Kaka watu hawana wivu na hakuna mtu anafaidika lolote ila la msingi ni je hii mikopo inayotoka karibu na uchaguzi ina faida yeyote kwa uchumi wa Tanzania!!!!
Hatukatai kila Idara na Benki Kuu zina budget zake husika but kinacholalamikiwa hapa ni kitendo cha BOT kuingilia kazi za investment banks na commercial banks na building society.
Umeshawahi kusikia wapi Bank of England ikatoa mortgage financing, Federal Reserve ya US imetoa mortagage. These are toxic assets cause kwanza ni long-term commitment and probability of default ni kubwa na ndio maana banks zinacharge interest kubwa kufidia loss zitakazotokea.
Gavana anasema wanafanya uchunguzi yakinifu kabla ya kutoa mikopo but come on hakuna ambaye anayeweza kutabiri kesho mimi na wewe tutaamkaje. Prof Merton mwenyewe anakwambia probability of default na metrics za kumeausure distance to default cannot full explain default risk exposure. The future is unexplainable sasa BOT inakopesha watu Billion 3 bila ya interest chukulia watu watano kati yao wamefariki baada ya miezi 6 tumepoteza milioni 500 ambazo hizo milioni 500 hata kama tutarecove tunabahati sana kupata 75%. Msitudanganye wazee hatujawa wajinga kiasi hicho.
Ni mawazo mgando vile vile kufikiria kuwa uchumi wa kibepari unaendeshwa kiholela kama baadhi ya watu wanavyotaka kutuaminisha si kweli. Mikopo ya hovyo kama hii kwa wafanya kazi wa BoT ndiyo inayo distort circulation ya pesa na kusababisha spiralling ya inflation.
Mashirika yote zamani yalikuwepo kwenye hii bonanza ya kuwagawia wafanyakazi wake fedha kwa mfumo wa kutoa mikopo isiyokuwa na riba. Matokeo yake mambo haya yalisababisha mashirika mengi kufa. Benki kuu inaweza kufa ikifanya ujinga huo? Haiwezi benki kuu itachota moja kwa moja kutoka hazina.
Kulinda soko ni lazima kuwa na Busara katika ufanyaji wa maamuzi. Haya nayaita ni maamuzi ya kijinga wakati huu ambao tuna sera ya serikali kutojihusisha na Biashara. Taasisi nyingine zote wanachofanya ni kujadiliana na Mabenki ili wafanyakazi wao wapate interrest naffuu. Hata Benki kuu hizi fedha wangezikopesha kwa mabenki kwa masharti nafuu zaidi halafu mabenki ya Biashara ndo yakatoa mikopo hiyo kwa wafanyakazi wa benki kuu, hata kama ni kwa interrest kidogo zaidi kuliko wengine fedha hii ingekuwa na maana zaidi. Fedha ingeingia kwenye circulation kwa kufuata sheria zote za mfumo wa kibepari na hao wafanyakazi wangekuwa makini wakati wa manunuzi ya vifaa vyao. Lakini kitakacho tokea ni mtu kwenda kununua kiwanja akiambiwa ni milioni tano anatoa tu bila hata negotiation kwa sababu fedha yake amechotewa tu!! Hii ndo inflation wajomba!
Tatizo wengi hapa tunajiita mabepari wakati bado hangover ya ujamaa ni kubwa. Hii kutoa fedha kwa mtindo kama huo ni hangover ya ujamaa. Tunaamini kuwa tunafanya ubepari, lakini ni uongo. Ubepari unahakikisha kuwa watu hawagawiwi hovyo hovyo bila kufanyia kazi. Ubepari haugawi vitu bure. Hii si mikopo. Ni kama watu kupewa bure, ni mikopo gani isiyo na riba? Ni kutoa bure. Hata kama ina riba, ni sheria gani inayowaruhusu benki kuu kutoa mikopo kwa individuals? LAZIMA TUUNGALIE UBEPARI KWA KILE AMBACHO NI UBEPARI. Tusiwe tunafanya mambo ya kijamaa halafu tunadai eti tunatekeleza ubepari, ubepari wa wapi wa kugawiana bure? Hapa ni rahisi. Benki kuuu wanachota fedha kwa kucharge interrest kwenye kodi za Wabongo halafu wanajidai eti wanafanya biashara, wanashindana na nani?
