BRELA: Kalynda ilipewa leseni ya kuuza vifaa vya kielektroniki

BRELA: Kalynda ilipewa leseni ya kuuza vifaa vya kielektroniki

Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA} inapenda kutoa ufafanuzi kwa Umma kuhusu kampuni inayoitwa Kalynda E-Commerce Limited baada ya kuona na kupokea malalamiko kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kuhusu uhalali wa biashara inayofanywa na kampuni hii.

Kampuni ya Kalynda E-Commerce Limited ilisajiliwa tarehe 14 Juni, 2022 na kupewa cheti cha usajili Namba. 156483877. Kwa mujibu wa katiba ya kampuni (Memorandum and Articles of Association) shughuli kuu za kampuni ni pamoja na;

1. Uuzaji wa jumla wa vifaa vya kielectroniki na mawasiliano,
ii. Ufanyaji wa biashara ya kitekinolojia ya kimataifa mtandaoni.

Vilevile, Kalynda E-commerce Limited ilipata Leseni ya Biashara tarehe 21 Juni, 2022 yenye Namba 20000031405 ambayo itaisha muda wake wa matumizi tarehe 20 Juni, 2023. Leseni iliyotolewa ni ya kufanya biashara ya masoko na mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao pekee (Online Marketing and Sa/es).

Wakati wa uwasilishaji wa maombi ya usajili wa Kampuni na Leseni ya Biashara taarifa zilizowasilishwa zilionesha ofisi ya Kalynda E-commerce Limited zipo Kiwanja Na. 9, Mtaa wa Kaunda, Kata ya Msasani Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam.

Hata hivyo, kumekuwa na taarifa zisizo rasmi zinazoleta taharuki kwenye jamii kuwa Kalynda E-commerce Limited imekuwa ikifanya bias hara ya Upatu "Pyramid Business" ya kukusanya fedha kutoka kwa wananchi kwa ahadi ya kupata faida ndani ya muda fulani kinyume na bidhaa au huduma iliyoombewa na kupata leseni ya biashara.

Leseni ya Biashara ya Kalynda E-commerce Limited inamruhusu kufanya biashara ya masoko na mauzo ya bidhaa kwa njia ya mtandao pekee (Online Marketing and Sa/es). Ufanyaji wa biashara kinyume na leseni iliyotolewa ni kosa la jinai chini ya Kifungu cha 19 cha Sheria ya Leseni za Biashara, Sura Na. 208.

Wakala inapenda kutoa angalizo kwa umma kuwa kabla ya kuingia kwenye mahusiano ya kibiashara na kampuni yoyote ni vema kupata uthibitisho wa uhalali na uwepo wa kampuni hiyo pamoja na biashara husika kutoka BRELA na Mamlaka nyingine za Serikali. Taarifa zote za Makampuni na Leseni za Biashara Kundi "A" zinapatikana kupitia tovuti www.brela.go.tz au ofisi za BRELA.

Hivi karibu kumekuwa na matukio ya baadhi ya watu wasio waaminifu kughushi vyeti vya Makampuni, Majina ya Biashara na Leseni za Biashara kwa lengo ovu la kuwatapeli wananchi. Baadhi ya vyeti vilivyogushiwa ni pamoja na Kopa Fasta Company Limited, Champion Investments na Afric. Taarifa zimeshatolewa kwenye vyombo vya dola kwa ajili ya hatua za kijinai.

BRELA inapenda kuukumbusha Umma kutojihusisha na Taasisi zinazofanya baishara za upatu "Pyramid Business" kwani ni kinyume cha sheria za nchi.
 
Ndio washajitoa hivyo. Cha ajabu jamaa walikuwa na matangazo kila sehemu. Kuanzia mabango barabarani mpaka matangazo ya kwenye TV.

Ila kwa vile uchumi mgumu BRELA hawamiliki chombo chochote cha kuweza kupata habari hivyo kutoweza kusikia matangazo ya huduma tofauti na waliosajili. Halkadhalika watumishi wao wote ni vipofu kutoweza hata kuona mabango barabarani.

Hili li nchi lilivyo la ajabu ukute Bosi wa BRELA na mkewe wote wamepigwa pesa zao pia, wanaliwazana ujinga saa hizi.
 
Kwa hiyo tunasaidiwaje na serikali au tamko limetosha
 
Ajabu, eakati hao jamaa wa Kalyinda wakifanya matangazo yao, ina maana BRELA walikuwa hawayaoni kama yanaenda kinyume na leseni waliyopewa?

