Bravo nao wamebebwa?

Mnao uzoefu wa kwenda kushitaki CAS na kuandamana kwenda kushitaki Ikulu kwa mama . Nadhani huu ni muda sahihi kwenu sasa kufanya hivyo.
 
Eti hakukua na ucheleweshwaji wa mpira!!!

Goli kips wao kalala mara ngapi?

Wachezaji wao wametolewa na machela mara ngapi tena wakiwa hawajaumia.!!!!

Mnataka kutufanya wengine hatuna macho tunaangalia mpira Kwa makalio sio?
Nashauri FIFA walete Sheria mchezaji akijifanya kaumia akabebwa na machela atulizwe nje kwa dakika zisizopungua 2 kisha ndio aruhusiwe kuingia.
 
Ingekuwa kuna hesabu minimum na maximum kwenye dakika za nyongeza mngelalamika kule Morocco kuwa mwamuzi kawaonea? Likiwakuta nyie mwamuzi kawaonea ila likiwa favor nyie mnasema kuna minimum na maximum kwenye dakika za nyongeza.
Waliolalamika pia huko Morocco walilalamika kwa ushabiki tu.Hakuna official complaint.Tofautisha timu ikialamika na mashabiki kama wewe wakilalamika.
 
Furaha ya ushindi inawafanya wasione hilo.
 
Kama baada ya dk hizo Simba wangefungwa ungekuwa na ujasiri wa kuandika kuwa CS Faxien wamebebwa? dk zilizoongezwa ni kwa ajili ya Simba tu?
Mpira ni mchezo wa malengo. Kuna mechi Simba nae atatamani mpira uishie maana malengo yake yametimia tayari. Hawachezi tu.
 
Tumia akili kufikilia. Umepewa na mfano hapo juu na memba mmoja kuwa kuna mechi imeongezwa dakika 4 zingine baada ya dakika za nyongeza. Na hapo unasemaje?
Kwanini hili swali mnalikwepa? Baada ya kuongezwa dakika 7 palitokea tukio lolote la kupoteza muda?
 
Na ile yellow ilitakiwa kuwa red card kwa ukuta wa yerico.
 
Hizo dakika mbili unazozilalamikia hata wao walikuwa wanatafuta goli, walipopoteza mpira ikapigwa counter attack, pass ndefu ikamkuta Kibu D mkandaji akaweka chuma.
 
Kwa hiyo refa aliongeza dakika mbili ili Simba wafunge?
 
Reactions: Tui
Kama dakika zinaongezwa halafu pia zinachezewa vibaya lazima muda uongezwe kufidia unaopotezwa
 
Sio tu Muda ulizidishwa bila sababu na kwa Mazingira ya Rushwa lakini Refa Ali uinamisha uwanja kwa Muda mrefu.
Chem alone akiwa Last Man anamshika mtu alistahili red card, wageni wakichezewa faul refa anapeta Mwenyeji akijiangusha refa anatoa faul.

Waarabu walivumilia kupita kiasi ila Refa Ali lazimisha apigwe.

Refa aliye chezesha JKT Tanzania na Pamba hakua na tofauti yoyote na aliye chezesha Jana.
Ni aibu kwa marefa wa aina hii, Refa ndiye aliye sababisha taharuki na vurugu za Mashabiki kurushiana viti majukwaani.
 
Kama baada ya dk hizo Simba wangefungwa ungekuwa na ujasiri wa kuandika kuwa CS Faxien wamebebwa? dk zilizoongezwa ni kwa ajili ya Simba tu?
Nakujibu hapa hapa.
Mpira ni mchezo uliojikita kwenye muda, wachezaji na waalimu wao hutumia nguvu na akili kubwa kupanga mikakati yao kwa kuzingatia muda. Hakuna namna mwamuzi akachezesha nje ya muda bila kuathiri timu husika.

Timu inayosaka matokeo positive huku ikiwa nyuma hutamani muda wa kucheza usiishe na timu iliyo mbele kwa matokeo positivie hutamani muda uishe wakati wowote Sasa kwa kuwa refa hayuko upande wowote, usahihi wa kumaliza mchezo katika muda sahihi ni jambo muhimu na lazima kwake. Tofauti na hivyo atakuwa anapendelea upande fulani.

Wale waarabu hawakuwa na haja yoyote ya muda kuongezwa hata sekunde moja, Simba tulikuwa na sababu zote za haja ya muda kuongezwa hata sekunde moja.

Swali linarudi pale pale, kama muda wa nyongeza ulikuwa ni Dakika 7 tu, sasa baada ya dakika 7 kwisha, mbali na akili ya mwamuzi, nani alijua mchezo utaendelea kwa muda gani zaidi?
 
Taja tukio lolote lililopoteza muda baada kuongezwa zile dakika 7
Law of game inasema
The fourth official indicates the minimum additional time decided by the
referee at the end of the final minute of each half. The additional time may be
increased by the referee but not reduced.
 
Reactions: Tui
Kwanini hili swali mnalikwepa? Baada ya kuongezwa dakika 7 palitokea tukio lolote la kupoteza muda?
Tatizo lako ni uelewa.Dakika 7 ni minimum kwenye kuongeza.Maximum ni kufuata stopwatch ya Refa.
Just curious unalalama kwani Utopolo mechi mlicheza nyinyi?Au mmegeuka VAR ya mawakili wa kujitolea?
 
Nani kakuambia muda wa nyongeza ulikuwa dakika 7 TU?Hiyo TU unaitoa wapi?Jifunze law of the game inasemaje kuhusu added minutes in each half.Kuongelea usichokijua ni ujuha.
 
Aliyesema muda ni dk 7 ni nani? unajua sheria ya FIFA inayohusiana na muda inasemaje? je refa aliivunja? unatoa maoni kwa kuzingatia sheria husika au ni mapenzi yako tu. Unajua kuwa hizo dakika ni minimum na sheria imempa refa mamlaka ya kuongeza muda kadiri aonavyo inafaa? Tazama sheria hii hapa chini inavyosema halafu useme refa ameivunja vipi?Ukizingatia kuwa post hii inazungumzia sheria husika
 

Attachments

  • Screenshot_20241216-095927.png
    668 KB · Views: 2
Tatizo lugha wengi wanakurupuka bila kujua sheria ya added minutes inafanyaje kazi.
 
Acheni siasa kwenye mpira kama refa alifanya makosa kuna vyombo vinavyohusika kutoa adhabu iwapo itaonekana alivulunda mchezo.nyinyi mnatembea na hisia zetu na mnaacha kwenda na uhalisia ndo maana mpira wetu Tz haujui sababu ya hisia zenu za Uyanga na usimba.Ni aibu.
 
Yaani walivyokuwa wanajiangusha hovyo haukuona hadi unaongea hivo?

Bora uache kushabikia na kuangalia mpira kwa hali hiyo.
Usichange mambo, rudia kusoma.
Issue kubwa inayozungumziwa hapa, ni nini kilimzuia refa kumaliza mpira baada ya dakika saba za kufidia mchezo kumalizika?
Refa alipanga mchezo uchezwe dakika ngapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…