A
Anonymous
Guest
Mimi ni miongoni mwa walimu wa Sekondari (ajira mpya) mwaka 2025.
Baadhi tumeajiriwa mwezi wa pili, wa tatu hadi wa sita - lakini mpaka leo hatujapata pesa ya kujikimu.
Wenzetu walipewa pesa hiyo mnamo mwezi wa kumi na moja na na sisi hatujui muafaka wetu ni upi na kumekuwa na ubabaifu mkubwa wa utekelezaji wa majukumu katika halmashauri hii ya Bukombe.
Kwanza walimu wa biashara waliajiriwa mwezi wa pili lakini walikaa miezi miwili bila kupata mishahara yao ilhali watu walioajiriwa nao wakati mmoja na hata baada yao katika Halmashauri nyingine walipewa mishahara yao kwa wakati.
Tumekuwa tukifuatilia katika Ofisi ya Idara ya Elimu Sekondari na Ofisi ya Mkurugenzi lakini majibu yao ni kwamba pesa zikiingia mtapewa.
Hivi ni kigezo kipi kilitumika kuwalipa walimu wa Shule ya Msingi na kuacha malipo ya walimu wa Sekondari?
Naomba tusaidiwe kupata haki yetu, maana ni almost mwaka hatujapata malipo hayo.
Mpaka ajira nyingine mwaka huu zimetangazwa, sisi bado hatujalipwa
Asante