Pile F
Senior Member
- Aug 15, 2020
- 121
- 170
Habari gani Wakuu ninaamini mpo vyema kabisa. Naomba Moja kwa moja niende kwenye mada
Tanzania ni Taifa lenye bahati kubwa. Wazo la bandari ya Bagamoyo ni la kipekee na Mataifa Mengi yangeona yapo nyuma mno kama nchi ya Tanzania ingekuwa na hii bandari leo.
Mradi huu umeachwa na kuchelewa kwa sababu kuu ya hofu ya Utitiri wa Viongozi wapenda rushwa, wenye uadilifu mdogo na siasa za kusifiana, kuficha taaluma zao, maovu na kutii makubaliano legevu katika Taifa letu.
Bandari hii ingekuwepo katika Taifa letu tusingekuwa tunapambana na mambo Madogo na ya kionevu kama kuwaondoa Machinga Mtaani maana wangekuwa wameajiriwa au kujiajiri katika njia au maeneo mengine Mengi. Na inawezekana kuwa wasingekuwepo vilevile katikati ya miji ambako ndipo Wateja wao wengi na wakubwa walipo.
Kwa mfano;
Biashara zinazolazimika kufanyika Bandari ya LOBITO kule Angola kutoka katikati na kusini mwa Afrika-Congo DRC, Congo Brazzaville, CAR, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Malawi na kwingine zingemwacha Mtanzania akizalisha pesa za kigeni kupitia kuuza huduma na bidhaa kwa pesa nzuri na kupunguza makali ya Umaskini.
Kukua kwa sekta ya Utalii, Usafirishaji, Biashara za Supermarket na Hoteli kwa hadhi ya kimataifa. Pia kupitia uwepo wa Jamii ya kimataifa kutachangia sana kukua kwa Teknolojia na Uwekezaji katika Elimu, Viwanda, Kilimo na Masoko, Mawasiliano, Miundombinu na Mengi mazuri.
Wazawa watafanya Biashara za kisasa na Umaskini utapungua kwa kasi kupitia Ulimwengu unaotaka mazingira ya kufanyia biashara kwa gharama ya Dola nyingi na wakati mwingine kwa gharama ya pesa ya kiwango chochote.
Taifa litajitangaza bila nguvu kubwa kama ilivyo kwa UAE na mji wao maarufu wa Dubai pia Brazil zinazopata pesa nyingi kupitia Wageni wa kibiashara nchini.
Hili linawezekana kwa kuwa tuna mwambao mrefu wa bahari na wenye hazina kubwa ya Mali bahari pia visiwa salama kwa mazingira ya uzalishaji wa kisasa.
Tanzania itachapuka haraka na kuanza kuimarisha zaidi ulinzi pekee pamoja na Matumizi Bora ya Mazingira huku raia wake wote wakipata nafuu kubwa ya maisha kupitia kukua kwa Miji, AJIRA nyingi na Uchumi Imara wa Nchi.
NIONAVYO MIMI;
Ni fikra duni kuona kuwa TUTAIBIWA kama bandari ITAJENGWA.
Ni vipi uonavyo wewe kuhusu hii Bandari katika Pwani ya Tanzania kule Bagamoyo?