Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
😀😀😀Yule jamaa aliwahi kusema amewasiliana na mwendazake wakati ameshakata moto...usimchukulie siriazi🐒
Kasikilize mwananchi digital youtube. Mara ya kwanza alisita kushuka na wakazunguka huko misenyi. Ila wakarudi tena kutua hali ikiwa ileile. Huoni alikosea sana ?Si bora angerudi Mwanza. Alijiamini nini kushindana na nature?Ukiona ajali imetokea jua rubani kajitahidi mno. Ukipigwa na tail wind na ushashuka kiasi huwezi paa tena, hiyo ndo mwisho
Kampuni yenyewe inalipa kidogo .ila mkiwashitaki inabidi muombe kiasi kikubwa na mnegotiate. Unafikiri wakitoa tu wenyewe watatoa nyingi bila kushurutishwa ?Hata zisipofungua utaratibu huwa ni kuwa lazima wawalipe fidia
Huangaliagi ile channel ya dstv inayoonyeshaga investigation za ajali za ndege duniani kote?
Ambao hawakufikiwa na maji si walitoka mlango ulipofunguliwa. But let’s say uko sahihi, so rubani alikuwa anawasiliana vipi na rc😂Nadhani baadhi yao maji hayakuwafikia inaelekea ndege ilitanguliza nose chini ya maji ikajikita wengine wakawa juu wale waliokaa seat za nyuma
Vipi kama hakuwa na mafuta?Kasikilize mwananchi digital youtube. Mara ya kwanza alisita kushuka na wakazunguka huko misenyi. Ila wakarudi tena kutua hali ikiwa ileile. Huoni alikosea sana ?Si bora angerudi Mwanza. Alijiamini nini kushindana na nature?
Hiyo mawasiliano ya RC na Rubani ni SIASA tu!Ambao hawakufikiwa na maji si walitoka mlango ulipofunguliwa. But let’s say uko sahihi, so rubani alikuwa anawasiliana vipi na rc😂
RC muongo yule.Ambao hawakufikiwa na maji si walitoka mlango ulipofunguliwa. But let’s say uko sahihi, so rubani alikuwa anawasiliana vipi na rc😂
Precision air yapata ajali Bukoba ziwa Victoria
View attachment 2408224
View attachment 2408189
View attachment 2408195
===
NDEGE YA PRECISION YAANGUKA ZIWA VICTORIA MJINI BUKOBA
Ndege ya Shirika la Ndege la Precision, imeanguka ziwani mjini Bukoba, Mkoani Kagera asubuhi ya leo Novemba 6, 2022
Taarifa za awali zinaonesha ndege hiyo imeanguka ziwani, uokoaji wa abiria unaendelea.
Taarifa kwa kina zinafuata
=====
NDEGE YA PRECISION AIR ILIKUWA IKIJIANDAA KUTUA
Mmoja wa abiria wa Precision Air, Simon Mkina amesema tukio hilo limetokea asubuhi ya leo Novemba 6, 2022 Saa mbili kasoro dakika 10 wakati ndege ikiwa inajiandaa kutua.
Amesema “Nipo eneo la tukio, nilikuwa naisubiri hiyo ndege kurudi Dar es Salaam, ghafla tukaona ndege imepitiliza, rubani ikashindwa kutua kwenye njia yake, inawezekana amekosa mawasiliano au kuna hitilafu ilitokea.
Ameongeza “Mpaka sasa hatujajua nini hasa ni chanzo kwa kuwa rubani mwenyewe bado hajatolewa ndani ya ndege na uokoaji unaendelea.”
ABIRIA waliokuwa katika ndege ya shirika la ndege la Precision Air iliyoanguka katika Ziwa Victoria kabla ya kutua uwanja wa ndege wa Bukoba wameokolewa, Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Kagera, William Mwampaghale amethibitisha.
Akitoa taarifa ya awali kuhusu ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba, Mwampaghale amesema manusura wote wamepelekwa katika hospitali ya rufaa mkoa wa Kagera kwa ajili ya matibabu.
“Ndege ilipata ajali mita 100 kabla ya kutua uwanja wa ndege. Abiria wameokolewa na jitihada zinaendelea,” amesema nakuongeza “tukio lipo ‘under control.’”
