Labda niulize jamani pana tofauti gani kati ya mimba ya housegirl aliyepewa na baba mwenye nyumba na mimba ya mama mwenye nyumba aliyepewa na house boy!!! nadhani kama ni aibu wote wanapata aibu sawa baba akimpa HG mimba anamuaibisha mama, jamii na familia, na mama kupewa mimba na HB ni kumuaibisha baba, jamii na familia. UZINZI ni UZINZI ni dhambi na ni kitu kibaya either amefanya baba au amefanya mama, inapaswa kulichukia ili kwa nguvu zote, lakini bado sijaona sababu ya huyu mama kupewa lawama na kutakiwa aondoke au aachwe!
siku zote nitasimama kwa haki za akinamama wanaoonewa na kurundikiwa watoto wa kutoka nje na akina baba, kama baba atasamehewa kwa kuzaa nje na kuleta mtoto ndani ya nyumba basi na mama asemehewe na mtoto alelewe, au ikilazimika ahudumiwe ukifikia umri wa kwenda kwa babaye apelekwe. kama akina baba huwa shetani anawapitia kwenda nyumba ndogo na kuzaa na HG basi na huyu mama shetani alimpitia tatizo je yupo tayari kutubu na kukubali kutorejea kosa hilo. inavyoonekana huyu mama ameelewa kosa lake kwahiyo kaka anatakiwa atumie busara na kuangalia ni jinsi gani atahandle, kubwa issue kama hii inatakiwa iwe ni handled with care within family na kwanza huyo house boy anatakiwa aondoke wakati majadiliano yanaendelea, nadhani mke na mume wana nafasi nzuri ya kulizungumza hili kabla hata ya kuwashirikisha ndugu au wazee! maana ndoa niw ao si wazee! ingawa busara za wazazi zinahitajika pale mambo yanapoenda kombo zaidi.
But all in all, huyu kaka naye ajiangalie tatizo lipo wapi isije kuwa alimuacha huyu mama kama msimamizi wa miradi "just a business partner" and not wife na ndio hapo HB akatake chance! tatizo katika ndoa watu hujisahau, before ndoa 90% ya muda unatumika kujadili mahusiano ya mapenzi zaidi, baada ya ndoa 90% ya muda unatumika kujadili business na how to rise family income na hapo ndio mambo yanapoharibika!