Katika gazeti la Raia Mwema la tarehe 31/7/2013 kuna makala ya aliyewahi kuwa balozi wa Tanzania huko Uingereza na marekani kuhusu gesi iliyovumbuliwa nchini. Anatoa mawazo mazuri ya jinsi ya kuepukana na utajiri huu kugeuka kuwa laana ya maliasili !! Anampango wa yeye na taasisi anayofanyia kazi kualika wataalam mbalimbali wa nchini na nje ya nchi ambao watashiriki katika mijadala hiyo ya kifungua kinywa ambayo wachangiaji na michango yao haitatoka nje ya ukumbi wa majadiriano ikiwa na maana coverage ya waandishi wa habari haitaruhusiwa!! Anonymity inayotaka kutumiwa ni sawa kidogo kama JF vile lakini tofauti na JF hawa wenzetu watakuwa ni wateule wachache wanaofahamiana ndio wataalikwa!!! Ingekuwa vyema zaidi na kwa manufaa ya nchi kama zaidi ya hao mtakaowaalika mijadala iwe wazi kwa yeyote atakayejisikia kuja kuhudhulia kwani kuna wananchi wengi wa kawaida msiowajua wenye michango mizuri tu kama ilivyojidhihilisha hapa kwenye janvi la jamii [JF]. Make the Breakfast Debate inclusive!!! Naomba kuwasilisha.