Mwampaghale amewataka wananchi kupunguza taharuki na kuondoka eneo la tukio ili kuruhusu vyombo husika kuendelea na shughuli za uokozi.
Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokozi Zabron Muhuma amesema jeshi linaendelea na uokoaji ili kuhakikisha ndege hiyo inatolewa majini.
Imeandaliwa na Diana Deus
====
UPDATE: WATU 26 WAMEOKOLEWA KATI YA 43 KATIKA AJALI YA NDEGE
Ndege ya Precision Air iliyopata ajali wakati wa kutua Bukoba ilibeba watu 43 na tayari waliookolewa ni 26 ambao wamepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera.
Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Albert Chalamila ametoa taarifa hiyo kuhusu ndege hiyo ATR 42 yenye namba za usajili 5H BWF ambayo ilikuwa ikitokea Dar es Salaam kuelekea Bukoba na ilikuwa na safari ya kurudi Dar.
Aidha, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amesema zoezi la uokoaji la ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 2:35 asubuhi ikiwa ni mita 100 kabla ya kutua katika Uwanja wa Ndege wa Bukoba linaendelea kwa kuivuta ndege kuelekea ufukweni.
===============
UPDATE: WATU WATATU WAMEPOTEZA MAISHA KWENYE AJALI
Mganga Mkuu Mkoa wa Kagera Dkt. Isesanda Kaniki amesema hadi kufikia saa 9 alasiri wamepokea maiti za watu 3 waliofariki katika ajali
Amebainisha kuwa wamepokea jumla ya watu 26, Wanaume 17, Wanawake 9, huku Wanaume 2 na Mwanamke 1 wakipokelewa wakiwa wamefariki dunia.
UPDATE: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameagiza uchunguzi ufanyike ili kubaini watu wawili wanaozidi kwenye idadi iliyoainishwa mwanzo ya watu 43. Hatua hiyo imekuja baada ya kupatikana kwa miili 19 ya waliofariki huku wengine 26 kuokolewa hivyo kufanya idadi ya watu kuwa 45.
una uhakika walikuwa na mafuta ya kuwarudisha hadi Mwanza?Kasikilize mwananchi digital youtube. Mara ya kwanza alisita kushuka na wakazunguka huko misenyi. Ila wakarudi tena kutua hali ikiwa ileile. Huoni alikosea sana ?Si bora angerudi Mwanza. Alijiamini nini kushindana na nature?
Alikuwa anaweka matumaini kwa ndugu za waliokuwa kwenye ndege, hakuwa na jinsi lazima SIASA itumike.RC muongo yule.
Hiyo haipo. Mafuta huwa yapo ya kutosha kwa emergency. Kwani wewe unafikiri hawajui mtu unaweza kwenda Bukoba usishuke na kuamua kwenda kiwanja cha karibu. Kwa hapa ni Mwanza.Vipi kama hakuwa na mafuta?
Rubani haamui kutua au kuzunguka, anapokea maelekezo ya Tower ya eneo husika
Kwani waliofariki ni wa Bukoba (Kagera)?Mkurugenzi wa Precision Air ,jiandae kukutana na Wakili msomi Kibatala kisutu.
Kwani wakazi wa BUkoba ni wasomi watadai mabilioni ya Bima.
Sababu ya kitoto hii. Wanatakiwa wawe proactive na mafuta ya kukurudisha Mwanza incase of anything yanakuwa calculated.una uhakika walikuwa na mafuta ya kuwarudisha hadi Mwanza?
At the end of the day PILOT ON COMMAND ndo ana last say...tower anampa tu ushauriVipi kama hakuwa na mafuta?
Rubani haamui kutua au kuzunguka, anapokea maelekezo ya Tower ya eneo husika
Ndege haiwezi paa kama haina coverHii ndege ilikuwa na insurance kweli, ndiyo maana mkurugenzi analia gharama zake ni kubwa ikiwemo fidia
Hakuna ndege inayoruhusiwa kuondoka bila kua na mafuta mara mbili ya kiwango Cha mda unatumia kufika kwenye destination...hivyo basi mafuta ya kutosha kwenda kwenye alternative kiwanja lazima yawepouna uhakika walikuwa na mafuta ya kuwarudisha hadi Mwanza?