Brazil to play Tanzania in a friendly

Brazil to play Tanzania in a friendly

Hahaaaaaaaaaaaaa.......Nimefurahi sana leo mie........Tumefungwa mkono(05) na pia mahudhurio yamekuwa hafifu mnoo,dua zngu na wengine zimesikilizwa.....TFF imekula kwao leo.......hahaaaaaaaaa

Hope hili ni fundisho tosha
 
Hawa Brazil wabovu kweli, kigenge kama cha Tanzania wanakipiga 5 tena kinapata moja...!!!!
 
Tusubiri sasa mahesabu ya mpato yatatolewa baada ya wiki mbili
 
USD 2.5 mil gone plus a bonus ya goli 5. Hii ndio watu wa pwani twaita kukandwa maji umekandwa na mtoto umemkosa..

Abdulhalim, si nchi imetangazwa katika nchi 160 duniani? Sasa tusubiri kuona idadi ya Watalii itakavyomiminika kutoka katika hizo nchi 160. Hii amount waliyolipwa Wabrazil inabadilika kila leo sijui kama tutajua kiasi cha kweli walicholipwa maana tumeshasikia $6 miilion, $3 million na sasa $2.5 million.
 
Hatuna kipa siye........Kipa bomu kama nini...........Hivi Chuji na Boban ndo washatemwa kimoja Stars
 
Hivi kwa nini wasingechora/project picha ya mlima kilimanjaro/jina la mlima kilimanjaro pale katikati ya pitch?!kila mtu angejiuliza kile ni kitu gani?goole search za kilimanjaro zingekuwa all time high=Better awareness.
 
dollar mil 2.5 ingetosha kulipia matangazo south africa ya kutangaza vivutio vyetu vya nchi lakini tumeamua kuwapa wa Brazil hili tusikike kwamba wamecheza na sisi.


huu ni umaskini wa kujitakia,umaskini wa akili.
 
Tusubiri sasa mahesabu ya mpato yatatolewa baada ya wiki mbili
Ikiwa nchi ya Zimbabwe inayoendeshwa kwa martial law imeshindwa kurejesha gharama, sie tulojaa wasanii tutaeza?
 
Brazil is a bit lazy today, au hali ya hewa

Wanacheza kwa tahadhari maana kama hela tumewapa na huenda kesho wakaelea mbuga za wanyama kidogo si unajua tena. Ila Kipa hatuna kabisa hapo vijana wamejitahidi. Nina uhakika tungebadilishana makipa na Brasil wetu aende kwao na wao aje kwetu ingekuwa 1-1 au 1-2 ila si haya. Maana sisi beki yetu ipo loose + Kipa ndiyo kabisa.
 
Nina hasira za dhati kwa walioandaa hii mechi bila kutangaza vivutio vyetu ipasavyo.Hakuna Kilimanjaro,zanzibar,manyara,ngorongoro,gombe,ruaha....,hyo mjinga aliyeweka tangazo la Serengeti as if liko indoor ana matatizo ya akili.
Ni wakati muafaka hawa wazee wakaondoka sasa na hayo matoto yao yasiyo na kitu kichwani wakayaache yaendelea kupumzika kwenye masofa nyumbani.This was a big opportunity lost.
Nimeangalia mchezo wote; mchezo ule umerushwa na TV nyingi sana duniani kutokana na umaarufu wake No1 playing aginst No 108. Ingawa uwanja ule ulikuwa unaonekana mzuri, lakini matangazo yote pale uwanjani yalikuwa hayaitangazi Tanzania kwa vyovyote vile
 
Hivi kwa nini wasingechora/project picha ya mlima kilimanjaro/jina la mlima kilimanjaro pale katikati ya pitch?!kila mtu angejiuliza kile ni kitu gani?goole search za kilimanjaro zingekuwa all time high=Better awareness.


Hata tangazo la safari larger would have done it kuliko hiyo Serengeti, na NMB.

Tanzanians are not strategic at all.
 
Kweli nchi yetu inahitaji kuongozwa na vijana.


Vijana tujitokeze jamani kuokoa nchi yetu hawa wazee akili zao zimelala sana.
 
pole mtanzania mimi, kufungwa ni mimi, wala sitaweza kuwa mbrazil,
najivunia changu kibovu, kufungwa ni mimi, wala sitaweza kuwa mbrazil,
hakuna mbili bila moja, wala kumi haiwi shilingi, kama moja haipo kamili,
 
kwani nyinyi mlitaka matokeo au mlitaka Brazil waje muwaone tu? wamekuja mmewaona mambo mengine yote ni irrelevant.

Hapo mimi simo, si nia yetu kuwaona tu, ni kuwaona na kujitangaza na sisi kwamba kandanda tunaliweza. Sasa tuwaone na kufungwa matano tulichofanya ni nini kama siyo kujiharibia sifa kimataifa? Utaona kwenye ranking za FIFA zitakazotoka sasa kama siyo tutakuwa wa 160 kutoka 118?
 
Back
Top Bottom