Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hawajui tu namna wanavyoturudisha kwenye umaskin saiv Pay Pal ndio njia rahisi ya kufanya na kupokea malipo da kweli Bongo nyosoHa ha ha wanataka tutumie visa na Mastercard MKUU, even ipay imepigwa vannes no international translation in tz direct
Tanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au MarekaniKuna makundi na makundi ya vijana wasomi walionyimwa ajira wamejiajiri huko. Sasa nako wanapazuia. Nchi hii nani kairoga??
"vijana msisubiri serikali iwaajiri, tumieni ujuzi mlionao mjiajiri wenyewe." -serikali.
Fact, work smart not harderTanzania kumekuwa na tatizo kubwa la ajira. Njia moja ya kuondoa hilo tatizo ni kwa watu kutafuta kazi za kufanya online, yaani mitandaoni. Kazi zipo nyingi. Mfano, waweza pata kazi ya kutafsiri website ya kampuni au mtu kwa Kiswahili au kutafsiri kitabu. Unafanya online malipo yanakuwa kwa njia ya PayPal hata kwenye simu yako ya mkononi, hata mwajiri au mnunuzi awe Ulaya au Marekani
Pia, mtu waweza chora hata katuni, ramani za nyumba n.k ukauza online. Au, ukajitungia wimbo wako wa kienyeji binafsi nyumbani kwako bila hata kwenda studio, ukauweka kwa mfumo wa video au audio ukauuza online kwenye maduka kibao ya online.
Tatizo kwa Tanzania haijaruhusu matumizi ya kupokea pesa kwa njia ya PayPal ambapo mtu aki-click tu kununua bidhaa yako, pesa yako inaingia chapchap kwenye PayPal account yako.
Kenya walisharuhusu; vijana wengi hushinda mitandaoni wakitengeneza pesa wakiuza bidhaa zao, viwe vichekesho, michezo ya kuigiza n.k ambavyo huviuza online. Wanaweka clip zao kwenye maduka ya online mtu ananunua anamlipa online kupitia Paypal.
Kuna shughuli nyingi za ujasiliamali online. Kikwazo kwa nchi yetu ni upataji wa pesa wa kazi yako au mauzo yako online. Bado tuko enzi za mawe tukiamini minjia ya kizamani ya kupokea hela. Na hivyo kuifanya nchi yetu kuwa ni ya kulipa zaidi pesa za kigeni na si ya kupokea pesa za kigeni.
Serikali ikiruhusu upokeaji pesa kupitia PayPal itafanya vijana wengi waingie mitandaoni kutafuta pesa.
Biashara za online zaweza kufungua Watanzania wengi kupata pesa toka nje, sababu ni juhudi ya mtu binafsi tu auze nini. Waweza kujirekodi unarukaruka kama ngedere ukiimba hovyohovyo tu bila hata vyombo halafu ukaita wimbo Crazy Monkey Song ukauweka online na ukauza. Wapo watu wana pesa wanapenda vituko wananunua.
Taasisi za elimu nazo ziweke kwenye mitaala ujasiliamali wa online wasibakie tu kufundisha ujasiriamali wa kuzurura tu juani wa kimachinga.
Tanzania hatutaki kama unataka bitcoin hamia ulayaUnashauriwa kunyamaza kama hujui, bitcoin ni uwekezaji kama uwekezaji mwingine, btc imetengeneza mabilionare especially wale walio ikubali mwanzoni.
Nchi za wenzetu kuna ATM mashine za kuwithdraw btc ?
Bitcon inatumika kukopa kwny baadhi ya institutions kama dhamana. Kama ww ulikushinda basi
Wew na serikali hakuna wa kuzuiaTanzania hatutaki kama unataka bitcoin hamia ulaya
Inamaana Sisi twenye vibitcoins vyetu tumeshaliwa [emoji26]
Hivi kama wewe ulisomea udaktari na vifaa unavyo na hata madawa unayo unadhani ni sahihi ukaanza kutibu watu nyumbani kwako bila kufuata taratibu kwa kisingizio cha kuokoa maisha ya watu?Kaka Achana na transaction ,
Kuna Watu wamewekeza milion of money?
Inamaana kama serikali imeshindwa kuitambua ! Vp kuhusu hao watu?
Naje vp tutafika uchumi wa kati kwa style hii
Swali kwann mnahusisha currency nyingine za kawaida tulizoziea?Umeliwa vipi mbona bado zinauzwa na kununuliwa kama kawaida?
Umeliwa vipi mbona bado zinauzwa na kununuliwa kama kawaida?