, inakuja kufuatia kuwepo kwa waraka wa baraza la mikopo la nyumba, ambalo limetaja viwango vya mikopo kwa madaraja tofauti katika matawi yake yote ya Mwanza, Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na Mbeya.
Waraka huo, unaonyesha kila mfanyakazi ataweza kukopa kati ya Sh 100milioni ikiwa ni kiwango cha juu na Sh 30 milioni kiwango cha chini kulingana na wadhifa wa mtumishi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
Akizungumzia waraka huo, Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu, alisema ni utaratibu ambao benki imejiwekea ili kuwawezesha wafanyakazi wake kimaisha.
Profesa Ndulu, alisema BoT, ilijiwekea utaratibu huo baada ya kuangalia mahitaji ya msingi ya makazi kwa watumishi wake.
"Ni utaratibu ambao upo kwa karibu miaka 20 sasa, lakini sasa tumeuboresha kwa kuangalia mahitaji ya mikopo kwa umakini," alifafanua Gavana Ndulu.
Profesa Ndulu ambaye amekuwa katika mchakato wa kuisafisha taasisi hiyo ya fedha, aliweka bayana kwamba mikopo hiyo, imekuwa ikitolewa kwa umakini ili kuhakikisha inarejeshwa.
Alisisitiza kabla benki hiyo, haijatoa mikopo, inatafuta taarifa za wahusika ili kubaini kama wana madeni ndani na nje ya benki hiyo.
"Hatukopeshi tu bila kufuata utaratibu, vipo vigezo vya mtu kukopa mbali ya madaraja, tunaangalia madeni ya mtu ili tujue uwezo wake wa kurejesha," alisisitiza Ndulu.
Alisema kiutaratibu benki hiyo, inaangalia madeni ili kila mfanyakazi abaki angalau na theluthi moja ya mshahara baada ya kukatwa madeni anayodaiwa.
"Na wao ni binadamu kwa hiyo lazima tuhakikishe angalau, wanabakiwa japo na theluthi moja ya mshahara, baada ya makato," aliongeza gavana huyo.
Facebook