Brake Master Cylinder: mafuta ya brake kuvujia kwenye booster housing. Nini tatizo? Nini tiba?

Hivi kumbe ukibadilisha hizi Dots vinakufa? Didn't know!

Hata mimi nimejifunza kitu. Kumbe hizi DOTS hazitakiwi kubadilishwa.

Ila sasahivi sokoni dot 3 imekuwa adimu, wauzaji wanasema eti dot 3 imeshapigwa marufuku na mamlaka duniani sababu ya mazingira. Inakanganya.
 
Kubadili master cylinder yote complete. Okay.

Hivi kununua master mpya ya kichina (aftermarket) ina ubora?

Maana spea used/mtumba za kijapan huwa ni bahati nasibu Sana.
Aftermarket haitafanya kazi kwa ufanisi ule ule by 100% na ziko prone to failure. Used za kutoka na gari huwa ukibahatisha nzuri inakuwa sawa sana
 
Kama hela ipo funga master cylinder Mpya
 
Wengi huweka DOT 4 kwakua ndio inapatikana kwa wingi sana madukani. DOT 3 kuna kipindi ilihadimika sana

Hiyo ni kweli kabisa. Dot 3 imeanza kuwa adimu, hata mafundi ukimuambia akuwekee dot 3 unamuona kabisa anavyokushangaa.

Na mafundi wetu wengi hawa wa mtaani wanakwambia eti dot 3 inakuwa replaced na dot 4 bila shida yoyote.

Hizi mambo zinakanganya.
 
Mi ilishaniulia master cylinder nikabadili ila sahizi brake ipo kama haipo. So spongy

Ulibadili master na ukaweka recommended fluid dot 3, Ila brake ipo spongy?!!

Basi hapo yawezekana na booster ilishaumia. Badili na booster.
 
Ulibadili master na ukaweka recommended fluid dot 3, Ila brake ipo spongy?!!

Basi hapo yawezekana na booster ilishaumia. Badili na booster.
eeh nimekuwa nikiweka Dot 3 sema master ya dukani
 
Hiyo ni kweli kabisa. Dot 3 imeanza kuwa adimu, hata mafundi ukimuambia akuwekee dot 3 unamuona kabisa anavyokushangaa.

Na mafundi wetu wengi hawa wa mtaani wanakwambia eti dot 3 inakuwa replaced na dot 4 bila shida yoyote.

Hizi mambo zinakanganya.
Anakuchomesha yani hapo we katafute Dot 3 kariakoo hadi uipate
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…