Brazil to play Tanzania in a friendly

Brazil to play Tanzania in a friendly

Tusubiri sasa mahesabu ya mpato yatatolewa baada ya wiki mbili

Milioni 300 kwenda juu kwa makadirio ya haraka haraka ukishaondoa watakazoiba.....bado ni hasara tu
 
nia kubwa ilikuwa kutangaza nchi sasa mbona sijaona coverage ya Brazil kufika bongo kwenye vyombo vya habari?

Kwenye ESPN vivo sport online walikuwa wanatangaza na pia mmewalipa hela nyingi na biashara zao zimekuwa haswa zikitangazwa ukizingatia mabango yalionekana wakati kamera zikiwanasa wachezaji. Au kwa maana nyingine matangazo yao yako mbele na ya Chui laga, NMB yako kuleee nyuma kudadeki masharti magumu.

ESPN huwa ni wababe wa dunia mangi wako vizuri sana tena dunia nzima. Hiyo South America ni wao kwani ndo wanaongea kireno na spanish na hata America ya kaskazini mexico na USA pia mechi hii imetizamwa. Nimeona waati mechi imeisha wameanza kuonyehsa Mexico ikicheza pia. Acha ulaya sasa.
 
Abdulhalim, si nchi imetangazwa katika nchi 160 duniani? Sasa tusubiri kuona idadi ya Watalii itakavyomiminika kutoka katika hizo nchi 160. Hii amount waliyolipwa Wabrazil inabadilika kila leo sijui kama tutajua kiasi cha kweli walicholipwa maana tumeshasikia $6 miilion, $3 million na sasa $2.5 million.
IMO, naona contract ya Wabrazil ni hiyohiyo 2.5, ila tabaka tawala kupitia Kigumu chama cha mapinduzi kinaeza kikawa kinakazia swaumu ile (6-2.5) kwene account yao ya 'mengineyo'..Close call.
 
Eti Golikipa wetu ni mtu wa karibu sana na mkuu Balatamba, Arsene Wenger, masanilo!........ Nilimuona wapi vile?....Yaani as if ndio siku yake ya kwanza kudaka.....
 
Hahaaaaaaaaaaaaa.......Nimefurahi sana leo mie........Tumefungwa mkono(05) na pia mahudhurio yamekuwa hafifu mnoo,dua zngu na wengine zimesikilizwa.....TFF imekula kwao leo.......hahaaaaaaaaa

Hope hili ni fundisho tosha
Walitangaza kwa mbwembwe, Tiketi daraja la kwanza A zimeisha, na wamshukuru Manji kuwalipia wanachama wote wa Yanga. Ilitakiwa Ticketi zianze uzwa wiki moja iliyopita, halafu jana na leo wangeshusha mzunguuko mpaka alfu 10,000 baada ya kuona mauzo hafifu. Ila ndiyo hivyo tena, poor strategy.
 
IMO, naona contract ya Wabrazil ni hiyohiyo 2.5, ila tabaka tawala kupitia Kigumu chama cha mapinduzi kinaeza kikawa kinakazia swaumu ile (6-2.5) kwene account yao ya 'mengineyo'..Close call.

Inawezekana kabisa...kwamba $3.5 millioni imeingia katika mfuko wa chama kwa maandalizi ya kuelekea October 31, 2010
 
hawa Brazil kama inawezekana kusema kweli bora waondoke na ndugu yao Maximo july naona mbali sana.


huyu kipa kusema kweli kanikera sana na wala Brazil isiwe kigezo cha kumtetea na imeweza kuonesha uwezo mbovu wa Maximo.
 
Nina hasira za dhati kwa walioandaa hii mechi bila kutangaza vivutio vyetu ipasavyo.Hakuna Kilimanjaro,zanzibar,manyara,ngorongoro,gombe,ruaha....,hyo mjinga aliyeweka tangazo la Serengeti as if liko indoor ana matatizo ya akili.
Ni wakati muafaka hawa wazee wakaondoka sasa na hayo matoto yao yasiyo na kitu kichwani wakayaache yaendelea kupumzika kwenye masofa nyumbani.This was a big opportunity lost.

