Bro to bro: Hili suala la kuombaomba michango ya harusi ni kujidhalilisha sana

Kawaida tu , kama jamii tunasaidiana tu , mimi nakuchagia vizuri tu ila nisikose bia zangu nikija harusini🤔
Na hii tabia ya kufuatilia kula ulichochangia, inakuwa ni 'uwekezaji' sasa na siyo 'mchango'.

Kumchangia mtu ili asaidike ni kule mtu kujitoa bila kupata return papo kwa papo, ni kama utoavyo sadaka.

Tungelikuwa na tabia ya kuchangiana bila kushadadia kula na kuteketeza mamillioni kwenye sherehe, maharusi wangelikuwa wanapata mtaji angalau kuanzishia maisha yao.
 
Umesema vyema
 
Harusi yangu watu 70 tu tulialika lakini walikuja 150+ tuliwamudu wote walikesha pale hawasahau.
Walikula,wakanywa ,wakadance hadi asubuhi.
Hamna aliyechanga senti 10.
Saafi sana, hongera na hii ndio maana ya kuwaita "wageni waalikwa"

Hizi mambo za kuchangisha michango wageni waalikwa hakuna tofauti na ule msemo "mgeni njoo mwenyeji apone"
 
Kuita mwanamke yeyote anayekuwa anaolewa kamalaya unasahau hata aliyekuzaa ni mwanamke? Unasàhau una dada, mama, shangazi? Wote watakuwa kwenye kundi hilo hilo.....kusumbua watu kwa michango ndo ilikuwa point hapo, mi mwenyewe nawashangaa sana watu mtu anataka kuoa au kuolewa analazimisha michango wee utafikiri anakuolea wewe, kwanini mtu asifanye sherehe ya harusi kulingana na budget yake na watu wake wa karibu?
 
Uliwahi kuwekewa bunduki ili umchangie mtu hizo sherehe?
 
Ukiona mtu analalamika hivi, ni dhahiri kwamba aliyemuomba mchango si mshkaji wake na ameombwa mchango, hana, hataki na hajui anakataa vipi. Sasa ndio anaamua kuja kupayuka huku. GenZ mambo ya kijamii ninyi mnafanya personal, mwishowe mseme MSIBA KILW MTU ANAFIWA, WE JIFUNGIE NA FAMILIA YAKO, LIENI, KAZIKENI WENYEWE NA MAISHA YATAENDELEA
 
Usiniambie na wewe upo kwenye kundi la wapuuzi waombaji wa michango ya harusi. Harusi sio dharura JIPANGE
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…