Nimetafakari tu ufupi wa maisha yetu sisi wanadamu. Walakini, bado yapo mambo ambayo nafsi yangu ingetamani kuyafanya au yatimie mnamo au kablya ya umauti. Mambo hayo ni:
1. Kuwa na mapatano na muumba wangu;
2. Kutembelea mabara yote hapa duniani;
3. Kuacha legacy nzuri na mali kwa watoto na wajukuu;
4. Kutumia sehemu ya mali zangu kwa ajili ya kusaidia yatima; na
5. Kuona taifa langu linakua kiuchumi na haki na upendo kutamalaki.