Elison Ndalichako
JF-Expert Member
- Oct 31, 2017
- 275
- 449
Vyovyote utakavyoniita, ila binafsi nasijisikia fahari kubwa sehemu ya mafanikio ya mtu. Huwa naenda mbali zaidi na kumwambia mhusika kama kuna kamati aniweke.Usiniambie na wewe upo kwenye kundi la wapuuzi waombaji wa michango ya harusi. Harusi sio dharura JIPANGE
Umesema vyemaSiwezi kuchangia harusi hata iwe ya ndg yangu akinialika ntaenda kumpongeza na kumpa hongera tu
Unavyoona kuomba omba michango ni sahihi?lakini kila mtu anafanya anachoona ni sahih kwake wengine wasipochagisha wengine hawajisikii raha
kwangu mimi sio sahihi kuomba omba ni kujidharau mwenyeweUnavyoona kuomba omba michango ni sahihi?
Waachie wazazi wafanye wanachotaka. Mimi nimechangia watu na nitawachangisha niliowachangia.Kuna hiki kitu haujagundua.
Na naongea kwa uzoefu binafsi na marafik rika zangu wa karibu.
Asilimia kubwa ya vijana hatutak kufanya sherehe ya Harusi. Ila huwez kukaa na Mtoto wa mtu ndan had ufanye baadh ya process.
Kwahiyo unavyoanza kutoa taarifa kwa wazaz. Wao sasa wanashika hatam ya kukuongoza uanzie wap na wap. Unakubaliana na mambo yote (kupeleka barua, kupeleka posa/mahar kujitambulisha au kuvalisha pete. , ) ila likija sasa kwenye sendoff na sherehe ya harusi vijana tunapinga kidogo kwa kusema mm sina marafik weng na harus ni gharama.
mzaz/mlezi anakuambia ni Lazima. Mm nimechanga za watu weng na kuhudhuria sherehe zao. Alaf ww uoe bila harus. Haiwezekan.
nitaita Ndugu zako vikao tutashikana mashati na utaoa kwa sherehe.
Na upande wa kike pia unaweza kuamua kama upande wa kiume.
Na hizi zote vijana weng Hatupend. Ila sasa wazaz washaamua.
Kwahiyo na ww inabidi ukomae kutafuta hela kwa marafik kufikia budget ya harusi. (Ndio huo Usumbufu unaouona) wengne anaweza hata asikutafute miaka 5 alaf gafla anapiga sim kukualika kwa kukao na siku ikifika hata usipoenda watapiga sim ya kuomba pledge yako.
Kama ni Mshkaj wako, uwezo unao, au unajua kuna siku utaomba msaada kwake pia kwa namna yoyote. mpe tu Sapport 😂😂😂😂
Hivi, UNA NDUGU??Ukishaingia kwenye mtego wa michango ya harusi huchomoki. Hili ni kundi ambalo kuchomoka ni ngumu kweli kweli. Kanuni : 1. Katu usichangishe fedha kwa ajili ya harusi yako au yeyote unayemjua. 2. Usihudhurie vikao vya harusi vya yeyote 3. Ukiombwa mchango jibu kwa ujasiri kuwa wewe hujishughulishi na mambo ya harusi kabisa ila unaweza kuchangia maharusi eg sufuria ya kuanzia maisha.
Nina ndugu ndiyo. Ni hivi: Mmi sikufunga harusi ya sherehe wala sikukusanya michango na mtu yeyote akija kwangu eti ni mchango wa harusi huwa sitoi. Tena nasema kabisa kuwa sitoi kwa sbabu sina, ila kwa sababu sitoi michango ya harusi. Kama ni ugonjwa, elimu, michango ya kufanya mambo ya maendeleo, kusaidia etc natoa sana kama nina uwezo, lakini harusi ng'o! Njoo niambie nataka kuanza maisha na mke wangu na sina kodi ya nyumba, kama ninazo nitatoa lakini siyo sherehe ya harusi.Hivi, UNA NDUGU??
Mbona hamuongei uhalisia wa kifamilia wa watanzania? Au wenzetu familia zenu ziko out of touch mnaishi wenyewe wenyewe?
Umesema vyemaNina ndugu ndiyo. Ni hivi: Mmi sikufunga harusi ya sherehe wala sikukusanya michango na mtu yeyote akija kwangu eti ni mchango wa harusi huwa sitoi. Tena nasema kabisa kuwa sitoi kwa sbabu sina, ila kwa sababu sitoi michango ya harusi. Kama ni ugonjwa, elimu, michango ya kufanya mambo ya maendeleo, kusaidia etc natoa sana kama nina uwezo, lakini harusi ng'o! Njoo niambie nataka kuanza maisha na mke wangu na sina kodi ya nyumba, kama ninazo nitatoa lakini siyo sherehe ya harusi.
Sahihi, kwa kuwa harusi sio dharuramtu yeyote akija kwangu eti ni mchango wa harusi huwa sitoi
Nakubaliana na wewe . Wakati naenda kuoa tena mtoto wa kishua, wazazi wake waliniulizaHivi inakuwaje mwanaume mzima unafikia hatua ya kupiga simu na kutuma meseji za kuombaomba michango ya sherehe ya harusi yako?
Unajikuta ghafula umeungwa kwenye group la harusi, humo bwana harusi mtarajiwa anajidhalilisha kwa kuombaomba michango mpaka unaona aibu wewe.
Hivi ni lazima uchangishe watu kwa ajili ya tukio la kukaoa hako kamwanamke kako?
By the way harusi ni utoto sana na ujinga na fake event, unapanda range na kamalaya kako kesho tunawaona kwenye IST au daladala umeshikilia bomba.
Hakuna mtu aliyewahi kupokea tuzo ya harusi bora. Usijimalize kwa madeni na kujidhalilisha kuombaomba.
Fanya sherehe yako ndogo, vaa pendeza na mkeo, alika watu wachache utakaowamudu ifanye sherehe yako ipendeze tunza kumbukumbu kwa picha na video.
Anzisha ndoa yako in peace not pressure. Usitake kuwaimpress watu for one day halafu ukabaki na years of stress za madeni.
Marriage is for life. The wedding is for a day.