British Council mbioni kufunga Ofisi zake Tanzania kama sehemu ya mpango wake wa kubana matumizi

British Council mbioni kufunga Ofisi zake Tanzania kama sehemu ya mpango wake wa kubana matumizi

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079
Taasisi ya kimataifa British council inapanga kufunga ofisi zake katika nchi tisa, zikiwemo Tanzania na Msumbiji, kama sehemu ya mpango wake wa kupunguza matumizi. Hatua hii inakuja huku kukiwa na tahadhari kwamba kupungua kwa uwepo wake nje ya nchi kunaweza kuathiri uwezo wa Uingereza kujenga uaminifu na kushirikiana na wadau wa ndani.

Msemaji wa British Council ambayo katika mwaka wa fedha wa 2024/25 ilipokea ruzuku ya pauni milioni 126.5 kwa ajili ya kuendesha miradi ya maendeleo ya Uingereza ng'ambo, aliiambia kampuni ya habari ya Devex kuwa wanapendekeza kusitisha uwepo wao wa ana kwa ana katika nchi tisa, ambapo wamekuwa tayari kuzitaja nchi saba kati ya hizo.

Nchi hizo ni pamoja na Tanzania na Msumbiji, hadi nchi zenye uchumi wa kati zikiwemo Botswana, Peru, Chile, pamoja na Trinidad na Tobago. Taasisi hiyo iliongeza kuwa, nchi sita kati ya hizo saba hivi sasa zinapokea ufadhili wa misaada ya kimaendeleo (ODA), huku Croatia ambayo ni nchi ya saba iliyotajwa ikipokea ufadhili usio wa kimaendeleo (non-ODA).

Nchi hizi pia zilitajwa kwenye barua ya hivi karibuni kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Maendeleo ya Uingereza (FCDO), ambayo ndiyo inayofadhili British Council, kwenda kwa wabunge. Barua hiyo ilieleza kuwa majina ya nchi mbili zilizobaki yamehifadhiwa kwa sasa kwa sababu ya siri za kibiashara.

1783690187631.png

=============

The British Council will close its country offices in nine countries, including Mozambique and Tanzania, as part of its financial turnaround plan, amid warnings that a smaller overseas footprint could damage the United Kingdom’s ability to build trust and work with local partners.

A spokesperson for the British Council — which in fiscal year 2024/25 received £126.5 million in grant funding for delivering U.K. development-related work overseas — told Devex it is proposing to end its on-the-ground presence in nine countries, seven of which it was willing to name. These range from major development partner contexts such as Mozambique and Tanzania to middle-income countries including Botswana, Peru, Chile, and Trinidad and Tobago. Six of the seven currently receive official development assistance funding, with Croatia — the seventh named country — receiving non-ODA funding, the institution said.

The countries were also identified in recent correspondence from the Foreign, Commonwealth & Development Office — which sponsors the British Council — to members of Parliament, which said the names of two further countries were being withheld due to “commercial sensitivities.” The letter says the choices were made “primarily on the basis of where the greatest savings can be realised relative to the impact of current operations,” rather than because of the importance of outreach in those countries.


Source: devex
 
Kingereza cha nini sasa wakuu,

Wakati sisi agenda yetu ni kusambaza kiswahili duniani.

To hell with them.
 
Ila hawafungi Kenya, Uganda..

Tanzania itakuwa imeponzwa na Samuya kupitia mauaji ya halaiki ya MO29.

Tlaatlaah
Gentleman,
mie sio changamoto hapo,
nadhani hiyo ni hiyari yao kuifunga kama ilivyokua hiyari yao kuifungua Tanzania.

Na wakiona inafaa zaidi,
hata ubalozi wao humu nchini ikiwapendeza waufunge pia, kwasababu ni hiyari yao na haihusiani kabisa na masuala ya ndani ya Tanzania hata kidogo.🐒
 
Wafunge tu kwanza naona wamechelewa sana
pia nashauri wafunge na balozi zote za huku na kule kwao!
#HAKI.
 
Kingereza cha nini sasa wakuu,

Wakati sisi agenda yetu ni kusambaza kiswahili duniani.

To hell with them.
Hiyo labda ajenda yako wewe. Ila inajulikana mmeanza kukishobokea ki_Arabu.
 
Pesa zenyewe hawana kwasasa!!! Mwisho kusikia msaada kutoka Uk. lini🤠
 
Back
Top Bottom