Brighton & Hove Albion F.C. (The Seagulls) | Special Thread

Brighton & Hove Albion F.C. (The Seagulls) | Special Thread

Tukutane hapa mashabiki wa The Seagulls! [emoji838][emoji836]
Baada ya kuchoshwa na upuuzi wa Manchester United, naona umeamua kutafuta furah.

Ongera kwako mkuu, michezo sio uadui, kama tuliweza kuacha ziwa la mama zetu itakua timu?

Watu wanahama Nchi, Dini itakua timu? kiufupi haujafanya makosa.
Hongera kwako.
 
Tupo na Everton kwao pale. Mwaka jana tulimtwanga 4-1 palepale. Hii jumamosi 2 tu zinamtosha.
 
Mkuu, haya ni mapito tuu. Manchester ya asali na maziwa inarudi soon tuu hapo
Hilo ndilo ninalo amini mimi.
Binafsi nimeamua kutoangalia game yeyote ya Manchester United, sinto nunu jersey, sinto fuatilia usajili wala jambo lolote linalo ihusu timu, mpaka pale timu itakapo kua vizuri, na sio malayakwanza kufanya hivyo, lakini sihami timu ng'o.

Nimezaliwa kuishabikia Manchester United, hivyo nitakufa nikiwa shabiki lia lia wa hiyo timu, ila kwasasa najiweka pembeni kwanza.

Kichaka nilicho kichagua ni kurudi ligi ya nyumbani, na kuishabikia timu ya marehem babu yangu, na kweli hawanihangushi.
 
Mara moja!? [emoji16]

Nilikuwa United tokea enzi za Fergie ila kinachoendelea hakieleweki.

Kuhamia Brighton sitegemei watashinda EPL kabla ya United ila ni rahisi kufurahia mchezo wa football ukishabikia lesser clubs maana kuna low expectations kutoka kwa mashabiki.
Jana tumegongwa tena na Newcastle, tena pale pale kwenye vitofali vya kuchoma.

Wametupasua goli 3 bila, yani ni haibu mpaka basi.

Bora umuangalie Azizi K, kuliko kumuangali Fernandez.
 
muanzilishi wa hii thread ndio wale malaya malaya aliowazungumzia mwalimu Nyerere
Mjuu leo umetoa boko kwa kauli hii.
Kumbuka kupanga ni kuchagua, hivyo kwakua kaamua kuhama timu ilikua haina haja ya kumdhihaki.

Tumngoje siku akija tena kule kwetu na kijifanya kushabikia timu yetu, hapo tutamuona hamnazo.
 
Mimi Kama fan wa Di Zerbi nitakuwepo na humu kunsapoti Di Zerbi

Moja ya makocha ambao Pep ameuomba uongozi amrithi akiondoka


Kwa wasiojua ,Pep ameiga baadhi ya vitu kwa Di Zerbi

Di Zerbi ana lack kitu kimoja tu ili Brighton iwe tishio Sana

Ana lack kitu tunaita Rest defence

Ndio maana wanaoifunga Brighton Ni wale wanaokubali kuwa underdog ,ukisema Brighton Ni timu ndogo tu utakula hata mkono na mpira mwingi utapigiwa


Brighton vs man City Etihad , Pep alikuja na mpango wa man to man ,

Siri ya Di Zerbi huwa anaacha mtu mmoja kama spare man,


Ukicheza na Brighton Kama unajijua huwez kupress acha kabisa ,ukifanya press isiyo sahihi wanakuadhibu

Huyo ndiye Roberto Di Zerbi ,mpe wale wachezaji wa man u anagombea ubingwa EPL


Dunk , Gross wanakwambia Di Zerbi kawaonesha njia nyingine ya football

Kaangalie Mahojihano ya Kevin Prince Boateng anasema akiwa na miaka 32 , pale Sassuolo,Di Zerbi alimfanya awe Bora ,anamtaja Kama kocha Bora , alimfanya mtu Kama kina locatteli watu waone ubora wao .

Anakwambia anawafundisha mpira kwa kuzingatia vitu vidogovidogo Sana ,kiasi kwamba mchezaji ukiwa uwanjani unakuwa na option had 4 zakupiga pass

Ndio maana hutakiwi kuwa press Brighton Kama unajijua huwez kupress kwa usahihi

Bajet yake pale Brighton Ni €30m tu


Kaondoka Trosaard, Caicedo ,MacAllister timu bado inacheza vile vile
 
Jana tumegongwa tena na Newcastle, tena pale pale kwenye vitofali vya kuchoma.

Wametupasua goli 3 bila, yani ni haibu mpaka basi.

Bora umuangalie Azizi K, kuliko kumuangali Fernandez.
Unasema haufatilii habari za nyumbu, hakabu matokeo yake unakua wakwanza kuyapata [emoji1][emoji1][emoji1]

Sema siingia Kule jukwaa la nyumbu Kule unyumbuni Hadi team ikae vizuri
 
Unasema haufatilii habari za nyumbu, hakabu matokeo yake unakua wakwanza kuyapata [emoji1][emoji1][emoji1]

Sema siingia Kule jukwaa la nyumbu Kule unyumbuni Hadi team ikae vizuri
Mkuu huwa nayapata kupitia live score, hawa jamaa sijui vipi, siku ikicheza Manchester United lazima wanipe up date utadhani nimewaomba.

Ila kiukweli tangu msimu uanze sidhani kama nimetazama walau game mbili za United.
 
CHEZAJI LA £100M. KAORU MITOMA!
20231103_155558.jpg
 
Huu Uzi mkali kuliko nyuzi za man city na Tottenham Hotspur
 
Back
Top Bottom