Mkweliii
Member
- Apr 15, 2025
- 16
- 5
UTANGULIZI.
Awali ya yote napenda kumshukru mwenyezi Mungu, muumba mbingu na nchi kwa kutujaria uhai, nguvu na uwezo wa kutukutanisha leo tukiwa wazima buheri wa afya.
SHUKRANI.
Kabla ya kuendelea naomba mniruhusu nitoe shukrani zangu za dhati kwa viongozi wafuatao ambao kwa namna moja ama nyingine wamegusa maisha ya wanabiharamulo katika nyanja chanya; napenda kuwashukuru wafuatao;
1. Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh, DTK SAMIA SULUHU HASSAN kwa kutupa fedha nyigi za maendeleo katika nyanja mbalimbali ikiwemo ile ya kimkakati kama vile barabara, umeme, elimu, afya, maji, nk.
2. Mh. Mkuu wa wilaya SACP ADVERA JOHN BULIMBA kwa kusimamia vyema fedha za serikali kiasi ambacho wilaya yetu imeendelea kujizolea sifa lukuki za kijamii na kitaifa kwa mfano wakati Mwenge wa Uhuru ulipo pokelewa na kukimbizwa wilayani 2023/2024 miradi yote iliyokaguliwa na Mwenge wa Uhuru ilipokelewa kwa kukidhi viwango vya ubora na kipindi cha 2024 wilaya yetu ilikuwa ya pili kimkoa na ya pili kitaifa. Hii ni historia kubwa katika wilaya yetu ya Biharamulo . Aidha niendelee kumpongeza Mh, Mkuu wa Wilaya kwa kuendelea kuboresha mazingira ya wafanyabiashara hapa wilayani. Vilevile nampongeza pia kwa kusimamia vyema suala zima la amani na utulivu katika wilaya yetu.
3. Mh. Mbunge wa jimbo la Biharamulo Magharibi MH, ENG, EZRA JOHN CHIWELESA Kwa kutuwakilisha vyema katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mh, Mbunge amefanya mengi ya kijimbo, kikanda na Kimataifa miongoni mwayo ikiwa ni pamoja kuwatetea wakulima na wafugaji kupata maeneo ya malisho ya mifugo, kupata mbolea kwa wakati kupata masoko ya mazao yao, mfano zao la tumbaku, kahawa kutaja kwa uchache. Katika kuhakisha Elimu inakuwa kipumbele, Mh, Mbunge alitoa hoja Bungeni kuhusu Mikopo ya Elimu ya juu, hoja ambayo iliibua hisia kubwa ambayo baadae iliungwa mkono na Waheshimiwa Wabunge wote na kupelekea serikali kutoa mikopo kwa wanafunzi waliokidhi vigezo kwa ujumla. Mh, Mbunge amefanya mengi mazuri katika jimbo letu ikiwa ni pamoja na kusimamia vyema utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya 2020-2025. Katika hili sisi sote ni mashududa kwani tunaona barabara zinajengwa kwa kiwango cha lami, changarawe na vumbi katika maeneno mbalimbali katika jimbo letu. Aidha binafsi niendelee kumpongeza Mh Mbunge kwa usimamizi mzuri wa Mfuko wa Jimbo ambapo mfuko huo umefaninikiwa kuchochea miradi ya mendeleo ya maendeleo katika jimbo letu hususani katika ELIMU NA AFYA.
Vile vile Mh. Mbunge amekuwa mstari wa mbele katika mambo yote ya kijamii na hasa kwa uamuzi wake wa busara wa kuweka huduma ya magari ya msaada Jimboni magari ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa jimbo la Biharamulo na nje ya Biharamulo.
Halikadhalika Mh. Mbunge amefanya mengi hususani katika kuibua vipaji vya vijana katika michezo mbalimbali ikiwemo kuanzisha ligi za mpira wa miguu na kutoa seti za vifaa vya michezo ikiwemo jezi, mipira na n.k.
Aidha Mh. Mbunge si tu ametoa sapoti katika mchezo wa mpira wa miguu bali pia ameendelea kutoa mchango mkubwa wa kuibua vipaji katika tasinia ya uiambaji akitumia jukwaa la Biharamulo Star search jukwaa ambalo limeibua vipaji vya vijana wengi katika tasnia ya uimbaji na kutoa zawadi mbalimbali ikiwemo PIKIPIKI na zawadi za fedha taslimu na kuwapeleka studio baadhi ya vijana kurekodi nyimbo zao.
