BoT yatoa ufafanuzi kuhusu taharuki ya noti za Shilingi 10,000 na 5,000 toleo la 2003

BoT yatoa ufafanuzi kuhusu taharuki ya noti za Shilingi 10,000 na 5,000 toleo la 2003

Sijapewa username bado

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2024
Posts
1,775
Reaction score
2,891
Benki Kuu ya Tanzania inapenda kutoa ufafanuzi kwa umma kuhusu taharuki iliyojitokeza kuhusiana na noti za shilingi 10,000 na 5,000 toleo la 2003 zinazopaswa kuondolewa kwenye mzunguko zinazofananishwa na noti za thamani hiyo toleo la 2010 zinazoendelea kutumika.

Zoezi la kubadilisha noti hizo lilianza rasmi tarehe 06 Januari 2025 na litafikia ukomo tarehe 05 Aprili 2025 kama ilivyoainishwa kupitia tangazo la Serikali namba 857 na 858 la tarehe 11 Oktoba 2024. Noti hizo za mwaka 2003 ambazo zinaondolewa kwenye mzunguko na kukoma kutumika kuanzia tarehe 06 Aprili 2025 ni kama zinavyonekana hapa chini.

1743833742339.png
Noti za Shilingi 10,000 na 5,000 ambazo ni toleo la 2010 na marejeo yake zinaendelea kutumika na hivyo hazihusiki kwenye zoezi hili la ubadilishwaji linaloendelea.

Noti hizo zina makundi ya sahihi za Waziri wa Fedha na Gavana wa Benki Kuu ambazo ni kati ya Saada Mkuya na Prof. Benno Ndulu, Mustafa Mkulo na Prof. Benno Ndulu, Dkt. Philip Mpango na Prof. Florens Luoga Pamoja na Dkt. Mwigulu Nchemba na Gavana Emmanuel Tutuba. Noti hizo ni kama zinavyoonekana hapa chini.

1743833800141.png


1743833825845.png

Pia soma
 

Attachments

Back
Top Bottom