Kwa mtindo huo Benki kuu inashindana na Mabenki ya Biashara kutoa mikopo ambalo si jambo la haki kabisa. Inabidi Sheria zetu ziwe makini. Hapa ni watu kujigawia chao mapema halafu tunajificha kwenye kichaka cha eti tunatekeleza Ubepari, huo ni uongo, tena ni uzandiki. Hii inasababisha Mabenki ya Biashara kuendelea kucharge riba kubwa kwa wateja wachache wanaowapata. Cream ya watu ambao wanakopesheka na Mabenki mengine ndo hawa hawa ambao Benki kuu inawapa fedha bila riba. Sasa akienda kukopa Benki Mwalimu ni lazima Benki wamcharge interrest kubwa tu.
Hii ni mbovu na inavuruga uchumi, na huu si ubepari. Ni hangover ya ujamaa hii. Mabepari hawagawi bure hata siku moja. Lazima warudishe hata gharama. Mikopo kama hii bila riba hairudishi hata gharama. Ni kuwagawia bure! Kuhakikisha kuwa gharama inarudi lazima fedha hii ingepitishwa kwenye Mabenki ya biashara kwani ndo yanajua na yana utaalamu wa kukokotoa gharama halisi. Hapa Benki kuu hakuna cha ndullu wala nini, wamezama kwenye hangover ya ujamaa tu, full stop.
Huu mfano sio sahihi kabisa TBL na TCC ni kampuni binafsi hauwezi kufananisha na BOT chombo cha serikali.Hivi leo TBL na TCC wakitoa motisha wa namna hii tutalalakmika kwa ni na wa Chibuku au Mataputapu wasipewe?
Hapo Kishiko umeniacha hoi! nafikiri ndio maana unatetea BOT kutoa Mikopo kwa staff bila kuelewa Role ya BOT na Majukumu ya GOvernor katika ku-shape uchumi wa nchi na nguvu za Governor katika ku-control Uchumi.Kwani wamesema hii ni mortgage? Kwani ni lazima tufanane na Bank of England au FRB?
Mbona kama tunafananisha na FRB au Bank of England kuhusiana na mikopo, hatufananishi na mambo mengine?
Discetion ya wao kutoa soft loan kwa wafanyakazi ipo, inafuata kanuni zao na miongozo. Kama wangefanya kinyemela, hapo linaeleweka, lakini limefanyika kihalali na nina uhakika wa masharti yaliyowekwa ili kuhakikisha kuwa fedha zinarudi.
Labda niwakumbushe kitu kimoja, fedha yote iliyoliwa Tanzania na hasa BOT haikuwa mtajiwa BOT au fedha za Serikali, bali ni fedha zilizokaa benki bila kuwa na mtu au specifics.
Pesa zote zilizohujumiwa si mali ya BOT au URT, bali ni mali ya watu ambao hawajulikani walipo au wamesahau kuwa wanafedha zao na badala ya kuwekewa muda wa kuhakikiwa ili zitumike kwa Serikali kama Unclaimed Property, wajanja wakatafuta mbinu kuzichukua na kujisaidia!
May be mkilielewa hilo mtapata majibu kwa maswali yenu.
Greenspan watanzania badala ya kufikiria ni jinsi gani atawawezesha watanzania milioni 40 pamoja na wawekezaji sera zake ni za kuwafikiria wafanyakazi 600 wa Bot
Hivi kweli tutafika? hivi toka Greenspan wetu ameingia BOT ametoa sera gani ya kuweza kusaidia kufufua Uchumi wa Tanzania? au kuzui EPa ndio achievement yake na kufanya audit ya ajira ya watoto wa Vigogo?
