Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Bukoba: Ndege ya Precision Air yapata ajali Ziwa Victoria, watu 19 wafariki dunia

Kuna uzi mtu alitabiri kama wiki mbili zilizopita kwamba kuna ndege itaanguka TZ na akaishia kula matusi. Huu hapa

Ila amechemka kusema watu watakufa wengi na ndege kukatika vipande
 
Rubani wa ndege ya Precicion Air iliyopata ajali ziwa Victoria leo, Kapteni Buruhani Rubaga (pichani) ni mzoefu katika sekta ya anga kwa miaka 20, huku msaidizi wake, akijulikana kama First Officer Peter Omondi.

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amesema kuwa mawasiliano kati ya marubani walio ndani ya ndege na mamlaka yanaendelea.

Ndege hiyo namba PW 494, ina miaka 12 tu kazini; kwa wanaofuatilia mambo ya ndege na teknolojia ya anga, ndege hiyo bado ni mpya na kama mamlaka zilivyosema kuwa hali ya hewa ndiyo iliyosababisha ajali hiyo, naungana nao.

Waliowahi kusafiri na ndege hiyo wanaisifu kwa huduma nzuri na umahiri wa marubani.

Ndege hiyo ilikuwa inatokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba.

Taarifa zaidi zitatolewa na mamlaka husika.
#precisionair
View attachment 2408407
Kwahiyo Rubani Mzoefu Kazamisha Ndege au? Halafu naomba kujua inawezekana vipi Ndege kama hiyo ikwa imeanguka na Kuzimika kabisa hata kwa Mitambo yake halafu Marubani wake bado wawe na access ya Mawasiliano na Mkuu wa Mkoa Samjo Samjo ( Msanii ) kama Albert Chalamila na Wengineo?
 
BBC wameonyesha live ila huku ni kwaya tu as if ni kama kasiri fulani hivi yani hii nchi siasa mpaka kwenye uhai wa watu,poor country with evil political instability
Huo uokoaji wenyewe ni kuvuta ndege na manila.
Wakati kuna helkopta za kuzungukia majina ya mitaa na kuonyesha sensa. Yaani hii nchi imekuwa ya siasa kuliko kudeal na maisha ya watu. Tumuombe sana Mungu awafumbue viongozi wetu macho.
 
Watu wengi wanajifanya kuwa wanamjua yesu ama Mungu Ila hawajui kanuni za kiroho zinavyofanya Kazi. Yaani tumedandia hizi dini za weupe bila kuzijua Kuna vitu tulifulichwa.
Watu hawaelewi kuwa Kuna watu huwa wanaonyesha ama wanaona tukio la kesho na pia kuona visivyoonekana ,sio kwa ndumba wala kuchanjwa Bali wamepewa uwezo huo na muumbaji mwenyewe.
Nina mtu wa karibu yangu anaonaga tukio mpaka watu wanamchukia so ikanifanya kuzama deep down the sea not in the shores to find if the Pearl existence is Truth or people's myth. But I found it really exist but in not shallow water in the deep depths of the ocean.
Hata kwenye Biblia wapo wanaitwa waonaji...
 
Aanh

Ni hatari sana kupanda usafiri wa meli na ndege kwa hizi nchi zinazoitwa 3rd countries

Mika 5 nyuma nakumbuka natoka dar naenda mbeya na hizi ndege za mtumba alizotuletea anko magu
Maeneo ya iringa pale kitonga, ndege linayumba kwa sababu ya kani ya mvutano

Nilisali salamu maria mara 1, baba yetu mara 2
Na nikapiga Alu akbar kama 5 hivi
Kweli ni hatari, Ila tatizo umbali...
Ukitoka Dar kwenda Mza au huko Bk na basi ni kama unaenda nchi nyingine. Unadamka asubuhi unafika huko usiku wa manane! Basi ikikorofisha njiani inakuwa kero zaidi. So, watu hulazimika, hakuna namna!
 
Technically ndege ipo sealed kias kwamba ikiwa angani hairuhusu hewa kuingia. Same as kwa hilo tukio ndege kuingia ndan ya maji.

Maji yatakayofanikiw kuingia hayatakuwa mengi..

Hivyo Raia wapo salama kwa asilimia nyingi isipokuwa wale waliopata mshtuko wa hapa na pale.
Ingekua haijaingia maji Ingekua inaelea juu ya maji na sio kuzama kama inavoonekana
 
Kukaa under water Kwa dk 15 tuu , inatosha kuwaondoa wote , kimsingi sidhani kama kuna majeruhi , labda wakianza kushuhudia
kuna picha nimeona twitter kwenye comment wamelazwa chini kwenye post ya prezda na kama ni genius jibu tiyari unalo.

Hao majeruhi nadhani watakuwa ni invisible.maana sound nyingi uhalisia zero.
 
Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria
View attachment 2408224
View attachment 2408189
View attachment 2408195



===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA

Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022

Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.

Taarifa kwa kina zinafuata

=====

NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.

Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege umepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.

Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”

ABIRIA waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba wameokolewa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha.

Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mwampaghale amesema manusula wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.

“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema nakuongeza “tukio lipo ‘under control.’”

Mwampaghale amewataka wananchi kupunguza haharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.

Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndge hiyo inatolewa majini.

Imeandaliwa na Diana Deus

====

UPDATE: WATU 26 WAMEOKOLEWA KATI YA 43 KATIKA AJALI YA NDEGE
Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba ilibeba watu 43 na tayari waliookolewa ni 26 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera.

Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa taarifa hiyo kuhudu ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikua na safari ya kurudi Dar.

Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema zoezi la uokoaji la ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba linaendelea kwa kuivuta ndege kuelekea ufukweni.

===============

hatari
 
Hata kwenye Biblia wapo wanaitwa waonaji...
Sasa mbona juna watu wanakemea eti shindwa katika jina la yesu. Yaani watu na mapokeo yao bana mpaka nacheka. Napenda afrika tuwe Kama tulivyokuwa fresh na mind zetu before Arabs and Europeans invasion Kuja kutuchafua akili zetu.
 
Hiyo Milango ya Dharula huwa inafunguliwa na hao Cabin Crew Ndege yote Kasoro Mkia tu ikiwa imezama Majini tena katika Kina kama iliyopo?

Hivi una Akili kweli Wewe au unataka tu Kutuchosha hapa Watu wenye Akili nyingi kutuzidi mpaka zingine tunafikiria Kuzipunguza?
Katika mazingira ya ajali kama hiyo, Mungu huwajalia watu ujasiri na uthubutu wa hali ya juu!! Amini usiamini milango ya dharula ilifunguliwa na kwa taarifa zilizopo takriban watu 26 wameshaokolewa na kupelekwa hospitali ya mkoa-Bukoba!
 
Back
Top Bottom