Kuna fast charge za aina tofauti kulingana na namna simu inavyosapoti.
- Kuna simu zinazosapoti fast charging kwa fixed current na fixed voltage(Mfano: 5V, 2A). Kwa aina hii ya simu basi ukipata charger yoyote inayotoa 5V, na current ya kuanzia 2A na kuendelea, basi itafaa kutumika kwenye simu hiyo.
- Kuna adaptive fast charging ambayo simu inapokea voltage na current tofauti kulingana level ya battery kwa wakati huo, kwa mfano battery ikiwa na 0% - 50% , simu inapokea 12V, 0.5A, battery ikifika 51%-80% simu inapokea 7V, 1.5A, kuanzia 81%-100% simu inapokea 5V,2A. Sasa huu ni mfano tu. Kwa mfano huu ni lazima upate charger inayokubalika na simu husika, kwa sababu kunakuwa na mawasiliano kati ya simu na charger.