BRELA ( Business Registration and Licensing Agency) kuna matatizo makubwa! Waziri wa Viwanda na Biashara tunakuomba uingilie kati haraka!

BRELA ( Business Registration and Licensing Agency) kuna matatizo makubwa! Waziri wa Viwanda na Biashara tunakuomba uingilie kati haraka!

Fumadilu Kalimanzila

JF-Expert Member
Joined
Dec 10, 2016
Posts
1,770
Reaction score
5,423
Matumizi ya teknolojia yanapochukua nafasi kila mtu anategemea ufanisi kuongezeka!

Hii imekuwa kinyume kabisa kwa BRELA, inaumiza, kuleta hasira na hasara sana kwa Wafanyabiashara.

Mwaka jana mwezi wa nne 2020 nilianza mchakato wa kuhuisha taarifa za kampuni yangu ili kuomba leseni za biashara katika taasisi zingine ,mpaka leo bila mafanikio!

BRELA kila ukiwatumia nyaraka wanazotaka katika mfumo wao (ORS) ndani ya siku 3 wanakurudishia ufanye marekebisho mengine! Nimefanya marekebisho ndani ya miezi 10 mpaka nimechoka!

Nimepiga simu mara nyingi zinapokelewa na watu wa "customers' service" ambao pia inaonekana wako pale kwa malengo ya kupata mishahara tu mwisho wa mwezi!!

Nimewahi kuwauliza kama document mnai- assess kwanini msifanye hivyo kwa document nzima then mimi nifanye amendment once and for all! majibu yao ni ya kushangaza na hayana logic yoyote!

Wanaofanya document assessment inaonekana lugha ya kiingereza ( English) pia ni shida unless waniambie documents zinakuwa assessed na "System" au Robot !

Wanaandika sentensi fupi fupi na wala hawaandiki kukuelewesha mapungufu ya kurekebisha yalipo!
Mfano anakuambia," write the proper date " ! Unajiuliza ni date ipi na kwenye document ipi?! Maana unakuwa ume- upload documents nyingi na zenye tarehe nyingi na tofauti!!!

Nimehangaika BRELA toka mwezi wa NNE mwaka jana (2020) kwa kazi ambayo ilikuwa inanichukua siku 7 pale BRELA kukamilisha kipindi cha nyuma pamoja na URASIMU uliokuwepo!

Sasa haya maboresho ya BRELA maana yake nini?!
January hii wameniletea Invoice no.( control number) na nikajua nimekamilisha maana wamenifanyia assessment wao! Nimelipa zaidi ya milioni na nusu (Tshs.1.5 million ) .

Nikawapigia simu wakaniambia nia- upload pay in slip kwenye System (ORS) nikafanya hivyo!

Baada ya siku tatu 3 tena nimekuta wananiomba ni- upload tena document ambayo nilishawatumia!!!!!!!!!!!???????

Naona wameanza kuhuisha taarifa zangu upya tena !!!!!

Mwekezaji gani kutoka nje anaweza kuvumilia mambo ya ajabu ajabu kama haya!!!!!!

Wenzetu jirani wanasajili kampuni kwa muda wa masaa 24 lakini hapa kwetu mfanyabiashara yuko tayari kuhuisha taarifa zake na kuilipa Serikali fedha anazodaiwa lakini anaweza kuchukua mwaka mzima!!!!

Tusikimbilie kujiingiza kwenye mambo makubwa bila maandalizi ya kutosha!
Pia watu wengine waangaliwe sana kwenye hizi ajira za Serikali, wengi wanapenda na kulilia sana ajira lakini ni waganga njaa tu ambao hawana uwezo wa ku- deliver na si wabunifu katika kazi wanapopata hizi ajira!!!

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Godfrey Mwambe najua wewe ni mchapakazi na unajua maana ya Biashara na Uwekezaji kwani recently tu umetoka TIC tupia macho BRELA haraka hakuna kitu pale Nchi inapata hasara kubwa sana kwa uzembe !!!
 
Huyo uliemuomba sizan km atafuatilia weka apa picha za docs tukukosoe pia jitahid kuwa familar na watu wa pale BRELLA umalize shida zko usiishie online tu
 
ISHU YA BRELA KUKIMBIZA WAWEKEZAJI NI KUBWA KULIKO ILIVYOTARAJIWA.

Na Bashir Yakub, WAKILI
+255 714 047 241.

Naweka maoni ya watu chini hapa ili muone ukubwa wa tatizo. Na haya ni baadhi tu kati ya maelfu ya meseji za malalamiko nilizopokea.