Hao BRELA sioni tofauti yao na polisi wanaofika eneo la tukio majambazi wakiwa wameshaondoka, au gari la zimamoto kwenda eneo la tukio bila maji ya kuzima moto, hizi taasisi za serikali zinafanana sana tabia.
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Hili li nchi lilivyo la ajabu ukute Bosi wa BRELA na mkewe wote wamepigwa pesa zao pia, wanaliwazana ujinga saa hizi.[emoji23]
Waliopigwa hata wakiwaona hao mabosi wa Kampuni hawawezi kuwachujulia hatua yoyote,maana Kampuni yao ilikuwa unauza vifaa vya umeme!
 
Lakini shughuli za kampuni kwenye memorandum yawezekana na zaidi ya hiyo waliyoiandika brela
 
Wanaodhani wamepoteza fedha zao wawapeleke hao wahusika na upotevu huo Mahakamani,Serikali haihusiki na biashara za upatu.
 
mhudumu: mtume kuna ushuhuda huku
mtume: nini kimetokea?

mhudumu: kalyinda wamepiga mzigo.🤣🤣🤣
 
Mamlaka husika iweke taratibu za kufuatilia baadhi yake E commerces companies maana nyingi zinaenda kinyume na taratibu

Tuna kampuni nyingi mfano:- kariakoo mall,Darshopping,E partners lakini ukisajili kama kampuni ni lazima ueleze physical address yako kama kampuni japo tunafahamu duka mtandao shughuli zake ni mitandaoni yaan kila kitu mnamaliza hapo ila ikisajiliwa na kuweka physical address ni muhimu sababu
1:-mamlaka zinahitaji kufahamu shughuli zinazoendeshwa ni halali(TRA,fire,BRELA n.k) ila wanachofanya kwa brela zikisajili ni bhas hayo mengine hawafuatilii hadi muda wa usajili utakapoisha.

Changamoto kwa hizi E commerces companies
1:-Hawataki kufahamika ofisi zilipo kwa kuhofia kodi(TRA) na nyingi zimejificha (kuna kampuni kama 3 hivi ilitokea hadi watu wa delivery wafuatiliwe nyuma nyuma ndipo ofisi zikafahamika yaan wamejificha kariakoo huko kwenye apartments ndipo wanapofanyia shughuli zao
2:- Duka mtandao haswa wanaouza bidhaa mtandaoni hawatakiwi kukaa na bidhaa sehemu ya kazi lakini ukifika ndani wamejaza Bidhaa kama duka la kawaida japo nyingine hawatoi hapo maana ulipaji kodi wao na duka la kawaida ni tofauti
3:- kuna kampuni kama 2 pia kwenye cheti cha brela wameandika jina tofauti yaan usajili ni tofauti na vile wanavyojiita wao na ni kinyume na Sheria na wanafahamu Hilo
4:- wengi wanahofia pia sababu ya kodi kama nilivyoeleza namba 1 na unakuta mtu Ana EFD machines ya kuzugia haijasajiliwa hata na VAT,wanatoa machines za kihuni pia utaratibu wa e commerce kwenye baadhi ya vitu kodi haipo/ni ndogo lakini wanafanya uhunu wabaki kwenye level ya kutokuwepo kwa kodi, Kodi yao inakuwepo kutokana na idadi ya mauzo namaanisha ikifika kiasi kadhaa kwa kutokana na mauzo kwa mwezi ndipo Unaanza kulipa/kuongezeka lakini njia ya EFD receipt wanaikwepa ili kujiondoa kwenye Hilo jambo

Mamlaka husika zinapaswa kuzidi kutoa elimu,kwa kuongea na wahusika zaidi wa hizi biashara japo wengine wanaenda vizuri kwa kujirekebisha ila kwenye baadhi ya mambo.
Na haya ndio yaliyotokea

kalynda,imesajiliwa lakini address sehemu nyingine na shughuli inafanya aina nyingine,hata wahusika hawafahamiki(wengine/nyuma ya pazia wanachekelea muda huu)
 
Same day, different shit.

Kutoka Deci, D9, Qnet & co bado watanzania hawajifunzi..

Acha waendelee kuliwa
Kwahyo wakati ina tangaza mtandaoni kupitia reseni hyo wao hawakuona mpk jamaa wana tembea baada ya kushba pesa za wa2?
 
mbna hawawatafuti wakat usajili huhusisha details muhimu kama kitambulsho cha taifa nk?
 
Back
Top Bottom