Traxtion
JF-Expert Member
- Dec 10, 2021
- 8,000
- 16,414
Uchunguzi wa kifo (inquest) ulisikiliza kwamba kiasi cha 40ml cha hyaluronic acid pamoja na lidocaine kilidungwa katika kliniki moja nchini Thailand. Baadaye, Igho alilalamika kuwa na maumivu ya kifua na akaanguka. Alikimbizwa hospitalini, ambapo madaktari waligundua kuwa alikuwa na pulmonary embolism, yaani mshipa wa damu katika mapafu ulizibwa na mgando wa damu.
Licha ya kufanyiwa CPR kwa zaidi ya dakika 100, alifariki dunia. Uchunguzi wa mwili baada ya kifo ulibaini uwepo wa kitu kilichofanana na kile kichujio (filler) katika mapafu yake, na coroner akahitimisha kwamba utaratibu huo wa urembo ndio uliosababisha embolism iliyomuua.
Igho, ambaye alikuwa akijulikana kwa maisha yake ya kifahari, alikuwa na takribani wafuasi 185,000 kwenye Instagram. Alikuwa amemuoa fashion stylist Danielle Simba Allen.
Licha ya kuwa kifo chake kilitokea March mwaka huu lakini habari zake zimeanza kusambaa mitandaoni siku ya jana, jambo ambalo limeonesha jamii jinsi ambavyo insecurities kwenye size ya uume wako inavyoweza kukusababishia kifo.
Wapo wanaume wengi ambao wako insecure na size ya maumbile yao kwa hiyo wanaenda kufanya procedures kurekebisha size zao, na sometimes wanapitia dangerous procedures kama hii na huweza kuleta madhara zaidi