boxsi la chaki na shilingi elfu mbili ili apewe barua

boxsi la chaki na shilingi elfu mbili ili apewe barua

John porter

Member
Joined
Jul 8, 2013
Posts
65
Reaction score
28
Habari zenu wana JF
Nina mdogo wangu amemaliza la saba mwaka jana.. Tunamshukuru Mungu amefaulu vizuri sana na amebahatika kuchaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza..

Utata unakuja baada ya mdogo wangu huyo kwenda kuchukua barua inayomtambulisha kuwa amefaulu.. Ndipo walimu wao wanawaambia huwezi kuchukua barua bila kuleta boxsi zima la chaki na shilingi Elfu mbili..

Je hili swala ni haki? Lipo kisheria? Au walimu wameamua kujipatia pesa ya chai kwa kuwanyonya hawa wanafunzi?

Nawasilisha..
 
yap ni sahihi kabisa hiyo 2000/- ni kwa ajil ya hizo form na box la chak ni kwa ajil ya kuanzia muhula tena bado anatakiwa alete bunda la karatasi,jembe,ndoo ya lita 10 na slesha kama unafikir vitu hiv nigharama sana mpeleke kuleeee st.....
 
Acha Ubahiri Wa Kishamba, kama unaona chaki na elf mbili ni kubwa mpe mtaji mdogo wako aendelee kuuza vitumbua,ukiambiwa bia 2000/= na kiroba 1100/=.Hushangai Ila Elmu Ndo Unatafta Hadi Ushauri.
 
Acha Ubahiri Wa Kishamba, kama unaona chaki na elf mbili ni kubwa mpe mtaji mdogo wako aendelee kuuza vitumbua,ukiambiwa bia 2000/= na kiroba 1100/=.Hushangai Ila Elmu Ndo Unatafta Hadi Ushauri.

Kaka umenena point kubwa xana, hizi shule za kata ni mali ya wananchi xaxa wewe unataka akulipie nani mwanao akaxome bure, kama hyo hela na chaki ni mali mpeleke shule za Private ili usilalame.
 
yap ni sahihi kabisa hiyo 2000/- ni kwa ajil ya hizo form na box la chak ni kwa ajil ya kuanzia muhula tena bado anatakiwa alete bunda la karatasi,jembe,ndoo ya lita 10 na slesha kama unafikir vitu hiv nigharama sana mpeleke kuleeee st.....

Relax then,soma vizuri tena kwa umakini
 
Acha Ubahiri Wa Kishamba, kama unaona chaki na elf mbili ni kubwa mpe mtaji mdogo wako aendelee kuuza vitumbua,ukiambiwa bia 2000/= na kiroba 1100/=.Hushangai Ila Elmu Ndo Unatafta Hadi Ushauri.

soma tena......
 
Habari zenu wana JF
Nina mdogo wangu amemaliza la saba mwaka jana.. Tunamshukuru Mungu amefaulu vizuri sana na amebahatika kuchaguliwa kuendelea na kidato cha kwanza..

Utata unakuja baada ya mdogo wangu huyo kwenda kuchukua barua inayomtambulisha kuwa amefaulu.. Ndipo walimu wao wanawaambia huwezi kuchukua barua bila kuleta boxsi zima la chaki na shilingi Elfu mbili..

Je hili swala ni haki? Lipo kisheria? Au walimu wameamua kujipatia pesa ya chai kwa kuwanyonya hawa wanafunzi?

Nawasilisha..

maswali yako ni mazuri ila ni vigumu kuwajibia walimu ingekuwa vyema km nasi ungetupa majibu ya maswali yako baada ya kuwauliza walm husika zaidi ya hapo unaweza kuta hayo yalikuwa madeni ya mwanafunzi aliyokuwa anadaiwa kulingana na utaratibu wa shule husika!
 
2000/=Tu unaona ubahili wakati amefaulu sasa hapo ni mwanzo je akishajiunga ukisikia mchango wa assemble utafanyaje?
 
Kisheria si halali na hairuhusiwi. Ila ninachoona gharama ya kwenda kutafuta haki mbele ya sheria ni gharama zaidi kuliko kutoa hiyo chaki na sh. 2000. Amua mojawapo
 
wee vp? lete box hilo,na elfu 2 ya maziwa ala..nani anapenda kubugia michaki bila maziwa?
 
Chaki? Ndo mmeona shida? Mbona kuna shule unalazimika kupeleka kilo 50 za mahindi ndo mwanao apokelewe sekondari!
 
bajeti ya serikali imefika kikomo kiasi cha kuchelewa kupeleka hela za kuendesha shule kwa wakati,ili waendelee kusoma ni bora wachaange
 
Kuna taratibu zinazotumika kama by law kwa baadhi ya shule tu inawezekana kabisa walikubaliana hilo swala kwenye vikao vya walimu, wazazi na bodi za hule na yakapitishwa.
Kwani hukuona juzi ITV wananchi wa Morogoro wagmbana kupinga mchango wa Tshs 50,000/= ili kumuandikisha mtoto wa kuanza DRS 1?
 
shule ina mandate ya kufanya hvyo.cha msingi makubaliano ya walim na bodi ya shule.bodi inawaklsha wananchi.so sheria inatambua hlo.
 
Back
Top Bottom