Nakujibu hapa hapa.
Mpira ni mchezo uliojikita kwenye muda, wachezaji na waalimu wao hutumia nguvu na akili kubwa kupanga mikakati yao kwa kuzingatia muda. Hakuna namna mwamuzi akachezesha nje ya muda bila kuathiri timu husika.
Timu inayosaka matokeo positive huku ikiwa nyuma hutamani muda wa kucheza usiishe na timu iliyo mbele kwa matokeo positivie hutamani muda uishe wakati wowote Sasa kwa kuwa refa hayuko upande wowote, usahihi wa kumaliza mchezo katika muda sahihi ni jambo muhimu na lazima kwake. Tofauti na hivyo atakuwa anapendelea upande fulani.
Wale waarabu hawakuwa na haja yoyote ya muda kuongezwa hata sekunde moja, Simba tulikuwa na sababu zote za haja ya muda kuongezwa hata sekunde moja.
Swali linarudi pale pale, kama muda wa nyongeza ulikuwa ni Dakika 7 tu, sasa baada ya dakika 7 kwisha, mbali na akili ya mwamuzi, nani alijua mchezo utaendelea kwa muda gani zaidi?