We jamaa acha uongo russia haijawahi kukopeshwa mkopo na marekani eti uchumi wa russia umejengwa na marekani yaani adui yako kabisa umsadie kuimarisha uchumi wake leta chanzo cha hiyo habari inayoonyesha kwamba marekani imetoa dollar million kadhaa kuisaidia russia.
Ki historia Ukraine imebadilisha viongozi wengi kuanzia 1991 tena walikuwa wanabadilisha kwa kupokezana term hii akishika Pro-west term inayokuja inashika Pro-Russia hiyo imeenda hivyo mpka mwaka 2014 sasa unavyosema wakifanya uchaguzi, ndo russia huzivamia huo nao ni uongo.
Uvamizi uliofanywa Georgia ilikuwa ni baada ya kutaka kujiunga na NATO, Kama sikosea ni 2008 rejea NATO summit ya mwaka huo waliotaka kujiunga ilikuwa yeye na Ukraine ila baadhi ya member wa NATO walikataa ikiwemo German na Ufaransa ambao nao waliona wakizikubalia itazua vita ila walichowaahidi ni kwamba kwa baadae inaweza kuwafikiria na mwaka huo huo baada ya hiyo summit ndo georgia ilivamiwa na russia.