Brazil au Argentina mmoja bingwa Kombe la Dunia

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
12,706
Reaction score
52,355
Naiona kabisa Brazil Au Argentina wakichukua Kombe la Dunia kwasababu moja tu, timu nyingi za Ulaya huwa hazina bahati sana zinapocheza Kombe la Dunia nje ya Ulaya.

Ukindoa hiyo hoja mwaka huu, Brazil wana kikosi kinachokaribia kile cha mwaka 2002 ingawa siyo kwa asilimia kubwa. Pia Argentina ana kikosi cha wapambanaji kama kile cha Maradona cha mwaka 1986.

Pia ukienda na hii rekodi ya 1998 na 2018 Ufaransa, 2002 na 2022 inaweza kuwa Brazil, wakiwa na bahati mwaka huu ni wao.

Mwaka huu moto utawaka, ila natabiri kati ya Brazil au Argentina mmoja atachukua Kombe la Dunia 2022.
 
Hakuna ata timu Moja katika izo itakayocheza nusu final, America ya kusini kwasasa hawatishi Tena Wana majina ila watu hawana.
 
Hao Brazil, Argentina ni wazuri huko huko kwao.Hao hata Netherland na England zitawatoa jasho. Oops nilisahau Serbia na Portugal.
 
Ufaransa
Uholanzi
Ujerumani,
spain,
brazil,
england.
agentina.

hawa viumbe nimeorodhesha hapa juu mmoja wapo lazima awe bingwa.
 
Malizia tu, kombe linaenda kwa Malkia.

Tumempoteza Malkia, tutajifariji kwa taji.

It's coming home
It is not going to happen
Uingereza hana timu ya maana ukitoa kelele zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…