KWANZA kabisa nianze kwa salam.
Kuna hili wimbi la polisi wanachunguza
LBL na kukamata baadhi ya wahusika. Inaweza kuwa hatua nzuri na hapa naomba niwakumbushe
Kalyinda.
Mwaka 2022 ulikua mwaka wa neema sana kwa matapeli wa mifumo ya
Ponzi. Kabla ya kalynda walianza
SCATEC wakajipigia zao pesa wakasepa na kijiji September 2024.
September hio hio watu hawajapoa ikafunguliwa
KALYINDA na sales pitch yao ikawa ile ile sawa na
SCATEC tofauti ikawa majina na rangi ya website. Vibali vilipostiwa mtandaoni, kejeli zikawa nyingi, “
kama wewe unaogopa acha wenzako watajirike, hizi nyaraka za serikali tumetoa wapi kama sisi ni matapeli”.
Watu wakaweka hela. Hapa watu wakajiaminishana kwamba, sawa ni utapeli ila wa mwanzo wanapata hela kweli. Binafsi niliweza kuchomoa
100,000 nilioweka na nikaongeza
200,000 tena.
wote tunajua
KALYINDA ilizimika kama ndoto za kijana alietamani kuwa padri akishanusishwa bangi. Na tukaja kuambiwa vibali vilikua vya
biashara ya umeme.
Wakati watu wanapambania
KALYINDA IREJESHE PESA ZAO huko huko kwenye magrup zikaanza link za
BEST BEI 🤣.
Hawa wakawa wajanja zaidi. Wakawa wamefungua website watu wanaweza kuwekeza hela ila kuvuna ingeanza tarehe 20/10 (kama sikosei)
Watu tukatabiri hao hio siku wanasema kuvuna ndo siku yao kukimbia, tukaonekana masnitch.
Siku ya siku kweli yakatimia.
BEST BEI wakafunga website wakasema wamehakiwa na ndo safari.
HAYA YA LBL SIO MAGENI NA WATU HAWASIKII BADO WATATAKA KUJARIBU BAHATI YAO. KUPIGWA NI CONSTANT
Hata KALYINDA waliripotiwa hivo hivo na milard ayo 🤣.
Watu watalia na hautakua mwisho watakuja wengine tena na tutalia.