Bukavu: M23 yakaribia uwanja wa ndege wa Kavumu

Bukavu: M23 yakaribia uwanja wa ndege wa Kavumu

Kama ndo hivo; ni bora tukae pembeni tuwaachie mambo yao wayamalize wenyewe.
M23, kufa wanakufa. Kwani wao si wameumbika kama binadamu wengine? NA huenda wanapoteza zaidi. Ila, matokeo ndo huonyesha nani ana nguvu! Jeshi la DRC,lilifarakana na wazalendo. Wazalendo ndo wanatakiwa wakae frontline. Sasa, mtu ana training ya wiki moja au mbili. MWanajeshi aliezeekea kazini,aliepata mafunzo, anakimbia. Unategemea nini? Umemleta mamluki,unamlipa dola elfu 8 au 10 kwa mwezi. Mwanajeshi mzawa anapata 150. Unategemea hiyo vita inawezekana kweli?
 
Kinachoniuma sana Rwanda inaingia mala 90 kwa Congo Drc.

Yani Eneo la Rwanda ni mala 90 ya eneo la Congo.

Congo shenziiiiiii kabisa
ccmu wanafuata Nyayo za MOBUTU kuua uzalendo kwa wananchi kwa kuwatenganisha wananchi na siasa za nchi yao kwa kuwateka , kuwafunga au kuwaua kbs wote mnaojaribu kuikosoa au kuishauri serikali , inapofika muda unawaitaj wananchi kupigani nchi yao , unakuta wananchi hawana huo moyo tena maana nyiny wachache mlijiona ndo weny nchi na wananchi hawataki wapigani wachache
 
Yan askari anaacha kuwalinda raia au nchi yake unageuka kuwa mmojawapo wa waporaji. Inashangaza.
Usiamini maneno ya mtandaoni.
Ungejua mleta mada ni nani na lengo lake JF ni lipi, na majukumu kapewa na nani.

Siku yoyote ukiona mtu username ni Mtume Yohana alafu anauponda Ukristo, shtuka jiongeze.
 
KWani, mpaka hizo EAC na SADC zinamuamulu akae meza moja na M23, wakuu wa nchi hao wote ni wajinga?
walishakaa na walikubaliana kuunganisha jeshi liwe moja , ila baadhi ya waasi waligoma na kurud msituni , waasi ni km vile wana agenda ya siri sio kwa DRC tu bali hata Tz na wengineo wa ukanda huu , tuwe makini

Mwaka 1994 huki Arusha Rais wa Rwanda Habyamara na Jeshi la watusi la Kagame muafaka uliwataka waunganishe majeshi ila watutsi hawakuwa tyr na waliamua kuchochea vile vita vya 1994 , hawa watutsi hawajui amani km mnavyodanganyana humu
 
Unajua Afrika Kusini ilikuwa na wanajeshi wangapi hapo Congo?
Na unajua ilikuwa na majukumu gani?

Yani Afrika Kusini hii inayouza silaha Marekani, Ujerumani na Finland itishiwe na M23. Walete brigade mbili full armed na waje kupigana vita uone kama kuna panya wa Rwanda au M23 utamuona hapo Mashariki mwa DRC.
Sawa, ndo nachokuuliza, mzozo wa bungeni kwao unahusu nini! Hawajui wanajeshi wao ni mateka? Kwa taarifa yako sasa, M23 iko tayari kuwaachia huru, lakini, hakuna siraha wala gari kuachiwa. Tayari ni mali ya M23. Kilichoshindikana kuwaondoa mpaka leo, wanataka wakiondoka, njia ni Rwanda hamna option nyingine. Waondoke kama wanadiplomasia(hakuna kupekuliwa wala kupigwa picha). Rwanda hilo, ilishalikataa
 
walishakaa na walikubaliana kuunganisha jeshi liwe moja , ila baadhi ya waasi waligoma na kurud msituni , waasi ni km vile wana agenda ya siri sio kwa DRC tu bali hata Tz na wengineo wa ukanda huu , tuwe makini

