Kama ilivyo adha na taadhima kwenye mapenzi hakuna bingwa!unaweza ukawa bingwa leo lakini hauwezi kuwa bingwa milele!
Kabla haujafa hujaumbika!katika maisha usije ukasema kamwe sitafanya kitu fulani!
Bali sema Mwenyezi Mungu naomba nisaidie ama niepushe nisifanya jambo fulani maana binadamu ni kiumbe dhaifu ana mapungufu yake!
Mimi niliwahi kuapa kamwe sitawahi kuja kurudiana na Ex girlfriend yeyote yule kwa namna yeyote ile!
Na kweli nilikuwa bingwa kwa muda fulani ila baada ya miaka 15 ya ulimwengu wa mapenzi na wanawake tofauti tofauti sikuwahi kumrudia ex girlfriend!
Ila sasa iliwahi kunitokea nikamuacha demu mmoja bila sababu za msingi kwa kujua mimi nipo fiti tu mapenzi hayanababaishi aisee gafla nilianza kukonda kila nikimsahau hasahuliki (labda uchawi ulitumika,maana wanawake wachawi sana wa mapenzi)mara demu baada ya miezi miwili akaanza kumpost baby wake nikazidi kuumia futa picha zote tulizopiga,block moja matata lakini aah!wapi maumivu per day vile vile!
Niliteseka miezi mitatu nikaona cha kufia nini!
Nikaenda kumuomba turudiane kwa vile alikuwa na yeye bado ananipenda jamaa akachezea kibuti matata!
Kipindi hicho cha miezi mitatu nilikuwa na girlfriend mwingine ile nilikuwa sijusikii chochote hata nikilazimisha kumpenda nashindwa!
Je, na wewe ulishawahi kushindwa ku move on? Ilikuwaje?