Say it again bro. Kamuulize waziri wa michezo, na yule wa maliasili na utalii, kama vichwa vyao vina hata tone la ubongo. Hii ndiyo mechi pekee iliyoonyeshwa kimataifa na television mbalimbali duniani, badala yake naona hata uwanjani tunatangaza NMB. Mapumziko watu wanatangaza mambo yao binafsi. Ukiuliza utaambiwa hakukuwa na fungu la kuwekea matangazo. Sasa nia ya kutumia bilioni nne ilikuwa ni nini? Hawa wazee washajichokea, hawana lolote tena la maana kwa nchi yetu.
 
yani bifu la maximo na kaseja ndio limeenda kutuletea hili kipa kweli kiboko.kama kaseja hana nidhamu basi na maximo pia hana nidhamu kwa kumchagua kipa kama huyu.


hii mechi imetuongezea umaskini kusema kweli.

Maximo bora aende zake tu....Ukiachilia Kaseja pia ana Bifu na Athumani Idd 'Chuji' na Haruna Moshi 'Boban'
 
Eti Golikipa wetu ni mtu wa karibu sana na mkuu Balatamba, Arsene Wenger, masanilo!........ Nilimuona wapi vile?....Yaani as if ndio siku yake ya kwanza kudaka.....

Namkumbuka Ivo Mapunda!
 
Say it again bro. Kamuulize waziri wa michezo, na yule wa maliasili na utalii, kama vichwa vyao vina hata tone la ubongo. Hii ndiyo mechi pekee iliyoonyeshwa kimataifa na television mbalimbali duniani, badala yake naona hata uwanjani tunatangaza NMB. Mapumziko watu wanatangaza mambo yao binafsi. Ukiuliza utaambiwa hakukuwa na fungu la kuwekea matangazo. Sasa nia ya kutumia bilioni nne ilikuwa ni nini? Hawa wazee washajichokea, hawana lolote tena la maana kwa nchi yetu.
As you said it,viongozi wetu something is missing between their ears.
 
Mkuu, wewe humfahamu Dani. Jamaa ni kama kichaa vile na wenzake wanasema hata kwenye maoezi anaweza kukuweka vitu. Siku walishinda, walitaka na yeye aseme kitu baada ya mechi, Kwanza alikataa kabisaa na mwisho wakambeba mwisho akashika Microphone. Kichwani ukamwijia wimbo mpya wa SHAKIRA ulio kwenye staili ya Champeta au Soukous ya Brazil.



Ila yeye akaimba kivyake.


jamaa baada kutangaza utalii kwa kumrudishia ngumi alves anamuangalia tu .


hili kipa dunia ndio imemjua kuliko mlima kilimanjaro sasa.
 
Last edited by a moderator:
Nauliza swali wakuu...,KUNA MANTIKI GANI NMB Kujitangaza NJE ya Tanzania(taking context that,hiyo ni local bank,na hii mechi hasa kwenye TV itaoneshwa zaidi duniani).hao jamaa w TFF waliweka Criteria gani za Advertisers?au walikuwa wanaangalia fedha tu?

Kwa nini wasingeweka matangazo ya kuiuza Tanzania Nje ya NCHI?kwa nini TV adverts kama ESPN,aljazeera, etc zote ni local adverts?why?why?why?
am so mad at TFF,Serikali,na Vichwa maji woote walioshiriki kupanga hii mechi.
 
MTANGANYIKA unaichukuliaje mechi hii ? Hii timu ya Taifa ilikuja yenyewe kutokana na uhusiano wa nchi zetu au hapa kuna mtu amechangamkia tenda ?
 
Swali....Hivi mechi ya leo imetumika vipi kuutangaza utalii(tulioambiwa ndo lengo kuu la kuwaleta Samba Boys)????????????????????
 
Haya mpira kati ya Taifa Stars na Brazil umekwisha; Matatizo ya watanzania yako pale pale.


attachment.php

Brazil.JPG
 
Back
Top Bottom