Au tuseme sera za kuendeleza nchi ni Siri?
Hivi Kishoka unaelewa Role mojawapo ya BOT ni kuzuia muzunguko mbovu wa Peesa, kama Capital Flight inayofanywa na RITES? je Greenspan wetu amelishughulikia vipi suala kama Hilo?
Hivi unajua Role nyingine ni kuishauri serikali na kutoa sera ambazo zitawezesha Commercial Bank kuongeza fungu la mikopo ya Nyumba ikiwa ni pamoja kuwa na specific Deparment iwe ni NSSF, PPF, CRDB nk nk ambazo zipo wazi kwa watu wote kwa ajili ya mikopo ya Nyumba, badala ya sasa hivi kila shirika/kampuni nk wamekuwa ma-expert wa kutoa mikopo.
Je waelewa miongozo hiyo unayo sema ya Soft loan ina limitation, inatolewa in terms ya Salary advance, ambayo to the maximum ni 3 years salary.
sasa ukija mkopo unaozidi hapo inabidi ujiulize una resource za kuhifadhi hati za nyumba za wakopaji, wafanyakazi wa ku-manage hiyo mikopo, na siku hizi mambo ya Software, hivyo una progaramme ya kumanage hiyo mikopo?
Ni consequencies za capital outlay ya kutoa hiyo mikopo kwenye core activities zako ipoje?
Halafu hiyo context ya kusema BOT inafanya Biashara ? biashara gani binadamu anayofanya isiyo na Competition? maana Commercial Bank zote lazima wapitishie mambo ya huko, na kwa serikali lazima wapitishie transaction zao huko, na Treasury Bills lazima zipitie huko.mimi ninachona wanatoa huduma kama ilivyo Muhimbili, na angalau Muhimbili Hospital wana Competition ya Agakhan Hospital, Lugalo, Regency Mikocheni, na waganga wa Kienyeji.
Labda tunaweza walinganisha na JWTZ.
Gavana aikingia kifua mikopo ya watumishi BoTNa Ramadhan Semtawa
UONGOZI wa Benki Kuu (BoT), umetetea mikopo ya mamilioni ya watumishi wake kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, ukisema mpango huo, unalenga kuwajengea maisha bora watumishi hao.
Kauli hiyo, inakuja kufuatia kuwepo kwa waraka wa baraza la mikopo la nyumba, ambalo limetaja viwango vya mikopo kwa madaraja tofauti katika matawi yake yote ya Mwanza, Dar es Salaam, Zanzibar, Arusha na Mbeya.
Waraka huo, unaonyesha kila mfanyakazi ataweza kukopa kati ya Sh 100milioni ikiwa ni kiwango cha juu na Sh 30 milioni kiwango cha chini kulingana na wadhifa wa mtumishi kwa ajili ya ujenzi wa nyumba.
Akizungumzia waraka huo, Gavana wa BoT Profesa Benno Ndulu, alisema ni utaratibu ambao benki imejiwekea ili kuwawezesha wafanyakazi wake kimaisha.
Profesa Ndulu, alisema BoT, ilijiwekea utaratibu huo baada ya kuangalia mahitaji ya msingi ya makazi kwa watumishi wake.
"Ni utaratibu ambao upo kwa karibu miaka 20 sasa, lakini sasa tumeuboresha kwa kuangalia mahitaji ya mikopo kwa umakini," alifafanua Gavana Ndulu.
Profesa Ndulu ambaye amekuwa katika mchakato wa kuisafisha taasisi hiyo ya fedha, aliweka bayana kwamba mikopo hiyo, imekuwa ikitolewa kwa umakini ili kuhakikisha inarejeshwa.
Alisisitiza kabla benki hiyo, haijatoa mikopo, inatafuta taarifa za wahusika ili kubaini kama wana madeni ndani na nje ya benki hiyo.
"Hatukopeshi tu bila kufuata utaratibu, vipo vigezo vya mtu kukopa mbali ya madaraja, tunaangalia madeni ya mtu ili tujue uwezo wake wa kurejesha," alisisitiza Ndulu.