Kama hiyo haitoshi Mh. Mbunge ameendelea kuwa mbunifu na kuleta burudani nzuri ya Desember festival, Tamasha ambalo lilitia fora kwa mirindimo ya ngoma za asili na maonyesho ya vyakula mbalimbali vya asili bila kusahau mziki wa kizazi kipya ukiungwa mkono na wasanii wakubwa na wale wa ndani.
4. UONGOZI MZIMA WA CHAMA CHA MAPINDUZI WILAYA BIHARAMULO. Chini ya uongozi mahiri wa NDG. ROBERT ALFONCE MALULU mwenyekiti wa chama na kamati nzima ya siasa ya Halmashauri kuu ya CCM, pamoja SEKRETARIETI ya chama chini ya NDG ADAM SOUD kwa namna ambavyo wanakiongoza chama katika misingi ya utu , umoja, udugu na mshikamano. Kwa hakika chama kiko mikono salama na tayari kwa uchaguzi, kushinda na kushika Dola.
5. BARAZA LA MADIWANI chini ya Mwenyekiti wake MH. LEO RUSHAHU, aidha niwapongeze madiwani wote kwa kumshauri vizuri mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Biharamulo kusimamamia shughuli zote za maendeleo katika wilaya yetu, kiasi ambacho wilaya yetu imeendelea kufanya vizuri na kujipatia hati safi katika kipindi cha ukaguzi wa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG).
6. WANANCHI WOTE, mlioacha shughuli zenu kuja kunisikiliza hapa, eidha ana kwa ana ama kupitia vyombo vya habari.
7. UONGOZI WA KIJIWE CHA SADICK, kwa kukubali mazungumzo haya kufanyika katika eneo hili maarufu ambapo mara kadhaa tumepata fursa mbalimbali ya kufanya matamasha mbalimbali likiwemo lile maarufu la SIMBA NA YANGA. Ni mani yangu kuwa mwishoni mwa msimu wa ligi kuu tutakuwa hapa tena kusherekea ubingwa.
8. Mwisho ingawa si kwa umuhimu niwashukuru, WANAHABARI NA WAANDISHI WA HABARI: Asanteni sana kwa kuja.
NIA NA MADHUNI YA KUWAITENI.
Ndugu wananchi itakumbukwa kuwa mnamo mwaka 2020 nilitia nia ya kuomba ridhaa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Biharamulo Magharibi isivyo bahati kura hazikutosha. Baada ya mchakato wa mapendekezo ndani ya chama changu cha Mapinduzi (CCM), nilishika kijiti cha kukisaidia chama changu kufanya kampeni ya kutafuta kura za, Rais, Mbunge na Madiwani, katika kipindi hicho nilibahatika kusaidia kufanya kampeni katika KATA za Bihramulo mjini, Nyamahanga na Nyarubungo. Itakumbukwa kuwa ili kuhakikisha chama changu kinashinda kwa kishindo niliomba idhini ya kulea kata mbili kwa maana ya Nyamahanga na Nyarubungo.
Baada ya kufanyika tathimini ya kina ili bainika kuwa Kata ya Nyarubungo ilihitahiji nguvu ya ziada hivyo nilijikita zaidi katika kata ya Nyarubungo kuhakisha chama changu kinapata ushindi wa kishindo jambo ambalo kwa kusaidiana na kamati ya siasa ya kata na msaada kutoka chama wilaya tulifanikiwa.
Kwakuwa nilijifanyia tathimini na kuona kuwa nimepevuka vya kutosha kifkra kufikia hatua ya kuwa mtumishi wa wananchi na nikitambua vyema kuwa pindi mtu anapo amua kuwa mtumishi wa wananchi anakuwa mali ya wananchi niliendelea kukisaidia chama changu na kujitahidi kuendelea kuonyesha sifa za uongozi katika jamii yangu huku nikisukumwa na falsafa ya Mkomunisti, Vladimir I. Lenin ambaye alikuwa kiongozi na mwanamapinduzi wa Muungano wa nchi za Kisovieti (USSR) aliye wahi kusema ….to be a leader is to be a servant of the people (1917) kwa tafsri isiyo rasmi akimaanisha kuwa …. “kuwa kiongozi ya kupasa kuwa mtumishi wa umma…..”
