Bro, kwahiyo mkeo umemruhusu kujipost mtandaoni na ana zaidi ya picha 30? Sawa Bro


Kwamba mwanamke akiolewa basi anakosa haki za kujipost huko mitandaoni?

Hoja yako ambayo ingekuwa na mantiki labda anapost akiwaje, amevaaje, anafanyaje. .
Lakini kama anapost amevaa kwa heshima, anafanya vitu visivyovunja utu na maadili ya jamii, amekaa pozi la heshima au maadili ya kike. Hakuna shida yoyote.

Kumuoa mwanamke humnyang'anyi haki na Uhuru wake. Bali mna-share Uhuru wenu katika maadili na kulinda utu wenu.

Aki-cheat fukuza. Hilo alijue tangu Siku ya mwanzo.
Ila kumzuia na kumlinda asi-cheat huo ni ujinga na Woga wa kuachwa au kutafuta mwanamke mwingine.

Mwanamke anahaki ya kutumia Mwili wake atakavyo. Ila ukiona hukubaliani naye katika matumizi yake muache tafuta mwingine. Simple.

Huo muda wa kumpangia pangia mwanamke life style ni Bora utafute mwanamke mwingine mwenye life style unayoitaka.

Ndivyo Watibeli tunavyoishi. Hatutakagi vikao
 
Nishakuambia kuwa uhuru una mipaka yake Bado unakaza fuvu. Picha 30 za nini mke wa mtu? Uhuru gani unaouzungumzia hapa wakushare akisuka vzr anapost akitoka out picha je hizo picha zinamchango gani ama faida gani kwenye ndoa yako?
 
😀😀😀namba ya fulan ulikuwa kichwani...Mtibeli😀😀
Akawa anajipost sana...ila matokeo aliyemkusudia haone hizo status.

Akaja kuuliza hivi wewe upogo whatsapp kweli..Nikajibu ndio😀😀
 
Umeusoma uzi lakini?

Soma paragraph ya 2 na 6

''Mkeo kila kukicha anajipost mtandaoni kabinua matako yake nawewe pasina kuwa na haya una comment umedamsh''



''Ni hivi hizo nguo za kuonyesha maungo yake wala si ukisasa huo bali ni ulimbukeni na pia anajichoresha kujiletea vishawishi''
 
Mkuu nimeshuhudia miaka 3-4 hii wanaume wenzetu wanapeleka wake zao photoshop wakiwa mimba ajabu wanapiga picha wakiwa matumbo wazi na kwenye picha hizo ndume ipo imeshika lile tumbo na ile picha inapostiwa mtandaoni. Swali dogo tu hii picha ya mimba ya mkeo inafaida gani kwetu sisi?
 
Nishakuambia kuwa uhuru una mipaka yake Bado unakaza fuvu. Picha 30 za nini mke wa mtu? Uhuru gani unaouzungumzia hapa wakushare akisuka vzr anapost akitoka out picha je hizo picha zinamchango gani ama faida gani kwenye ndoa yako?

Mkuu Dunia haiko hivyo. Lengo la maisha mi kuishi. Na kuishi ni kufanya Jambo linalooupendeza na kukufurahisha.

Mwanamke kupost na kushare picha zake kama ni furaha yake hakuna tatizo lolote.
Anafurahia vile anavyoonekana na vile watu wanavyomuona.

Furaha yake ndio mchango wake ndani ya ndoa(familia yenu)

Tatizo kubwa walilonalo wanaume wengi hasa wasiojiamini, waoga wa kuachwa, kuishi wenyewe au kutafuta chimbo jingine ndio huwa na Sheria zisizo na kichwa wala miguu. Huwaza mambo ya ngonongono. Kwamba Mke ataliwa, mke anajitangaza.

Mkuu mkeo hata awe na kiswaswadu kama ni Malaya, kama hakupendi watu watajipihia tuu.

Yaani mkeo asipost picha zake mitandaoni na anapenda kufanya hivyo kisa ujinga na mawivu yako?😆😆 Kuwa serious.

Kadiri unavyoonyesha Wivu kwa mkeo ndivyo thamani yako kwake inashuka. Na anatafuta mwanaume Bora zaidi. Anaona hujiamini.

Anakuona huna Options (uwezo wa kupata mwanamke mwingine kama yeye)

Mpe Sheria moja. Uaminifu ni juu yake. Aki-cheat utamfukuza bila kikao.

Kisha mengine muachie

Sasa mtu asijipost kisa?

Mbona huwazuii wanaume?
Mbona hausemi mumeo kama anajipost picha zaidi ya 30 ni hatari?

Acha mawazo ya kizamani Mkuu.
Hiyo sio njia salama ya kuishi kwa furaha na Mkeo unayempenda.
 
Mada inazungumzia wanawake wanaobinua makalio na kuvaa nguo zinazoonyesha maungo sio kina mama wenye heshima ila wanapost maisha yao mitandaoni.
 

Nimeusoma.

Mke Kubinua makalio au kuvaa nguo zisizoeleweka hilo Kila mtu anajua ni tabia mbaya. Hata wanaopost.

Hiyo hoja imechomekewa tuu lakini lengo la mtoa mada ni kuzuia wanawake wasiwe wanapost picha mtandaoni bila kujali ni picha ya aina gani. Ndio maana title ya mada inajieleza zaidi.

Kwamba wanawake wasijipost hata kwa heshima kisa kuna wanaume wajinga wenye wivu? Hapana kwa kweli. Lengo la ndoa na familia sio kuchukuana mateka na kufanya watu watumwa
 
AYA yapili unasema huna mchango wowote kwenye familia hiki ulichoandika ni mchango pia
Ni mchango wa kijamii huo sisi wanajamii tunakereka hasa yanapowakuta inatumbidi kwa namna moja au nyingine twende tukatoe msaada kwa ujinga alio ulea muda mrefu.

Mfano jana nimetoka mnadani nataka kuoga tunasikia makelele laiti wasigewahi wanazengo wangekuta jamaa kakata mtu panga.

Ukiwaonya humu mtandaoni wanatuona sisi ni wakoloni kwa wake zetu na wengine wanatuambia tuache ushamba au tutafute hela.
 
Mada inazungumzia wanawake wanaobinua makalio na kuvaa nguo zinazoonyesha maungo sio kina mama wenye heshima ila wanapost maisha yao mitandaoni.

Mkuu hiyo hoja imechomekewa watu. Lengo la mada ni Wanawake wasipost picha zao mitandaoni.

Mtoa mada ni wale watu wenye mtazamo wa Watu kutokujipost mara kwa Mara. Na sababu zake zinatokana na mtazamo hasi alionao.
 
Huu uzi sio sheria bali ni maoni au mtazamo,
Hakuna aliyelazimishwa aishi atakavyo mleta mada,
Sio kila mtu atakubaliana na mleta mada but wapo watakaofaidika na ujumbe uliomo ndani ya mada,

Huu ni ushauri tu au mtazamo tu,
The rest it's up to you.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…