Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Lugano5

R I P
Joined
Jul 15, 2010
Posts
4,520
Reaction score
757
Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria

20221106_101403.jpg

IMG-20221106-WA0014.jpg





===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022

Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.

Taarifa kwa kina zinafuata

=====

NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.

Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege imepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.

Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”

ABIRIA waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba wameokolewa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha.

Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mwampaghale amesema manusura wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.

“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema nakuongeza “tukio lipo ‘under control.’”

Mwampaghale amewataka wananchi kupunguza taharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndege hiyo inatolewa majini.

Imeandaliwa na Diana Deus

====

UPDATE: WATU 26 WAMEOKOLEWA KATI YA 43 KATIKA AJALI YA NDEGE
Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba ilibeba watu 43 na tayari waliookolewa ni 26 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa taarifa hiyo kuhusu ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikuwa na safari ya kurudi Dar.

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema zoezi la uokoaji la ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba linaendelea kwa kuivuta ndege kuelekea ufukweni.

===============

UPDATE: WATU WATATU WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI

Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera Dkt. Isesanda Kaniki amesema hadi kufikia saa 9 alasiri wamepokea maiti za watu 3 waliofariki katika ajali

Amebainisha kuwa wamepokea jumla ya watu 26, Wanaume 17, Wanawake 9, huku Wanaume 2 na Mwanamke 1 wakipokelewa wakiwa wamefariki dunia.

UPDATE: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini watu wawili wanaozidi kwenye idadi iliyoainishwa mwanzo ya watu 43. Hatua hiyo imekuja baada ya kupatikana kwa miili 19 ya waliofariki huku wengine 26 kuokolewa hivyo kufanya idadi ya watu kuwa 45.

UPDATE: WATU 19 WAMERIPOTIWA KUFARIKI MPAKA SASA
Vikosi vya Uokoaji na Wananchi wanakaribia kuifikisha nchi kavu Ndege ya Precision iliyopata ajali Ziwa Victoria, Bukoba takribani mita 100 kutoka Kiwanja cha Ndege ilikotakiwa kutua, ajali hiyo imeua Watu 19 na wengine 26 wameokolewa.

WALIOFARIKI AJALI YA NDEGE KUAGWA UWANJA WA KAITABA
Miili ya Watu 19 waliofariki katika ajali ya ndege ya Precision Air inatarajiwa kuagwa leo Novemba 7, 2022 kwenye Uwanja wa Kaitaba, Bukoba.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema utaratibu wa zoezi la kuaga unatarajiwa kukuanza Saa 4 asubuhi ukiongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
 
Aanh

Ni hatari sana kupanda usafiri wa meli na ndege kwa hizi nchi zinazoitwa 3rd countries

Miaka 5 nyuma nakumbuka natoka Dar naenda Mbeya na hizi ndege za mtumba alizotuletea anko magu
Maeneo ya Iringa pale kitonga, ndege linayumba kwa sababu ya kani ya mvutano

Nilisali salamu maria mara 1, baba yetu mara 2
Na nikapiga Alu akbar kama 5 hivi
 
Mungu awaokoe waliomo. Maana ziwa kubwa kama hilo lakini hatuna mfumo mzuri wa kuokoa watu wakipatwa na majanga.

Tangu ajali ya Mv Bukoba mwaka 1996 ilipotokea hakuna juhudi za maana za kuwa na mfumo wa kisasa wa uokozi kwenye ziwa hilo kubwa barani Afrika.
 
Mitumbwi ya mbao ndo inaenda kuokoa, inajulikana wazi , huo uwanja upo karbu na ziwa , ajali kama hzi kikawaida ilitegemewa , mana duniani kote 80 % ya ajali za ndege hutokea during take_off and during landing , sasa wanakosaje facilities za uokozi kwenye maji , na ajari imetokea karbu na uwanja hapo na sio far away ,kweli hii nchi ipo Zama za kijenkitile ngwale,
 
Mungu awaokoe waliomo. Maana ziwa kubwa kama hilo lakini hatuna mfumo mzuri wa kuokoa watu wakipatwa na majanga.

Tangu ajali ya Mv Bukoba mwaka 1996 ilipotokea hakuna juhudi za maana za kuwa na mfumo wa kisasa wa uokozi kwenye ziwa hilo kubwa barani Afrika.
Inasikitisha sana
 
Inaonekana ni karibu na ufukweni sijui ingekua katikati huko kama tungejua.
 
Back
Top Bottom