Bro to bro: Hili suala la kuombaomba michango ya harusi ni kujidhalilisha sana

Bro to bro: Hili suala la kuombaomba michango ya harusi ni kujidhalilisha sana

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,548
Reaction score
28,817
Hivi inakuwaje mwanaume mzima unafikia hatua ya kupiga simu na kutuma meseji za kuombaomba michango ya sherehe ya harusi yako?

Unajikuta ghafula umeungwa kwenye group la harusi, humo bwana harusi mtarajiwa anajidhalilisha kwa kuombaomba michango mpaka unaona aibu wewe.

Hivi ni lazima uchangishe watu kwa ajili ya tukio la kukaoa hako kamwanamke kako?

By the way harusi ni utoto sana na ujinga na fake event, unapanda range na kamalaya kako kesho tunawaona kwenye IST au daladala umeshikilia bomba.

Hakuna mtu aliyewahi kupokea tuzo ya harusi bora. Usijimalize kwa madeni na kujidhalilisha kuombaomba.

Fanya sherehe yako ndogo, vaa pendeza na mkeo, alika watu wachache utakaowamudu ifanye sherehe yako ipendeze tunza kumbukumbu kwa picha na video.

Anzisha ndoa yako in peace not pressure. Usitake kuwaimpress watu for one day halafu ukabaki na years of stress za madeni.

Marriage is for life. The wedding is for a day.
​
 
Kawaida tu , kama jamii tunasaidiana tu , mimi nakuchagia vizuri tu ila nisikose bia zangu nikija harusini🤔
Hapana kaka kuna mambo ya msingi ya kusaidiana ambayo jamii hawasaidiani mfano matibabu na elimu

Ila likihusu huu ujinga wa harusi na sherehe za kipumbavu unakuta watu wanachangiana

Yote ni sababu wanajua watakuja kuila pesa yao

Dunia ina unafiki sana
 
Ujamaa umewaharibu sana,mtu anakua na mindset ya kuona kua kuchangiwa ni haki yake,

Kingine kuogopa kua,watu watanionaje nikifanya harusi ya kawaida tu? Maisha ni yako,huna haja ya kuwaimpress watu,

Live the life u love
Love the life u live.
 
Hii huleta tabia ya utegemezi,mtu anakua hajiandai wala hajiwekei akiba,akitegemea atachangiwa,

Siku zote tegemea ulichokishika mkononi na usitegemee utakacho tafuta au utakacho omba.
Bwashee , kwenye utamaduni wa jamii yangu huwa tuna share mambo mengi ya kijamii kwa pamoja , mfano hata pombe , mazishi , harusi , maendeleo ya kiuchumi na nk , ndio maana naona kawaida tu
 
Kawaida tu , uzuri kuchangia ni hiyari yako tu bwashee
Ni hiari sawa ila utakuta mwana anakuganda utafikiri bila hiyo 70k ya single au 100k ya double hawezi kufanya harusi

Yote ni kutaka makuu tu, wakati unapanga harusi ulikuwa haujui gharama zinahusika

Yaani wewe utuombe pesa zetu na bado utupangie kiasi na tarehe ya mwisho ya kutuma michango umerogwa nini
 
Ni hiari sawa ila utakuta mwana anakuganda utafikiri bila hiyo 70k ya single au 100k ya double hawezi kufanya harusi

Yote ni kutaka makuu tu, wakati unapanga harusi ulikuwa haujui gharama zinahusika

Yaani wewe utuombe pess zetu na bado utupangie kiasi na tarehe ya mwisho ya kutuma michango umerogwa nini
Una mchana tu kama haupendi bwashee, ila binafsi kwangu ukinipa kadi ya harusi tayari unanidai na kama mwana jamii napaswa nilipe sisi ni wamatumbi tu bwashee na sio wachina kiukweli 🤗
 
Hii huleta tabia ya utegemezi,mtu anakua hajiandai wala hajiwekei akiba,akitegemea atachangiwa,
Huu ndio ujinga wa mabwana harusi watarajiwa wote

Kuna bwana harusi mmoja kwenye kikao cha harusi anawaambia wanakamati

Anataka yeye na kamwanamke chake gari lao la maharusi kama sio Range basi Hummer hata kiwanja hana
 
Back
Top Bottom