Awali nilidhani tatizo ni katika kusajili kampuni/biashara pekee. Kumbe ni karibia katika kila jambo unalotaka kufanya kwenye system.

Iwe unapeleka Annual Return ni shida, Iwe unafanya mabadiliko yoyote ya ofisi, Director, Shareholder, CSecretry, nk. ni shida.

Itakuchukua wiki, mwezi, ht miezi kukamilisha. Kila ukisubmit dcmnts jibu ni lile lile la maudhi, Additional Information/Correction is required.....

Brela ni mwiba kwa Wawekezaji wa ndani na nje. Napaona inapofia nia njema ya Rais ya kukuza biashara na uwekezaji. Si pengine ni BRELA.

BRELA panahitaji mabadiliko ya haraka mno kuliko mtu yeyote anavyoweza kudhani.

Madhali hakuna mabadiliko, hatutaacha kupaza sauti.
Screenshot_20210124-125202_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20210124-125318_Samsung Internet.jpg
Screenshot_20210124-125707_Samsung Internet.jpg
 
Kwan hao Brela wanafanya kazi wenyewe, bila maagizo ya wakubwa .... sometime mnawasingizia tuu.....
 
Kwan hao Brela wanafanya kaz wenyewe , bila maagizo ya wakubwa ....sometyme mnawasingizia tuu.....
Siyo kila maagizo hufuatwa.
Mfanyakazi anaweza kuagizwa hivi na kisha yeye akafanya vile.
Hii ni kawaida kila sehemu na kila idara duniani kote.

Cha muhimu ni hao unaowaita Wakubwa basi wafuatilie Malalamiko na Utendaji wa watumishi wao, na kisha wafanye maboresho ili kuongeza Ufanisi katika Utendaji.

Maboresho ni mambo ya kawaida katika mfumo wowote ule wa Utendaji, Utawala na Uongozi.

Hata Machines, Software/Apps, Internet tu nazo huwa zinafanyiwa maboresho ili kwenda sawa na Uhitaji na Huduma.
 
Taarifa nadhani zimewafikia maana hii platform haina longolongo
 
Hivi yule waziri Bashungwa aliyemteua yule mtendaji mkuu wa Brela sijui alikuwa anategemea nini. Watumishi wa Brela wanachojua ni kupiga hela za hao wanaoitwa wawekezaji kutokana na huyo jamaa kuwa na kiburi kukosa ushirikiano na kuburuzwa na Afisa utumishi mmoja boguz kabisa.

Nilisajiri Kampuni yangu pale kwa shida mpaka nilipolazimika kumpa kitu kidogo jamaa mmoja afisa utumishi tulifahamiana naye Shinyanga nilipokuwa na Kampuni ya ujenzi. Ukisumbuliwa we tafuta tu huyo jamaa pale maana yeye ndio mwenye ushawishi pale kuliko Mtendaji Mkuu wa hicho kitaasisi.
 
BRELA wamegeuka kuwa kikwazo katika kukuza uchumi wa taifa hili
 
Halafu kina Kitila Mkumbo wanahangaika kuandika kwenye magazeti page nne kuhusu uwekezaji.

Ukija kwenye ground zero
Prof. Kitila Mkumbo ameandika sana kuhusu hizi mada. Now, kapewa wizara yenyewe kabisa, let's wait and see his performance. Sijui naye ni bingwa wa theories tu kama ilivyo kwa wasomi wetu au this time ataweza ku-convert theories into reality.
 
Halafu kina Kitila Mkumbo wanahangaika kuandika kwenye magazeti page nne kuhusu uwekezaji.

Ukija kwenye ground zero
Watanzania bwana huko kwingine koote hakuna tatizo, watu wanameza madesa balaa,

Lakini kwenye kufanya kazi na ubunifu hapo hakuna kitu aisee.

Unakuta mtu ana miaka kadhaa kwenye ajira lakini hajawahi shauri jambo lolote kuongeza ufanisi katika taasisi.
 
 
Kuna Mambo ukiwa uayasoma kwenye mtandao unaweza kusema ni uongo. Mpaka ukienda field ndio utajua hii nchi Magufuli ana kazi sana Tena sana.


Pale Brela nashauri watu wanyongwe kabisa. Hakuna sehemu inahujumu nchi Kama Brela makao makuu - Pale mnazi mmoja.


Najua mnasoma humu na Dawa yenu inachemka. Hakuna mabaya ya kudumu Endeleeni kutuzungusha na kula mirungula tu.
 
Back
Top Bottom