Na wewe ni mmoja wa victims walioathirika na hizo propaganda za Putin za kudai kuwa Marekani inataka kuiangusha Urusi. Iwapo Marekani ingekuwa inataka kufanya hivyo, kwanza isingesimamia hiyo Budapest memorandum kuhakikisha silaha zote za Nyuklia zinakwenda Urusi na kuiacha Ukraine haine Kitu. Pili, Marekani ilikuwa na takriban miaka kumi za kuingusha kabisa Urusi yote baada ya kuvunjika kwa USSR. Badala yake katika kipindi cha kuanzia 1994 hadi 2004 Marekani iliisaidia sana Urusi kuimarisha uchumi wake bila vikwazo vyovyote; Mpaka sasa hivi Urusi inadaiwa fedha nyingi sana na Marekani ilizokopeshwa kwa ajili ya kujenga uchumi wake. Elewa hapa kuwa inadaiwa pesa ilizokopa (kama Tanzania inavyokopa), siyo pesa za kuuza hati fungante kama ambazo Marekani inadaiwa.
Tatizo la Putin ni nia ya kung'ang'ania madaraka tu, kwani kosa kubwa la Ukraine na Georgia limekuwa lile la kufanya uchaguzi na kubadilisha viongozi. Huo unakuwa ni mfano mbaya sana mlangoni mwake ambaye haamini utamaduni wa kubadili viongozi; hawezi kuishambulia Belarus mpaka pale watakapobadilisha rais
Mkuu, nilikuwa naamini ukiandika kitu basi ni madini matupu, ila sasa napata mashaka kama una ID moja au?
Baada ya US kufanikiwa kuiangusha USSR ndo fedha hizo unozisema zikaingizwa kwenye mfumo wa fedha wa Russia.
Kila kitu kikabadilika na hata küpelekea Urusi kuwa nchi ya wapigaji, ikiongozwa na magenge ya wahuni, wenye pesa na madon.
Watu kuuawa mitaani ilikuwa ni kawaida na khasa raia wa kigeni waliuawa sana, nchi ilikuwa haina order.
Mazee au Deep State wakawa wamechoshwa na mwenendo wa Boris Yetsin na kama wakumbuka Yetsin alikuwa mlevi wa kupindukia.
Putin alianza kusogezwa kwenye system ilosukwa upya na DS na ndo akaanzia kwenye manispaa, ukurugenzi wa FBI baadae FSB, waziri mkuu na kisha uraisi.
Wakati jina la Vladimir Putin latajwa kuwa afaa kuwa waziri mkuu yeye mwenyewe alikuwa vekesheni nchi moja hivi akiwa mkurugenzi wa FSB.
Hiyo yote unosema US alitoa fedha yaweza kuwa ni sawa lakini fedha hizo zilikuwa zaliwa na wapigaji, maana huşuna huduma muhimu kama afya zilizorota.
Urusi sasa hivi ina fedha au mali katika mabenki ya US na huko West lakini ni fedha zake na zikichukuliwa ili apewe Ukraine huo ni wizi.
Pia hawa West wakichukua fedha za Russia watasababisha mtikisiko kwenye mfumo wa fedha kwani China au Saudi Arabia na nchi zingine zaweza kuamua kuundosha mali zao huko, wadhani litakuwa jambo jema?
Walosoma alama za nyakati ni wazalendo wa DS ambao walikuwa kutambua kuwa Urusi inaweza kusimama kuwa taifa kubwa tena lenye uchumi imara, kijeshi, kiteknolojia na kujasusi duniani na ikachagua rasmi nchi rafiki Iran na China kuwa nchi mwenza kwenye malengo hayo.
Kuvamiwa kwa Crimea 2014 mama Angela Makel amesema kwamba mkataba wa Minsk ulikuwa ni kuwanunulia muda Ukraine ili waweze kujijenga kijeshi kwa silaha za NATO.
Je, ulidhani Urusi na majasusi wake wangeketi tu bila kumtahadharisha Putin kuwa wakati wowote Urusi yaweza kuvamiwa?
Hata kuvamiwa kwa Ukraine mwaka 2022 ilikuwa ni baada ya waasi wa Donbas ambao walitangaza kujitenga na Ukraine ambao kwa sera zao mbaya za kikatili walikuwa wakiwatesa na kuwaua raia wengi yaani majority ambao wazungumza kirusi na si kiukraine.
Walosaidia kuiweka madarakani serikali ya Kyiv ni haohao West lakini wakawa wakiwafumbia macho hao wanazi na kuachia wafanye mauaji.
Ndugu, tambua kuwa Dunia sasa ishageuka uwanja wa vita, kuna binadamu wenzetu wajiona wao ni super race na waweza kufanya chochote na wasiwajibishwe.
Bila shaka umeona yanotokea Gaza ni mfano tosha. Kanchi kamoja kanaamua kuleta zogo na kasiguswe bali ni kushikwa tu sikio.
Vita kubwa ni resources na ni lazima utoe resources hizo kwa watu sahihi ambao ni nchi za Magharibi wakiongozwa na Marekani.
Russia wasema hapana lazima kuwepo usawa katika kuitawala dunia maana neno New World Order limebadilishwa na kuwa Rules Based Order yaani kikundi cha nchi chache chajipa mamlaka ya kuamua mambo ya Dunia.
Nina mengi ya kuchangia lakini haya yatosha.