Nikizungumza kama mtu wa marketing ngazi fulani ya elimu, nimeona makampuni mengi sana yana apply strategies kutoka marketing research proposals za miaka ya nyuma sana yani zinashindwa kwenda na wakati.
Ni kweli wasafi soap wamesahau kuwa maudhui haya ya uswahili wa vigoma na singeli vimekwishapita na wakati. Wakati huu vipo vitu vilivyoteka sana hisia za watu ambavyo wangeweza kuvitumia kutambulisha bidhaa na kuikuza.
Kwa utafiti mdogo tu, kwasasa zipo tasnia kadhaa ambazo zinafuatiliwa zaidi mfano, comedians especially stand up comedians, watu wa michezo hususani wachezaji lakini pia michezo hii ya tamthilia sitozitaja jina zimeteka asilimia kubwa sana ya watu wa jinsia zote, boss DIAMOND akaechinj na vijana wapange namna ya kupenya humu aisee hizi bidhaa zitafahamika sana.
Kama mpo humu watu wa wasafi soap wekeni milango wazi ya kupokea proposal za watu wenye mawazo yenye tija badalayake wekeni pembeni sifa na experience za makaratasi wengi wao wafanyakazi wenu wamekulia masaki wanakariri chunguzi za watu wengine, tunayoijua mitaa tupo mtaani.
Sio vyema kusema mlikurupuka ila kabla ya ku introduce bidhaa research ni muhimu, pili effective marketing strategy and planning na mwsh ni watu wa ku execute hyo plan.
All the best wasafi soap.