Mwaka 1994 huki Arusha Rais wa Rwanda Habyamara na Jeshi la watusi la Kagame muafaka uliwataka waunganishe majeshi ila watutsi hawakuwa tyr na waliamua kuchochea vile vita vya 1994 , hawa watutsi hawajui amani km mnavyodanganyana humu
Kikao cha juzi tarehe 8
 
Kabla ya DRC, South Africa kiliipata nini!Je, unajua wanajeshi wake sasa hivi wanatunzwa na M23? Maji, chakula, matibabu! Goma ilikaliwa na M23 tarehe ngapi? Kama intelligensia ya Afrika kusini iliingia mkenge, ya DRC inaweza! Na mbaya zaidi, wao wenyewe wanasalitiana.
je kwa hesabu za haraka unahis kikundi cha kias kinaeza fanikisha hilo bila nguvu nje ya Afrika ? ( Rwanda hana pia ubavu huo wa kuifanya SA hv )
 
Baada ya Goma kuangukia mikononi mwa M23, mtutu wa bunduki ulielekezwa Kivu kusini, huku mji mkuu ukiwa Bukavu.

Serikali ya Burundi kwa makubaliano na DRC, ilipeleka wanajeshi wapatao elfu 10 kuhakikisha Bukavu inalindwa kwa nguvu yote.

Uwanja wa Kavumu, unatumiwa na serikali ya Burundi na DRC kuleta siraha toka Kinshasa na Bujumbula.

Baada ya wanajeshi hao kushindwa kuwazuia wakiwa Kalehe, vita vinaendelea eneo la Katana, ambalo lipo umbali wa km 11 tu kutoka uwanja wa ndege huo wa Kavumu.

Kukamatwa kwa uwanja huo, kutaondoa uwezekano wa serikali ya Burundi na kinshasa kuongeza nguvu. Hapo juzi, jeshi la Congo lilivamia wafanyabiashara na kupora mali zao, benki zimeibiwa.

View: https://x.com/kabagambei/status/1888701569870319802?s=46
Video, ni wanaouwawa Kivu kusini,kisa kuwa watutsi.

DRC is a failed State.

Utawala uliopo huko upo dhaifu Sana.
Jeshi la Ulinzi la nchi hiyo pia lipo dhaifu Sana kupita kiasi.

Jeshi la DRC lipo uchi wa mnyama kwa Utawala wa Rwanda.
Kuna uasi wa chini chini usiokwisha ndani ya Jeshi la DRC.

Wanajeshi wengi sana wa DRC pia ni Wapiganaji wa Siri wa M23.

Viongozi wengi wa Serikali ya DRC pia ni Mawakala wa Siri wa Utawala wa Rwanda na Vikosi vya Waasi wa M23.

Try to imagine: General Kabarebe aliwahi kuwa Mkuu wa Majeshi (CDF) wa nchi hiyo ya DRC, lakini baadaye Mwanajeshi huyo alihama nchi na kwenda kuwa Mkuu wa Majeshi (CDF) wa nchi ya Rwanda.

Wewe uliwahi kuona wapi jambo la namna hii?
 
Kikao cha juzi tarehe 8
hayo maamuz ya juz yalishafanyika mara 2 , ila watutsi ndo wakaigi mara zote , kwann alienda Kagame na sio M23 , je Kagame ana maslai gan na DRC ? je Kagame ni kiongoz wa waasi ambao alishawakana sio wanyarwanda na yeye ni rais wa Rwanda ( yaan mnyarwanda )
 
Kwa namna nilivyojua chanzo Cha mgogoro ni kubaguliwa Kwa banyamulenge ambao walitenganishwa na mipaka tu ya kikoloni na hitimisha Kwa kuwatakia M23 ushindi mnono ili kuuondoa huo ubaguzi wa kijinga wa watawala wa DRC.yaano ni sawa na sisi tuseme wamasai siyo watanzania Kwa sababu Kuna wamasai wanaoishi Kenya.
Hujui kitu kijana wangu, hii siyo suala la banyamulenge kutengwa hapo ni PK anapambania mkataba wa makubaliano humo ndani yumo mzee kaguta.

Hili jambo lipo chini sana huko.
 