Katika mkitadha huo, mnamo mwaka 2022 chama kilifanya uchaguzi wa ndani ambapo katika chaguzi hizo nilijaliwa kupata nyazifa mbalimbali ikiwemo mjumbe wa mkutano mkuu Mkoa (nikiwakilisha Kata ya Nyarubungo), mjumbe, wa Halmashauri kuu wilaya na hatimae mjumbe wa kamati ya siasa wilaya ya Biharamulo na baadae mjumbe wa kamati ya maadili.
Nyazifa ambazo zinanifanya niendelee kuonyesha sifa za uongozi kwa kuendelea kukitumikia chama changu na kufanya kazi kwa bidii ndani ya chama ikiwa ni pamoja na kupokea maelekezo ya viongozi wangu na kuyafanyia kazi sambamba na kijaribu kutimiza wajibu wangu kwa wanachama wenzangu na wananchi kwa ujumla.
Vilevile kwa kushirikiana na kamati ya siasa kutoa ushauri wa namna nzuri ya kuleta ustawi ndani ya chama na jumuiya zake bila kusahau kusimamia serikali kutekeleza Ilani ya uchaguzi 2020/2025.
Kwa kuwa karibu tunaingia msimu wa kura za maoni ndani ya vyama vya siasa hususani Chama changu (CCM).
Baadhi ya ndugu, jamaa, marafiki na wazee wamekuwa na taraja nami ya kutaka niombe nafasi moja wapo katika uchaguzi mkuu huu wa 2025 uchaguzi wa RAIS, WABUNGE NA MADIWANI.
Kwa kuwa mimi ni mali ya umma na kwa kuwa nimekuwa nijitanabahisha katika mkitadha huo majibu yangu siku zote yamekuwa kusubiri muda uamue kwa kuwa niliendelea kuamini kuwa muda ni Hakimu mzuri, na sasa nadhani huu ndiyo muda muafaka wa kutolea majibu wapenzi na mashabiki zangu juu ya taraja ambalo wamekuwa wakitarajia kutoka kwangu.
Ndugu wananchi, ndugu, jamaa, marafiki na wazee wangu kwanza nikiri kuwa mmeonyesha upendo mkubwa na matumaini makubwa juu yangu asanteni sana kwa imani mliyo ionyesha na mnayo endelea kuionyesha juu yangu asanteni sana, ninaahidi kuendelea kuwa mwaminifu kwenu na kwa chama changu kwa majukumu yote ambayo chama kimenipatia na kitachonipatia hapo baadae.
Kwa kuwa bado ninaendelea na utumishi wangu ndani ya chama na kwa kuwa Mh. Rais Dkt, SAMIA SULUHU HASSAN ambaye ni mwenyekiti wa Chama Cha Mpinduzi (CCM) taifa wakati wa kikao cha Mkutano Mkuu cha tarehe 29/30 Mei 2025 kilichoketi mjini Dodoma alielekeza wajumbe wa kamati za siasa kuandika barua kwa makatibu wao iwapo wana nia ya kutia nia ya kugombea, nikatika mkitadha huo nami nimeona nitoe msimamo wangu.
Ambapo sasa natangaza rasmi kwamba;
Mwaka huu sitokuwa sehemu ya wagombea katika uchaguzi huu. Kama nilivyotoa ufafanuzi hapo awali kuwa tayari ndani ya chama ninazo nyazifa kadahaa ambazo ukomo wake ni mwaka 2027, hivyo nimeona ni vyema kwanza kuzitumikia nyazifa hizo mpaka kufikia ukomo wake.
Dhamira yangu imeniambia kuwa kuacha nyazifa hizo ambazo kimsingi ni za kujitolea ni kuonyesha uchu wa madaraka.
Mwisho lakini si kwa umuhimu napenda kuwa taarifu kuwa nimepata ufadhili wa kimasomo ambao unatarajiwa kuanza mnamo mwezi JANUARI 2026, katika hali hiyo inaniwia vigumu sana kutamani kazi ya kuwatumikia wananchi kwa kipindi cha miaka 5 ili hali nikiwa nafahamu fika kuwa ninatarajia kwenda masomoni kitendo ambacho kinaweza kutoa utumishi hafifu pia kufifisha ndoto zangu za kuendelea kusaka maarifa.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
KAZI NA UTU TUNASONGA MBELE!
NDIMI MTUMISHI WENU, BUCHANAGANDI KIIZA.
+255628628537.