BRAZIL: Mtanzania, Felix Alphonce Simbu ashika nafasi ya 5 katika Marathon za Olimpiki


Wewe vipi? Au uko ugaibuni umesahau uTanzania wako?
Kua wa 5 is a big deal. Lini ulisha wahi kuona bendera ya Tanzania kwenye bango la Olimpiks?
 
Nimeangali Olympic yote, nasema kwa uhakika kabisa 'HII NI AIBU KUBWA SANA'

Tanzania tulikuwa katika eneo la gold au Silver. Nyakati hizo akina Filbert Bayi wanatamba

Huwezi kuamini nikikueleza huyo Mtanzania ndiye wa kwanza 'kuonekana' japo katika 5 bora

Hiyo siyo nafasi ya kujivunia hata kidogo. Ukiangalia Wakenya, Waganda, Waethiopia walivyotawala hasa riadha, inasikitisha sana kwa Taifa letu

Kuna vitaifa vina watu chini ya 250K vina medali. Kwetu sisi tunajivunia nafasi ya 5!!!

Haya ni matokeo ya kutokuwa na maandalizi. Wizara ya michezo inatakiwa mtu wa Michezo, committed na anayejua tunataka nini.

Wenzetu leo hii wapo katika drawing boards wakitazama Tokyo 2020.

Hivi kweli hatuna watu wanaojua kuogelea wakaandaliwa kimashindano? Hivi kweli hatuna watu wanaokimbia siku hizi hadi tubaki tunashangalia mataifa jirani

Shame on you Tz, Shame on you!
 
Duh, sasa hapa kina MK254 na kina NairobiWalker watatuona mazuzu kama nafasi ya tano tunakuja anzisha uzi, wao waanzishe nini??ila nitawaelewa!
Anyway, hongera zake ila ALMOST DOESN'T COUNT!
Vitu vingine ni vizuri kwetu Tz ila tuwe tunachuna.
 
Amejitahidi kwa kujaribu cha msingi aangaliwe kwa ukaribu maandalizi mazuri ili mashindano mengine afanye vizuri zaidi na si kuachwa hivi hivi.
 
apokelewe kishujaa halafu apelekwe bungeni.... ajengewe nyumba apewe gari n.k
 
..huyu kijana akiwa trained vizuri anaweza kushinda marathon.

..zaidi tuwekeze kwenye riadha haswa mbio ndefu.

..nimeona USA wamepata medali kwenye marathon na meter 1500. Hayo ni matokeo ya wao kuwekeza kwenye mbio za masafa marefu.
 
Tanzania tuna safari ndefu katika hili hadi tunatia huruma! Kwenye soka kila wakati sisi huwa tunakufa kiume! Yanga kesho akimuotea Mazembe nae atakuwa ametolewa kiume! Na kweli huwa tunatolewa kiume na labda kupachikwa kale kakiungo pendwa kalimkomshinda uzalendo hata Braza Adam! Last week kuna mwogeleaji mmoja kasifiwa weeeeeeee; nae alitolewa kiume!
 
Nashindwa kabisa kusema kusifia mtu hapati medali yeyote ila tunajadili kujitahidi pale sio eneo la ajali pale watu wanapambanaa eti kiume, sasa unaanza kusifia chenga wakati huna goli, ? Tukae chini tulie na nafsi zetu zinazoshindwa kila Leo.
Duh, nakubali tulie kweli, kisha tufute machozi, tujipange ki hapa kazi, olympic ijayo 3 za juu zote zetu. Tuanze sasa hii habari ya kusubiri bado miezi 2 siyo sahihi kabisa 'Proper Planning Prevents Poor Performance'.
 
Ni wakati sasa wa serikali kuwekeza kwenye riadha.Hasa wilaya ya Ikungi mashariki.waende viijiji vya Mwisi,Mampando na Ntuntu.Huko kina Simbu wako wengi sana.
 
Aidha serikali itambue kuwa kina Samsoni Ramadhani na Isegwe waliowahi kushinda medali ni watoto wa sgd.Huyo simbu sijui Sara Ramadhani ni wa sgd.Sasa kulikuwa na sababu kweli ya kuweka kambi kilimanjaro? Unaweka watu kambini hamna hata chakula unategemea nini,SERIKALI WEKEZENI IKUNGI! Kama hatujapata medali kibao tu.
 
Lissu njoo na mpango mkakati wa kuinua Riadha
 
Pongezi zimfikie popote alipo.

Tunaweza kufanya vizuri zaidi kama maandalizi yataboreshwa
 
Ni wakati sasa wa serikali kuwekeza kwenye riadha.Hasa wilaya ya Ikungi mashariki.waende viijiji vya Mwisi,Mampando na Ntuntu.Huko kina Simbu wako wengi sana.

Fun Fact: Serikali ya marekani haina wizara ya michezo, lakini pale RIO wameondoka na medali 121. 😱
 
Nafasi ya tano yupo mbali japo kajitahidi aongeze juhudi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…