Sawa, ndo nachokuuliza, mzozo wa bungeni kwao unahusu nini! Hawajui wanajeshi wao ni mateka? Kwa taarifa yako sasa, M23 iko tayari kuwaachia huru, lakini, hakuna siraha wala gari kuachiwa. Tayari ni mali ya M23. Kilichoshindikana kuwaondoa mpaka leo, wanataka wakiondoka, njia ni Rwanda hamna option nyingine. Waondoke kama wanadiplomasia(hakuna kupekuliwa wala kupigwa picha). Rwanda hilo, ilishalikataa
Afrika Kusini idadi yake kubwa ya wanajeshi pale DRC kwenye SAMIDRC ni 800 at highest peak kipindi hiki, wakati Rwanda ina wanajeshi 10,000 Congo disguising as M23 na wanauwawa daily hata maofisa.

South Africa haina helicopters wala fighters, last time 2013 ilipoleta helicopters M23 waliacha kupigana ndani ya wiki tu maana walikuwa wakijikisa kidogo wanauwawa. Ndio ile mission wabongo waliisifia sana JWTZ wakati kazi kubwa ilifanywa pia na South Africa hasa air cover.

Ukisema South Africa ilete idadi sawa ya wanajeshi wa Rwanda hapo Congo na ije na silaha zake nzito, Rwanda wanajeshi watakimbia majukumu wawe wafugaji wa Banyamurenge.
 
je kwa hesabu za haraka unahis kikundi cha kias kinaeza fanikisha hilo bila nguvu nje ya Afrika ? ( Rwanda hana pia ubavu huo wa kuifanya SA hv )
Kwani, hiyo DRC inapoleta mamluki, warundi wasouth na kuferi, hao wote hawana nguvu? Swali la kujiuliza nadhani lingekuwa ni nani yupo nyuma ya hawa watu! MONUSCO ilisema haiwezi tena kutumia mifumo yake kwa sababu ya system ya Rwanda ya jamming. Mpaka Rwanda iwe na mfumo huo,ambao wanachama wa UN hawawezi kubypass, hauoni kuna jambo au nguvu kubwa nyuma ya haya yote!?
 
Kwani, M23 ni mwanachama wa EAC? Usichanganye mafaili ndugu. Waliitwa wakuu wa nchi, wanachama wa EAC na SADC. Issue ikiwa wao kwa wao, waone kipi kifanyike. Na hili, ni baada ya kuona kunaenda kuzuka mzozo kati ya jumuia hizi mbili. Mpaka sasa, EAC, kuna ambao wapo upande wa DRC, na wengine upande wa M23. SADC hivo hivo.
Kikao chao ndo kiliamua DRC ikae na M23. Hilo ni jukumu la Angola na Nairobi kusimamia makubaliano hayo kati ya Rwanda, tall na M23. Kagame anahusika kwa uwepo wa FDLR asiyoyitaka huko DRC.
 
Rekebisha. Aliwahi kuwa CDF wa nchi mbili hizo kwa wakati mmoja
 
Afrika Kusini idadi yake kubwa ya wanajeshi pale DRC kwenye SAMIDRC ni 800 at highest peak kipindi hiki, wakati Rwanda ina wanajeshi 10,000 Congo disguising as M23 na wanauwawa daily hata maofisa.

South Africa haina helicopters wala fighters, last time 2013 ilipoleta helicopters M23 waliacha kupigana ndani ya wiki tu maana walikuwa wakijikisa kidogo wanauwawa. Ndio ile mission wabongo waliisifia sana JWTZ wakati kazi kubwa ilifanywa pia na South Africa hasa air cover.

Ukisema South Africa ilete idadi sawa ya wanajeshi wa Rwanda hapo Congo na ije na silaha zake nzito, Rwanda wanajeshi watakimbia majukumu wawe wafugaji wa Banyamurenge.
Nimeuliza, wanajeshi wa SA, waliokwenda huko kama SAMIDRC, leo hii wako wapi?
 
Attachments

  • IMG_0021.jpeg
    IMG_0021.jpeg
    167.3 KB · Views: 3
Back
Top Bottom