BRAZIL: Mtanzania, Felix Alphonce Simbu ashika nafasi ya 5 katika Marathon za Olimpiki

Nape: Chukua huyu jamaa na yule dada wa kichaga wa kuogelea (Ingawa anaongea kiswangish) waweke kambini mpaka Olympic ijayo.
 
Simbu. ..msema ukweli ni mpenzi wa Mungu....umetutumikia kweli kweli....
 
....wabongo bana...watu wa vitu kidogo...mtu hajashinda imekua breaking news duh!...akirudi mpelekeni bungeni pia...ama ikulu akapewe mkono na mkulu...LOL...tunaporidhika na vitu vidogo kamwe vikubwa itakuwa ndoto kuvipata...tuwaige wakenya....tuko nao jirani....tunafanana kimaumbile...hali ya hewa kwao kama kwetu...mbona wao wanaongoza kwa bara la Africa???....tusipojiuliza na kupata majibu...na kuyafanyia kazi tutabaki kuwa wasindikizaji...huku tukijisifu....
 
🙁Wabongo bana sijui lini tutaacha ushamba, hata hii inapostiwa humu? Mtu kashika nafac ya 5?

Tubadilike jamani, sio kila ukionacho ukipost....
 
Kiukweli katutoa kimasomaso tukatamkwa kabla ya Olympic kuisha.
 
Kenya medals 10
Tanzania medal 0
Hivi Tumbotumbo kazi yake kubwa ni kufungia tu magazeti?
Kutayarisha teams kwa mashindano makubwa siyo kazi yake
 
Nape: Chukua huyu jamaa na yule dada wa kichaga wa kuogelea (Ingawa anaongea kiswangish) waweke kambini mpaka Olympic ijayo.
Afu atayajibu magazeti sa ngapi? Kwenye issue ksma hizi hutamuona Nape.. Ukitaka kumuona Nape gazeti limuandike jpm vibaya
 
Hata kama Bwana Simbu hakupata medali, ni lazima apongezwe kwani baada ya mbio za zaidi ya saa mbili, huyo mshindi wa Gold kamzidi dakika mbili na nusu tu wakati kuna watu waliioachwa ka karibu dakika 45 na wengine kushindwa kumaliza!
 
Juma Ikangaa aliwahi kushika nafasi ya 6.


Huyo jamaa mashindano kama haya ya kitaifa yaani bila zawadi ya fedha kwa mshindi alikuwa hashindi.
Zile Marathoni za malipo kwa washindi kama vile Fukuoka , Boston , London, au Berlin Marathoni alikuwa anashinda sana tu.
 
Hivi hao wanawake wanaobeba karai la medali walichaguliwa kwa kuangalia shepu za miguu yao? Naona wote wanafanana miguu!
 
Hilo jina la simbu naona kama linafanana na WANYATURU wa singida. Nimewahi kuishi vijijini singida kuna watu wanakimbia ni balaa. Mimi ninadhani nguvu tunayoitumia na fedha tunazozitumia kwenye football mara HISA, mara VIKOBA mara KUKODISHWA tungezitumia kwenye riadha , kurusha mkuki na long jump kwa kuandaa mashindano ya riadha kuanzia ngazi ya kijiji hadi taifa HAKUNA TAIFA LOLOTE LA AFRICA LINGEFUA DAFU MBELE YA BONGO
 
Nguvu na rasilimali za kudhibiti upinzani zingeelekezwa kwenye michezo tungefika mbali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…