Breakup ya kwanza ilikuaje?

Breakup ya kwanza ilikuaje?

Mi nliumia ile mara ya kwanza kupenda nlisota sio powa nlikuwa nalala usingizi flan ambao unakua umelala lakini Mtu akikuita unaitika, vinywaji vyote vilibadilika ladha mdomoni Mwangu, kila Kitu nliona kero hata Mkono wangu ukigusa shingo nliona kama nakereka usingizi hamna kbs
 
Huo tunaita ubatizo wa moto 🔥
Mwanaume sharti apitie hiyo mara moja, na mara moja tu! Baada ya ubatizo unakuwa senior kamili sasa tayari kuishi nao kwa akili.
Hakika mkuu, inakufanya uanze kuangalia wanawake na mahusiano kwa jicho la tatu. Ambalo ni ngumu sana kuwa nalo iwapo hujapitia hizi stage.
 
Hakika mkuu, inakufanya uanze kuangalia wanawake na mahusiano kwa jicho la tatu. Ambalo ni ngumu sana kuwa nalo iwapo hujapitia hizi stage.
Mimi baada ya kuachwa na mwanamke wa pili tena ambaye tumefanya mengi halafu akasema hakuna anachojivunia aiseee lile pigo sitalisahau. Mpaka sasa naweza kuja kuoa ila itakua ngumu sana kumtendea mwanamke kama nilivyojimaliza mwanzo.
 
Ghafla akaniambia via sms kuwa yuko lodge na ampendaye,nikadhani utani nikapiga simu akapokea afu akampa njemba ikaniambia "stop bothering my queen"afu na yeye akaniamba mazoea yafe,just ghafla tu na hatukuwa na tofaut,aisee nikaenda kumweleza rafik yangu,alisikitika sana maana nilikua mnyonge vibaya mno,ningezubaa ningekufa kwa mawazo na njaa,mazoez yakaanza kwa kasi,gym na mimi afu na hiphop hardcore nikamsahau yule manzi,tangu hapo sijawah kuwa na mwanamke mmoja japo nimeoa ila vya pembeni sikosi!
 
Dah mie nadhani bado maana nimewza hapa idadi ya pisi nlizopukutisha na kupiga chini pamoja na zile zilizonipiga chini sijawahi umia zaidi ya mmoja tu ambaye siku tunalimana maneno ya kumwagana akaropoka kuwa mm sijui show na alikuwa ananivumilia tu...dah asikwambie mtu nliumia mwezi mzima badae nkasema ntamtokea tena Ili akiingia kingi aisome namba ila ndio hivyo alishastuka.Kifupi yule manzi ananiuma hadi Leo na Sio Kwa lingine bali neno lake like.
Hapo ungemeambia nae awe anahjsafisha vizuri,ndo maana hukua na mzuka nae,,hako kambinu kumwambia awe anajisafisha vizurinilikatumia kakaleta matokeo ilimuuma,ila kiukwel hakua mchafu
 
Ngoja ni rudi nyuma kidogo....

Baada ya kukutana na huyu mrembo kuna kitu nilihisi ambacho ni ngumu kueleza kwa lugha tulizonazo, ila kuna kama JE-DAVU flan nilihisi ambayo haielezeki... nimekumbana na pisi kali sana na tuliachana ila kwa huyu, nahisi upendo haukutokana na muonekano wa nje nahisi. Ingawa alikua kisu pia, so kama kawaida yangu sikutilia maanani hizo hisia nikawa najivungisha kama si care sana.

Siku 3 tu za kumjua nikama vile tumejuana maisha🤣 kulikuwa na chemistry flan ambayo ilinifanya nilewe kabisa nikawa vulnerable asee sikuwahi kujihisi nimependa kiasi kile, kwenye shoo nilijihisi peponi, hata productivity yangu kazini ilipungua sometime nadoji siendi nasingizia ugonjwa, ili tu nispend time naye. Mpk hapo mtu alikua haniambii kitu maana huu upendo ulikua next level..

Kupunguza stori, kwa mara ya kwanza nilihisi uhalisia wa kukutana na mtu sahihi. Wengine ilikua nikishaona ya ndani attraction kwisha. Ila huyu nilimpenda beyond that, nilitaka kabisa awe wa kufa kuzikana. Alinifanya nisiwe na tamaa tena, kwa madem wengine. She was my perfect match.

Ila wakuu kuna kitu kinaitwa right person wrong timing.. kuna vitu viko nje ya uwezo wetu. Sitaki kuexpose nini kilitokea mpk kuachana ila kaeni mki jua mpk mungu aamue huwezi kuwa na mtu sahihi. Mtu sahihi huja baadae kabisa mpk uwe emotionally strong kucontrol desires.

Nahisi labda hakuona intensity ya upendo nilokua nao kwake? Sijui, labda alipitiliza kupenda mpka kuumia? Maana upendo halisi hufungua moyo na kuufanya uwe vulnerable? (It opens old wounds!) Sijui ila ni dhahiri tulipendana. Ilikua kama addiction hata tukizozana asubuhi, jioni sex kama kawa... so mimi nilihisi hii itakua sio sawa. Ile jeuri ya kila mmoja wetu ilikua inatutafuna na nilitaka kuondokana na huu upendo wenye utamu na uchungu ndani yake. So nika end things japo nilijua kabisa itanichukua mda kuja ku get over her. Ilinifunza vitu vingi kujihusu na jinsi nilivyochukulia mahusiano na wanawake pia.
haku kutafuta??
 
Mi nliumia ile mara ya kwanza kupenda nlisota sio powa nlikuwa nalala usingizi flan ambao unakua umelala lakini Mtu akikuita unaitika, vinywaji vyote vilibadilika ladha mdomoni Mwangu, kila Kitu nliona kero hata Mkono wangu ukigusa shingo nliona kama nakereka usingizi hamna kbs
Huo usingizi mkuu hata mimi nauelewa🤣🤣 unakua nikama haulali bali unapumzisha mwili tu.
 
Mimi baada ya kuachwa na mwanamke wa pili tena ambaye tumefanya mengi halafu akasema hakuna anachojivunia aiseee lile pigo sitalisahau. Mpaka sasa naweza kuja kuoa ila itakua ngumu sana kumtendea mwanamke kama nilivyojimaliza mwanzo.
Mapenzi hayana formula mkuu lazma kunakuumizwa na kuumiza!
 
Mi nliumia ile mara ya kwanza kupenda nlisota sio powa nlikuwa nalala usingizi flan ambao unakua umelala lakini Mtu akikuita unaitika, vinywaji vyote vilibadilika ladha mdomoni Mwangu, kila Kitu nliona kero hata Mkono wangu ukigusa shingo nliona kama nakereka usingizi hamna kbs
Em subiri kwanza…. Mkono ukikugusa unaona nini??!!! 🤣🤣🤣🤣🤣
Nyie kupenda gani huko mtakuwa machizi mjue!!
 
Back
Top Bottom