Bulaya: Kikokotoo kipya cha Mafao ni kibovu na kinawapangia Wastaafu matumizi ya fedha zao

Bulaya: Kikokotoo kipya cha Mafao ni kibovu na kinawapangia Wastaafu matumizi ya fedha zao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya, amesema sio sawa kwa Mtumishi aliyeitumikia Tanzania kwa miaka mingi kumpangia matumizi ya fedha ya fedha yake kwa kumpa asilimia 25 huku asilimia 75 unasema utamlipa polepole.

Bulaya amesema Uongozi wa Hayati Dkt. Magufuli ulilazimisha kuweka mfumo mbovu na wa kinyanyasaji na hata ripoti ya Waziri Mkuu iliyosomwa jana Bungeni haisemi wazi ni kwa namna gani Serikali itatatua malalamiko ya Wafanyakazi katika Mafao yao.

Aidha, ameitaka Serikali kuacha kuchukua mikopo kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwasababu fedha hizo sio za Serikali bali wao ni watunzaji tu.
 
Aidha, ameitaka Serikali kuacha kuchukua mikopo kwenye Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwasababu fedha hizo sio za Serikali bali wao ni watunzaji tu.
Serikali haitakiwi kuchukua hata senti. Kenya walipiga vita hilo suala na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia shirikisho lao la wafanyakazi. Sisi TUCTA yetu ina wana-ccm tu na vibaraka kibao washenzi tu
 
Mbunge wa Viti Maalum, Esther Bulaya, amesema sio sawa kwa Mtumishi aliyeitumikia Tanzania kwa miaka mingi kumpangia matumizi ya fedha ya fedha yake kwa kumpa asilimia 25 huku asilimia 75 unasema utamlipa polepole...
Namuunga mkono huyo mbunge namwona ndiye mtetezi maana tangue enzi za hayati utetezi wake kwa michango ya wafanyakazi kwenye mifuko ya jamii haiwanufaishi.

Napendekeza asilimia 80% ilipwe kwa mkupuo kwa mstaafu bila amasharti na asilimia 20% ndio ilipwe kidogo kidogo ili mwenye nacho aiwekeze kwa manufaa ya familia yake.
 
Safi sana kwa hoja hiyo maana ni unyanyasaji mkubwa kumpangia mtu matumizi ya pesa zake... Nashauri mambo yawe kama zamani.. mtu apewe pesa yake yote ajue atakachofanyia maana ni jasho lake na sio la serikali..
 
Serikali haitakiwi kuchukua hata senti. Kenya walipiga vita hilo suala na wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kupitia shirikisho lao la wafanyakazi. Sisi TUCTA yetu ina wana-ccm tu na vibaraka kibao washenzi tu
Na wanao umiza watumishi ni wanasiasa ambao wamewahi kuwa watumishi wa umma. Wakiingia ktk siasa wanageuka wachawi.
 
1618448055866.png

Bado mnauliza hawa ni wabunge wa chama gani?
 
Back
Top Bottom