Alisema kiutaratibu benki hiyo, inaangalia madeni ili kila mfanyakazi abaki angalau na theluthi moja ya mshahara baada ya kukatwa madeni anayodaiwa.
"Na wao ni binadamu kwa hiyo lazima tuhakikishe angalau, wanabakiwa japo na theluthi moja ya mshahara, baada ya makato," aliongeza gavana huyo.
Tuma maoni kwa Mhariri
Tatizo nililoliona ni ama watu wengine hawaelewi Role ya BOT au kwa makusudi mazima mtu anataka kupotosha ukweli au mtu mwingine anashindwa kutofautisha Benki Kuu na Benki zingine hivyo kushindwa kuelewa taratibu au Principles of Engagement and operations ambazo kwa BoT hazijalishi kama wewe ni mjama au simjaa, kwamba jukumu la benki kuu ni kuzisimamias Benki ili kuwe na level playing field kwa watoa huduma yaani Benki na kwa walaji ambao ndio sisi wakopaji, tuinaowekeza nk.Unajua kaka mie saa zengine sielewi sijui Rev.Kishoka na wenzio mtusaidie majibu ya maswali yafuatayo Kwanza BOT inafanya biashara???? Pili nini kazi ya BOT kama sio kufanya biashara. Tatu kwani wafanyakazi wa BOT hawawezi kwenda kukopa katika Commercial Banks BOT ikawaguarantee mikopo yao kwanini wang'ang'anie mikopo BOT??? Nne je Ndulu ameshindwa mawazo kama BOT inareserve kubwa ya cash kwanini asitoe mikopo kwa mabenki kwa riba ya chini ili mabenki nayo yatoe mikopo ya bei nafuu kwa wakulima??? Tano je hii mikopo tunahakika gani watanzania wengine watafaidika au ndio mwenye nacho ataongezewa na asiye nacho ndio kinachokuliwa ili wapate figure za kuwaonyesha World Bank kwamba nyumba za makaazi zimejengwa wapate kuongezewa pesa kumbe ni nyumba za watu wenye uwezo wa kujenga ndio wamepewa walengwa kalaghabao???? Mkinijibu maswali haya mie nitafahamu kwanini BOT inatoa mikopo but for now it does not make any sense to me.
In addition, someni makala ya raia mwema ya leo jamaa wanaanza kulalamikiana wao kwa wao wafanyakazi wa chini wanadai mikopo ya makarani ni midogo kuliko wanene BOT unajiuliza kumbe hii mikopo ni dili ehhh!!!!
Tatizo nililoliona ni ama watu wengine hawaelewi Role ya BOT au kwa makusudi mazima mtu anataka kupotosha ukweli au mtu mwingine anashindwa kutofautisha Benki Kuu na Benki zingine hivyo kushindwa kuelewa taratibu au Principles of Engagement and operations ambazo kwa BoT hazijalishi kama wewe ni mjama au simjaa, kwamba jukumu la benki kuu ni kuzisimamias Benki ili kuwe na level playing field kwa watoa huduma yaani Benki na kwa walaji ambao ndio sisi wakopaji, tuinaowekeza nk.
Na zaidi ya hapo ku-control mambo yanayo husiana na mzungulko wa Pesa iwe za nje au za ndani, ndio hapo Bot inapotakiwa kuishauri/kutoa angalizo na kuzuia transaction fulani ambazo hazina maslahi kwa taifa. kama hiyo ya ukodishaji wa mabehewa ya Rites na Management fees nk nk.
Waziri amesema kuna tatizo,wamesimamisha utoaji mikopo.MTAALAMU WETU WA BENKI KUU bwana KISHOKA UKO WAPI?
maana wewe ulisema tunawasingizia,
Mimi na August tuliwahi kusema mikopo hii ni hatari kwa uchumi wa Tanzania waichunguze Serikali. Sijajua wale waliokuwa wanasupport wanasemaje????