Habari wana jukwaa,
Kabla ya kuanza huu uzi napenda kunukuu maneno ya marehemu Ruge "Ogopa sana Mungu na technology".
Haya sasa naomba niulize je tunawezaje kusonga mbele pasipo technology? Na je teknolojia inazuilika? Zipi hasara za kuizuia au kuchelewa kuifahamu?
Binadamu amepitia zama nyingi sana kama zama za mawe, chuma n.k. Sasa lengo la zama au vipindi vyote hivyo ni kuweza kuyakabili mazingira na changamoto za kiuchumi, kiutamaduni n.k ndani yake.
Zama tulizonazo sasa ni zama za sayansi na teknolojia na hii ni katika nyanja za kiuchumi, kiutamaduni, na kijamii mambo mengi yanaenda na sayansi.
Ajabu ni kwamba BoT anashindwa kuendana nayo kwa sababu dhaifu. BoT kama chombo kikubwa cha usimamizi wa fedha imetangaza kutoitambua pesa ya kidigitali maarufu kama Cryptocurrency.
Na hii imekuja kutokana na Wimbi la watu wengi kuingia kuwekeza huko. Na maana yake hii biashara inaenda kufa Tanzania. Je hii ni sawa?
Na vipi kuhusu watu waliyowekeza mamilioni huko? Ila vipi fursa ya biashara hii kwa siku za usoni?
China ilikuwa miongoni mwa nchi zilizopiga marufuku biashara hii. Lakini sasa imeruhusu hii biashara na kusababisha kuongezeka thamani nafikiri kwa watu mnaofuatilia mmeliona hili, Marekani ni moja ya nchi ambayo mabilionea wake wamewekeza kwenye Cryptocurrency.
Na sasa ukienda nchi zilizoendelea kuna ATM za Cryptocurrency (Bitcoin), pia
Kuna makampuni yanayotoa mikopo kwa dhamana ya Bitcoin.
Je Tanzania kwa kupitia BoT hawaoni fursa ya nchi kubwa kuwekeza huko. Kama sijakosea hata Rais wa Kenya Mr. Kenyatta aliongelea positive hii biashara.
Tanzania tunakwama wapi? Kwa mtazamo wangu naenda kinyume na BoT kwa kutoa sababu dhaifu.
View attachment 1261444